“Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara,” EnglishConnect kwa ajili ya Walimu (2023)
“Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara,” EnglishConnect kwa ajili ya Walimu
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Hapo chini kuna baadhi ya maswali kuhusu EnglishConnect. Maswali yanayoulizwa mara kwa mara ya ziada kwa ajili ya wanafunzi, walimu na viongozi yanaweza kupatikana kwenye englishconnect.org/help.
Je, ninahitaji uzoefu wa kufundisha ili kuwa mwalimu wa EnglishConnect?
Ni kwa jinsi gani nitawafundisha wanafunzi kama sijui lugha yao?
Je, tunaweza kuongea lugha ya mama wakati wa kikundi cha mazungumzo?
Ni kwa jinsi gani nitaweza kuwafundisha kikundi chenye lugha nyingi tofauti?
Ni kwa jinsi gani nitaweza kuwasaidia wanafunzi kufanya mazoezi ya Kiingereza kila siku?
Ni kwa jinsi gani nitaweza kukipanga kikundi cha EnglishConnect?
Je, mkutano wa kikundi cha EnglishConnect unachukua muda gani?
Je, kikundi changu kinapaswa kukukatana mara ngapi?
Je, ninaweza kufundisha zaidi ya somo moja katika mkutano wa kikundi?
Ni kwa jinsi gani nitajua ni daraja gani la EnglishConnect mwanafunzi anahitaji kujiunga nalo?
Ni kwa jinsi gani nitamsaidia mwanafunzi anayejiunga na kikundi ambacho tayari kinaendelea?
Je, itakuaje kama mwanafunzi anakosa mkutano wa kikundi au anaacha kuja?
Ni kwa jinsi gani nitawasaidia wanafunzi ambao wanajifunza kwa kasi zaidi?
Ni kwa jinsi gani nitawasaidia wanafunzi ambao wana uwezo tofauti wa kuongea Kiingereza.
Je, nitafanya nini wakati mwanafunzi anauliza maswali kuhusu sarufi?
Je, ninapaswa kusahihisha matamshi?
Ni kwa jinsi gani nitasajili na kusimamia kikundi changu cha EnglishConnect?
Ni kwa jinsi gani wanafunzi watapokea vyeti vyao vya EnglishConnect?
Je, ninahitaji na uzoefu wa ufundishaji ili kuwa mwalimu wa EnglishConnect?
Hauhitaji kuwa na uzoefu wa kufundisha ili kuwa mwalimu wa EnglishConnect. Labda wewe kamwe haujafunza Kiingereza awali na unahisi wasiwasi jinsi ya kuanza. Hiyo ni sawa. Masomo ya EnglishConnect yamesanifiwa kwa umakini na uangalifu kwa kutumia kanuni za ufundishaji wa lugha na kanuni za kiroho ili kukusaidia kufanikiwa. Hauhitaji kuwa mbobezi. Hauhitaji kuwa unajua jibu la kila swali. Wajibu wako ni kuendeleza ukuzaji wa lugha kwa kutoa msaada kwa ajili ya mazoezi. Hauhitaji kufundisha sarufi au kuelewa kila kitu kuhusu Kiingereza. Badala yake fokasi katika kutengeneza mazingira ambayo wanafunzi wanaweza kuhisi faraja kuongea Kiingereza na kujifunza kutokana na makosa yao.
Ni kwa jinsi gani nitawafundisha wanafunzi kama sijui lugha yao?
Kufundisha Kiingereza ukitumia tu Kiingereza ni kawaida sana kote ulimwenguni. Kwa kweli, hii inaweza kuwa baraka kwa sababu huongeza kiasi cha Kiingereza ambacho wanafunzi wanasikia na kutumia. Kumbuka kuongea kwa Kiingereza rahisi. Tumia picha, ishara za mikono na lugha ya mwili ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa msamiati wa maneno na mipangilio. Unaweza kuonyesha picha, kuchora picha au kuiigiza. Unaweza kuwaelekeza wanafunzi kwenye nyenzo zilizotafsiriwa katika EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi au EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi, au unaweza kutumia kamusi ya mtandaoni. Hii pia itawafundisha wanafunzi jinsi ya kutumia nyenzo zilizopo ili kupata majibu. Epukana na ufafanuzi mrefu. Badala yake, kwa urahisi waonyeshe wanafunzi kile cha kufanya kwa kufanya maonyesho.
