2024
Siku Ambazo Kamwe Hazitasahaulika
Novemba 2024


Kikao cha Jumapili Asubuhi

Siku Ambazo Kamwe Hazitasahaulika

Dondoo

bango

Pakua PDF

Kati ya sasa, 2024 na 2034, tutapata uzoefu wa matukio muhimu ambayo yataleta fursa zisizo kifani za kutumikia, za kuungana na waumini na marafiki na za kutambulisha Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kwa watu wengi zaidi kuliko hapo kabla. …

Kwa sababu ya hilo, ninatamani kuzungumza nanyi enyi wa kizazi kinachoinukia, kuwaalika kupata taswira ya jinsi muongo huu ujao wa kusisimua, ambao hautasahaulika kamwe unavyoweza kuwa kwenu ninyi. …

… Kwako binafsi, huu utakuwa muongo usiosahaulika kamwe. Lakini itakuwa mara mbili ya hayo ikiwa kwa ari utajitahidi kuwa nuru ya ulimwengu ya jinsi habari njema ya Yesu Kristo inavyoweza kurutubisha na kustawisha si tu maisha yako bali pia yale ya familia yako, marafiki na wafuasi wa mitandao ya kijamii.

Unaweza ukawa unajiuliza jinsi ya kufanya hili. …

Kwanza, ishi Injili ya Yesu Kristo. …

Pili, fikia kwa huruma ili kuwajali wenye mahitaji. …

Tatu, waalike wote waipokee injili. …

Nne, ziunganishe familia kwa milele yote. …

Wapendwa kaka zangu na dada zangu, marafiki zangu wapendwa vijana, yawezekana kukawepo na magumu kwa kila mmoja wetu katika siku za mbeleni. Hata hivyo, tunapouingia muongo huu wa nyakati zisizo na kifani, na tushiriki habari njema kupitia shughuli rahisi za kuishi, kujali, kualika na kuunganisha. Tunapofanya hivyo, Bwana atatubariki kwa uzoefu usiosahaulika kamwe.