Kikao cha Jumamosi Asubuhi
Kumfuata Kristo
Dondoo
Kumfuata Kristo siyo zoezi la juujuu au la mara moja moja. Ni dhamira endelevu na njia ya maisha ambayo inapaswa kutuongoza nyakati zote na katika mahali popote. Mafundisho Yake na mifano Yake huonesha njia kwa ajili ya kila mwanafunzi wa Yesu Kristo. …
Amri za Mungu zinatoa mwongozo na nguvu za kuimarisha katika maisha yetu. …
Lingine katika mafundisho ya Mwokozi wetu linaonekana kuhitaji kusisitizwa tena katika hali za siku yetu.
Huu ni wakati wa maneno mengi makali na ya kuumiza katika mawasiliano ya umma na hata wakati mwingine katika familia zetu. …
Je, wafuasi wa Kristo wanapaswa kufundisha nini na kufanya nini katika wakati huu wa mawasiliano yenye sumu? Je, mafundisho na mifano Yake ilikuwa ipi? …
… Tunajitahidi kuwapenda na kutenda mema kwa wote. Tunahitaji kuepukana na ubishi na kuwa wapatanishi katika mawasiliano yetu yote. Hii haimaanishi kulegeza misingi yetu na vipaumbele vyetu bali kuacha kuwashambulia wengine kwa ukali kwa sababu ya misingi yao na vipaumbele vyao. Hicho ndicho Mfano wetu Mkamilifu alichofanya katika huduma Yake. Huo ndio mfano Yeye aliotuwekea wakati alipotualika tumfuate Yeye. …
Kama wafuasi wa Kristo, tunafundisha na tunashuhudia juu ya Yesu Kristo, Mfano wetu Mkamilifu. Kwa hiyo acha tumfuate Yeye kwa kuachana na ubishi. Tunapofuata sera zetu pendwa katika vitendo vya umma, acha tustahili kwa ajili ya baraka Zake kwa kutumia lugha na mbinu za wapatanishi. Katika mahusiano ya familia zetu na binafsi, acha tuepukane na kile kilicho cha ukali na chenye chuki.