2024
Ushindi wa Tumaini
Novemba 2024


Kikao cha Jumamosi Asubuhi

Ushindi wa Tumaini

Dondoo

bango

Pakua PDF

Kipawa cha tumaini ni endaumenti ya thamani kuu kutoka kwa Mungu. …

Tunapoimarisha imani yetu katika Yesu Kristo, tunaona zaidi ya mapambano yetu hadi kwenye baraka na ahadi za umilele. Kama nuru ambayo uangavu wake unakua, tumaini linaangaza ulimwengu ulio na giza, na tunaona siku zetu tukufu za usoni. …

Kaka zangu na dada zangu, tumaini ni zawadi hai, zawadi ambayo hukua tunapoongeza imani yetu katika Yesu Kristo. … Tunajenga kiini hiki—matofali ya ushahidi wa imani yetu—kupitia sala, maagano ya hekaluni, kushika amri, kuendelea kusherehekea maandiko na maneno ya manabii wa siku za leo, kupokea sakramenti, kuwahudumia wengine, na kuabudu kila wiki na Watakatifu wenzetu.

Ili kuimarisha tumaini letu katika wakati wa ongezeko la maovu, Bwana amemwelekeza nabii Wake kuifanya dunia iwe na mahekalu Yake. …

Hakuna maumivu, magonjwa, hakuna udhalimu, hakuna mateso, hakuna kitu chochote kinachoweza kutia giza tumaini letu pale tunapoamini na kushikilia kwa nguvu maagano yetu pamoja na Mungu katika nyumba ya Bwana. Ni nyumba ya nuru, nyumba ya tumaini. …

Akina kaka na akina dada, amani unayoitafuta inaweza isije haraka kadiri unavyoitaka, lakini ninakuahidi kwamba unapomtumaini Bwana, amani Yake itakuja.

Na tukuze imani yetu ya thamani, tukisonga mbele tukiwa na mng’aro mkamilifu wa tumaini. Ninashuhudia kwamba tumaini letu ni Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Kupitia Yeye, ndoto zetu zote za haki zitapatikana. Yeye ni Mungu wa tumaini—ushindi wa tumaini. Yeye yu hai na anakupenda.