Kumbuka kwamba mnajifunza pamoja. Mara kwa mara waalike wanafunzi kumgeukia Bwana kwa ajili ya usaidizi. Kama mwalimu wao, unaweza kuwa mfano wa imani na juhudi. Kuongea Kiingereza na wanafunzi ni tendo la imani. Bwana atakubariki wewe na wanafunzi mnapotenda kwa imani kuongea Kiingereza.
Je, tunaweza kuongea lugha enyeji wakati wa kikundi cha mazungumzo?
Utawasaidia wanafunzi sana unapofokasi juu ya kuongea Kiingereza kote katika kikundi cha mazungumzo. Unaweza kufanya hivi kwa kuweka mfano. Fanya kadiri uwezavyo kuongea Kiingereza. Tumia maneno rahisi na sentensi fupi. Zungumza polepole na urudie maneno na virai mara kwa mara. Andika maneno na virai muhimu ubaoni. Unaweza pia kutumia picha, kuchora picha au kuigiza. Epukana na ufafanuzi mrefu na kutafsiri kila kitu unachosema. Kama itabidi utumie lugha ya mama, omba ruhusa kwanza na utumie lugha ya mama kidogo inavyowezekana na kisha urudi kwenye Kiingereza. Wahimize wanafunzi kuongea Kiingereza sana kadiri wanavyoweza na wasiogope kufanya makosa. Wasaidie wao kupata ufanisi na pongeza kila juhudi. Kama wanafunzi wanahitaji msaada zaidi, waelekeze wao kwenye vitabu vya kiada vya mwanafunzi, ambapo wanaweza kupata nyenzo katika lugha yao ya mama. Unapofokasi juu ya kuwasaidia wanafunzi kujifunza kwa kutenda, utakuwa na jukumu dogo la kutumia lugha ya mama.
Ni kwa jinsi gani nitaweza kufundisha kikundi chenye lugha nyingi tofauti?
Kufundisha kikundi chenye lugha nyingi tofauti ni nafasi nzuri ya kuwahimiza kuongea Kiingereza kwa sababu Kiingereza ni lugha ya kawaida katika kikundi. Kama mwalimu, tumia toleo la Kiingereza la kitabu cha kiada. Wasaidie wanafunzi kutumia kitabu cha kiada cha mwanafunzi katika lugha yao ya mama, kama kinapatikana, ili waweze kufaidika kutokana na tafsiri. Kama inawezekana, waweke wanafunzi katika vikundi vidogo ili kujadili kanuni ya kujifunza katika lugha yao ya mama, lakini hakikisha hakuna hata mmoja ametengwa. Kama kuna mtu mmoja tu anayezungumza lugha fulani katika kikundi, acha hicho kikundi kijadili kanuni ya kujifunza katika Kiingereza rahisi ili kwamba wote wajumuishwe.
Ni kwa jinsi gani nitaweza kuwasaidia wanafunzi kufanya mazoezi ya Kiingereza kila siku?
Ili kujifunza Kiingereza, wanafunzi wanahitaji kukuza tabia ya kufanya mazoezi kila siku. Wahimize wanafunzi kuwa na tabia hii kwa kutafuta njia rahisi za kujumuisha Kiingereza katika shughuli zao za kila siku (ona sehemu ya “Mazoezi ya Kila Siku”). Kwa mfano, wanafunzi wanaweza kuchagua kutazama maonyesho au kusikiliza muziki kwa Kiingereza. Unaweza kuwahimiza wanafunzi kutumia orodha ya mawazo ili kuboresha kujifunza kila siku inayopatikana kwenye “Personal Study Tracker” katika utangulizi wa kitabu cha kiada cha mwanafunzi. Tumia orodha hii ili kuwapa mwongozo wanafunzi kupata njia za ubunifu zenye maana za kufanya mazoezi kila siku.
