Kikao cha Jumamosi Jioni
Utakatifu kwa Bwana katika Maisha ya Kila Siku
Dondoo
Kote kutuzunguka sisi kuna fursa za kucheka, kufurahia, kuona kwa macho ya shukrani. Yetu ni injili ya shangwe na utakatifu kila siku ya maisha. Utakatifu hubainisha vitu kwa ajili ya dhumuni takatifu. Lakini utakatifu pia unatualika sisi kujaza maisha ya kila siku kwa utakatifu—kushangilia katika mkate wa kila siku katikati ya mibaruti na miiba ya ulimwengu. Ili kutembea na Bwana, lazima tuwe watakatifu, kwani Yeye ni mtakatifu, na ili kutusaidia sisi kuwa watakatifu, Bwana anatualika kutembea pamoja na Yeye.
Kaya ya watu wa imani na jumuiya ya Watakatifu zinaepukana na kutengwa na kuepuka umati mpweke. Utakatifu kwa Bwana unasema hapana kwenye lugha chafu, hapana kwenye ujanja wenye hila za kuhujumu wengine, hapana kwenye mambo ambayo huzalisha hasira na ubaguzi. Utakatifu kwa Bwana unasema ndiyo kwenye utakatifu na staha, ndiyo kwenye kuwa kwetu huru zaidi, wenye furaha zaidi, wakweli zaidi, toleo letu bora zaidi kadiri tunavyomfuata Yeye katika imani.
Utakatifu kwa Bwana hufanya maisha yetu ya kila siku kuwa matakatifu. Hutuleta karibu zaidi na kuwa wenye furaha zaidi kwa Bwana na kwa kila mmoja na hutuandaa kuishi na Mungu Baba yetu, Yesu Kristo na wale tuwapendao.
Tunaweza kuhisi upendo Wake pale tunapofanya utakatifu kwa Bwana kuwa wetu kila siku, kwa furaha na kwa milele yote.