Kikao cha Jumamosi Asubuhi
“Hii Ni Injili Yangu”—“Hili Ni Kanisa Langu”
Dondoo
Kama vile tu baruti pasipo nitroglycerin haikuwa na umuhimu, Kanisa la Mwokozi ni maalumu tu endapo litakuwa limejengwa juu ya injili Yake. Pasipo injili ya Mwokozi na mamlaka Yake ya kusimamia ibada zake, Kanisa halingekuwa la kipekee.
Pasipo matokeo ya udhibiti ya kielselguhr, nitroglycerin ilikuwa na thamani yenye ukomo kama kilipuzi. Kama historia inavyoonyesha, pasipo Kanisa la Bwana, uelewa wa mwanadamu juu ya injili Yake pia haukuwa thabiti—ukihatarishwa na anguko la mafundisho na kuwa kwenye ushawishi wa dini tofauti tofauti, tamaduni na falsafa. …
Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho linawezesha ufikiaji wa nguvu za Mungu kwa sababu limeruhusiwa na Yeye katika vyote kufundisha mafundisho ya Kristo na kutoa ibada za kuokoa na kuinuliwa za injili. Mwokozi anatamani kutusamehe dhambi zetu, kutusaidia tufikie nguvu Zake na kutubadilisha. Yeye aliteseka kwa ajili ya dhambi zetu na anasubiri kwa hamu kutusamehe kutokana na adhabu ambayo vinginevyo tungeistahili. Yeye anatutaka tuwe watakatifu na tukamilishwe ndani yake. …
Ninakualika ujitoe kwa dhati zaidi kwa Mwokozi, injili Yake na Kanisa Lake. Unapofanya hivyo, utatambua kwamba muunganiko wa injili ya Mwokozi na Kanisa Lake unaleta nguvu katika maisha yako. Nguvu hii ni zaidi ya ile ya baruti. Itapasua mawe yaliyo katika njia yako, itakubadilisha kuwa mrithi katika ufalme wa Mungu. Na wewe “utajazwa na hiyo shangwe ambayo haiwezi kuelezeka na iliyojaa utukufu.” [Helamani 5:44].