Wakati wa mkutano wa kikundi, waalike wanafunzi kujifunza na kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku na kufuatilia juhudi zao. Ungeweza kuwauliza wanafunzi wachache kushiriki mambo mahususi waliyofanya katika mazoezi ya kila siku. Ungeweza kufikiria kutengeneza mahali mtandaoni, kama vile chati ya kikundi, kwa ajili ya wanafunzi katika kikundi. Shauriana na viongozi wako ili kupata njia zifaazo za kusaidia kikundi kubaki kimeungana wakati wa wiki kupitia jumbe za kikundi au njia zingine. Unaweza kuwasaidia wanafunzi wanapofanya kazi kufikia malengo yao, lakini kumbuka, wao ndiyo kimsingi wana jukumu kwa ajili kujifunza kwao wenyewe.
Ni kwa jinsi gani nitaweza kukipanga kikundi cha EnglishConnect?
Shauriana na uongozi wa tawi/kata husika ya Kanisa ili kufanya maamuzi kuhusu upangaji na uendeshaji wa vikundi vya EnglishConnect. Kwa kawaida, walimu wawili watu wazima wanapangiwa kwa kila kikundi. Fikiria mahitaji ya wanafunzi na uwezo wa sehemu husika unapofanya chaguzi kuhusu mahali, ratiba na kasi ya kujifunza.
Je, mkutano wa kikundi cha EnglishConnect huchukua muda gani?
Masomo ya EnglishConnect yanaweza kuwa takribani dakika 60 hadi 90. Fuata muda uliyoorodheshwa kwa ajili ya kila shughuli. Usiondoe shughuli yoyote; tumia muda mchache uliopendekezwa kwa ajili ya mkutano mfupi wa kikundi na utumie muda mrefu uliopendekezwa kama muda unaruhusu.
Muhimu: Shauriana na wale ambao wanasimamia mpango huu na fikiria mahitaji ya wanafunzi na uwezo wa sehemu husika unapofanya maamuzi haya.
Je, kikundi changu kinapaswa kukukatana mara gapi?
Kawaida, vikundi hukutana mara moja kwa wiki. Kama wakipenda, vikundi vinaweza kukutana mara nyingi zaidi. Ili mikutano ya kikundi iwe na ufanisi zaidi, wanafunzi wanahitaji kuwa na muda wa kutosha kati ya mikutano ili kukamilisha sehemu ya “Personal Study.”
EnglishConnect 1 na 2 kila moja ina masomo 25. Kama vikundi vinakutana mara moja kwa wiki, itachukua miezi sita kukamilisha daraja ya kwanza. Kama vikundi vinakutana mara mbili kwa wiki, itachukua miezi mitatu. Kama unapenda, unaweza kugawa mpango kwenye sehemu ndogo, au masomo. Kwa mfano, unaweza kuchagua kuanzisha kikundi ambacho kitakutana kwa miezi mitatu tu mara moja kwa wiki ili kukamlisha sehemu ya 1 hadi 3. Ukitumia njia hii unaweza kuwasaidia wanafunzi kubakia wenye dhamira.
Muhimu: Wakati unaratibu mkutano wa kikundi ambacho hakianzii na sehemu ya 1, fikiria kuanzia ratiba ya masomo ya kikundi chako na somo la 1. Hii itawazoesha wanafunzi jinsi ya kutumia kitabu hiki cha kiada Shauriana na wale ambao wanasimamia mpango huu na fikiria mahitaji ya wanafunzi na uwezo wa sehemu husika unapofanya maamuzi haya.
Je, nitaweza kufundisha zaidi ya somo moja katika mkutano wa kikundi?
Kama watapenda, vikundi vinaweza kufanya zaidi ya somo moja katika mkutano wa kikundi. Kwa ajili ya mikutano kuwa na ufanisi zaidi, wanafunzi wanahitaji kuwa na muda wa kutosha kabla ya mikutano ili kukamilisha sehemu ya “Personal Study” ya kila somo.
Ona “Je, kikundi changu kinapaswa kukukatana mara gapi?” kwa maelezo zaidi kuhusu ratiba na kasi ya somo.
Ni kwa jinsi gani nitajua ni daraja gani la EnglishConnect mwanafunzi anapaswa kujiunga nalo?
