Kikao cha Jumapili Asubuhi
Ee Vijana wa Haki Tukufu ya Uzaliwa
Dondoo
Haki ya mzaliwa wa kwanza! … Ni neno la kuvutia. Lakini lina maana gani? …
… Tunazungumza kuhusu urithi unaopokea kama mrithi pamoja na Kristo kwa sababu ya uhusiano wa agano ambao umechagua kuingia pamoja Naye na Baba yako wa Mbinguni. …
Fikiria hilo! Mungu anakuamini—kati ya watu wote duniani, watoto wa agano, wafanyakazi Wake—kusaidia katika kazi Yake ya kuwaleta watoto Wake wote salama nyumbani Kwake. …
… Wewe ni wa uzao mtukufu. Uhusiano wako wa agano na Mungu na Yesu Kristo ni uhusiano wa upendo na tumaini ambapo unaweza kufikia kiwango kikubwa cha neema Yao—Msaada Wao wa kiungu, endaumenti ya nguvu, na nguvu ya kuwezesha. Nguvu hiyo si tu fikra za kutamanika, haiba ya bahati au unabii wa kujitimiza. Ni halisi.
Unapotimiza majukumu yako ya mzaliwa wa kwanza, hauko peke yako kamwe. … Unafanya kazi bega kwa bega na Yesu Kristo. Kwa kila agano jipya—na kadiri uhusiano wako na Yeye unavyozidi kuongezeka—mnashikiliana kwa nguvu na kwa nguvu zaidi mpaka mnapofungamana kwa uimara pamoja. Katika ishara hiyo takatifu ya neema Yake, utapata vyote, tamanio na nguvu ya kuishi jinsi hasa Mwokozi alivyoishi—tofauti na ulimwengu. Unaweza hili kwa sababu Yesu Kristo yuko nawe! …
… Usiruhusu ulimwengu ukubadilishe wakati ulizaliwa ili kuubadilisha ulimwengu.