2024
Kutafuta Majibu ya Maswali ya Kiroho
Novemba 2024


Kikao cha Jumapili Asubuhi

Kutafuta Majibu ya Maswali ya Kiroho

Dondoo

bango

Pakua PDF

Kuuliza maswali na kutafuta maana ni sehemu ya asili na ya kawaida ya uzoefu wetu wa maisha. … Mpango wa Mungu ni wa rehema kwa vizuizi vya ubinadamu wetu; unatupatia Mwokozi wetu, Yesu Kristo, kuwa Mchungaji wetu Mwema; na kutupatia msukumo wa kutumia haki yetu ya kujiamulia kumchagua Yeye. …

Njia ya Mungu Baba na Mwanaye ya kutupatia hekima Yao huwekea kipaumbele kualika nguvu ya Roho Mtakatifu kuwa mwalimu wetu binafsi pale tunapomweka Yesu Kristo kuwa kiini katika maisha yetu na katika utafutaji wetu wa dhati wa majibu Yao na maana Yao. …

… Bwana ametuambia kwamba kupitia utiifu wetu na bidii, tunaweza kupata maarifa na akili. Sheria na amri za Mungu hazijakusudiwa kuwa vikwazo katika maisha yetu bali njia yenye nguvu kuelekea ufunuo na elimu binafsi ya kiroho. …

… Tumebarikiwa kuwa na Yesu Kristo kama Mponyaji wetu Mkuu. Utiifu wetu kwenye sheria na amri za Mungu unaweza kufungua njia kwa ajili ya Mwokozi wetu kutoa uelewa na uponyaji anaojua tunauhitaji, kulingana na mpango Wake wa tiba uliopendekezwa kwetu.

Marafiki wapendwa, ninashuhudia kwamba maswali yetu ya dhati ya injili yanaweza kutoa fursa kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kutusaidia tukue. … Ninashuhudia kwamba kuweka tumaini lako kwa Baba wa Mbinguni na kwa manabii Wake aliowatuma watakusaidia kuinuka kiroho na kukusukuma mbele kuelekea uwanda mpana wa Mungu.