EnglishConnect 1 inahitaji mtu ajue kusoma na kuandika katika lugha ya mama na uwezo wa kusoma herufi za Kiingereza na maneno ya msingi ya Kiingereza. EnglishConnect 2 ni kwa ajili wanafunzi ambao wanaweza kusema sentensi za msingi na kujibu maswali ya msingi kwa Kiingereza. Ili kuamua kama mwanafunzi anapaswa kujiunga na EnglishConnect 1 au EnglishConnect 2, unaweza kutumia usaili wa uhodari wa kunena katika kiambatisho B.
EnglishConnect 3 ni kozi ya wastani ambayo huwasaidia wanafunzi kukuza ujuzi wa kimasomo wa lugha ya Kiingereza. Ili kujiunga na EnglishConnect 3, wanafunzi lazima watume maombi na kupata alama za kuhitimu kwenye mtihani wa upangaji. Wanafunzi wanaweza kutuma maombi kwenye engelishconnect.org/join.
EnglishConnect 3 ni Nini?
EnglishConnect ina madaraja mengi tofauti ya kuwasaidia washiriki kupiga hatua. EnglishConnect 1 na 2 zinawasaidia wanafunzi kukuza ujuzi wa msingi wa lugha ya Kiingereza. EnglishConnect 3 ni kozi ya wastani ambayo huwasaidia wanafunzi kukuza ujuzi wa kimasomo wa lugha ya Kiingereza. Inawasaida wanafunzi kujiandaa kwa ajili ya BYU-Pathway Worldwide. (Jifunze zaidi kuhusu BYU–Pathway Worldwide kwenye byupathway.org.)
EnglishConnect 3 ni kozi ya gharama nafuu ya mtandaoni ya mazungumzo inayofanywa mtandaoni au katika jengo la mikutano la eneo husika. EnglishConnect 3 inajumuisha nyenzo za kujifunza mtandaoni zilizo na mrejesho binafsi kwa kila mtu katika kusikiliza, kuongea, kusoma na kuandika. Wanafunzi wanaweza kusonga mbele katika kozi kulingana kasi yao wenyewe. Wanafunzi wanaweza kurudia EnglishConnect 3 mara nyingi wanavyopenda ili kutimiza malengo yao. Kuhitimu EnglishConnect 3 kunawaruhusu wanafunzi kuachana na upimaji wa Kiingereza wakati wa kutuma maombi ya BYU–Pathway Worldwide.
Ili kujiandaa kwa ajili ya EnglishConnect 3 wanafunzi wanapaswa kukamilisha EnglishConnect 1 na 2—ikijumuisha shughuli za kitabu cha kazi, hasa katika shughuli za kusoma na kuandika. Wahimize wanafunzi wa EnglishConnect 2 kutuma maombi kwenye engelishconnect.org/join.
EnglishConnect 3 inatolewa kupitia BYU–Pathway Worldwide kwa pamoja na viongozi wa eneo husika na wamisionari wa huduma wa Kanisa. Viongozi wanaopendelea wanaweza kufanya kazi pamoja na mameneja wa ustawi na kujitegemea katika eneo lao ili kufundisha EnglishConnect 3 katika maeneo yao.
Ni kwa jinsi gani nitamsaidia mwanafunzi kujiunga na kikundi ambacho tayari kinaendelea?
Masomo yamesanifiwa ili kwamba wanafunzi wapya waweze kujiunga na kikundi cha EnglishConnect wakati wowote. Kama wanafunzi wanataka kujiunga baada ya vikundi kuwa tayari vimeanza, wakaribishe, wapatie EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi au EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi (au kuwaonyesha wao jinsi ya kupata kitabu cha kiada katika Maktaba ya Injili), na kuwasaidia wao kushiriki. Wewe au mwanafunzi mwingine anaweza kuwasaidia wanafunzi wapya kuunganika na kikundi kwa kuwaonyesha wao jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya somo lifuatalo. Pia, wanafunzi wanaweza kuchagua kurudia daraja kama wanahitaji mazoezi zaidi.
Je, itakuaje kama mwanafunzi anakosa mkutano wa kikundi au anaacha kuja?
Wakati mwingine wanafunzi wana changamoto ambazo zinafanya iwe vigumu kuhudhuria kikundi, na mara kwa mara wanasita kurudi tena kwa sababu ya kuabika au woga. Wanaweza kudhania kwamba wamekosa mengi sana na hawawezi kuwafikia wanaohudhuria. Wafikie na waalike wanafunzi waliokosa kuhudhuria waje kwenye somo linalofuata bila kujali mara ngapi wamekosa kuhudhuria. Toa usaidizi na uhamasishaji. Wahakikishie wao kwamba EnglishConnect imesanifiwa ili kwamba wanafunzi waweze kujiunga wakati wowote. Wanafunzi wanaweza kuanza tena kwa kuhudhuria kikundi na kujiandaa kwa ajili ya somo linalofuata. Fikiria kumwalika mshiriki moja au zaidi wa kikundi kuwasiliana na wanafunzi waliokosa kuhudhuria na kuonyesha kuwaunga mkono.
Muhimu: Hupaswi kushiriki taarifa za mawasiliano za mtu bila ruhusa yao ya maandishi.
Ni kwa jinsi gani nitawasaidia wanafunzi ambao wanajifunza kwa kasi ndogo kuliko wengine katika kikundi?
Baadhi ya wanafunzi wanahitaji muda zaidi kuelewa na kuongea lugha. Wanafunzi hawa watafaidika sana kutokana na kukamilisha sehemu ya “Personal Study” Kabla ya kushiriki katika kila kikundi cha mazungumzo. Waalike wao kufanya mazoezi ya msamiati na mipangalio ya sentensi kabla ya kikundi kukutana. Wakati wa somo, waweke wanafunzi katika jozi kukiwa na wanafunzi wengine ambao wanaweza kutoa uhamasisho na usaidizi. Wahimize wanafunzi wote kufanya mengi kadri wanavyoweza na kukubali makosa kama sehemu ya mchakato wa kujifunza. Unaweza pia kuchagua kupitia tena na kurudia shughuli. Wakumbushe wanafunzi wote kwamba kukamilisha sehemu ya “Personal Study” kabla ya kushiriki katika kikundi cha mazungumzo kinachofuata ni muhimu katika maendeleo yao.
Ni kwa jinsi gani nitawasaidia wanafunzi ambao wanajifunza kwa kasi zaidi?
Unapojihusisha na wanafunzi, unaweza kutambua kwamba baadhi wanaelewa vyema na wanaweza kukamilisha shughuli za mazoezi kwa urahisi. Fikiria kuwachochea wanafunzi hawa kukuza kwa kina kujifunza kwao kwa kujumuisha maelezo zaidi au kufanya shughuli ile ile katika muktadha tofauti. Kwa mfano, wakati wanafunzi wanafanya mazoezi ya kukutana na mtu, waombe wao wafanye mazoezi ya kukutana na rafiki mpya au mwajiri mpya. Wanafunzi hawa wanaweza pia kuimarisha maarifa yao ya Kiingereza kwa kuwasaidia wanafunzi ambao wanajifunza kwa mwendo wa polepole. Wanafunzi wote wanaweza kufaidika kwa kumfundisha mwenza na kuwasaidia wengine kufanyia mazoezi msamiati na mipangilio katika Kiingereza.
Ni kwa jinsi gani nitawasaidia wanafunzi ambao wana uwezo tofauti wa kuongea Kiingereza.
Kuwa na wanafunzi walio katika viwango tofauti vya uwezo wa kuongea Kiingereza ni kawaida na ni fursa kwa wao kusaidiana. Kusaidiana kunaweza kukuza urafiki na ukuaji. Kila mmoja ana kitu cha kutoa. Kwa mfano, baadhi ya wanafunzi wanaweza kusaidiana kuhisi kujiamini kwa sababu wako tayari kufanya makosa. Waweke wanafunzi katika jozi katika njia tofauti. Unaweza kuwaweka wanafunzi katika jozi na mtu aliye katika kiwango sawa ili kuwasaidia wao kupanua uwezo wao pamoja. Au unaweza kuwaweka wanafunzi katika jozi na mtu aliye katika kiwango kingine. Wanafunzi wa kiwango cha chini watafaidika kutokana na maoni na usaidizi. Wanafunzi wa kiwango cha juu watafaidika kutokana na kumfundisha mwenza na kuelezea kwa Kiingereza. