Kikao cha Jumapili Asubuhi
“Ni Mimi”
Dondoo
Kote katika historia wengi wamerahisisha, hata kushusha thamani ya mfano wetu kumhusu [Yesu Kristo] na ushahidi Wake wa Yeye ni nani. Wameshusha thamani ya wema Wake kuwa kitu cha kujidai, haki Yake kuwa hasira, rehema Yake kuwa uhuru. Sisi hatupawi kuwa wenye hatia juu ya mitazamo hiyo miepesi kumhusu Yeye ambayo inapuuza mafundisho tunayoyaona kuwa magumu kwetu. “Upuuzi” huu umekuwa wa kweli hata kuhusu wema Wake wa juu, upendo Wake.
Wakati wa huduma Yake duniani, alifundisha kwamba kuna amri mbili kuu. … “Mpende Bwana Mungu wako [na] mpende jirani yako kama nafsi yako.” Ikiwa sisi tutamfuata Mwokozi kwa uaminifu katika hizi sheria mbili muhimu zilizoungana bila kutenganishwa, tunapaswa kushikilia kwa nguvu kile ambacho Yeye hasa alikisema. Na kile ambachoYeye hasa alikisema kilikuwa, “Kama wanipenda, zishike amri zangu.” Jioni ile ile, Yeye alisema “pendaneni; kama nilivyowapenda ninyi.” …
… Je, Yesu alipenda vipi?
Kwanza, Yeye alipenda kwa “moyo [Wake] wote, uwezo, akili na nguvu,” ikimpatia Yeye uwezo wa kuponya maumivu ya kina na kutangaza uhalisia mgumu zaidi. …
Sifa ya pili ya hisani ya Yesu ilikuwa ni utiifu Wake kwa kila neno litokalo kinywani mwa Mungu, daima akiwianisha mapenzi na tabia Yake kwa ile ya Baba Yake wa Mbinguni. …
… Tutakaposimama mbele Yake na kuona vidonda katika mikono Yake na miguu, tutaanza kuelewa kile ilichomaanisha Kwake kubeba dhambi zetu na kuzoea huzuni, kuwa mtiifu kikamilifu kwa mapenzi ya Baba Yake—yote hayo kwa sababu ya upendo safi kwetu.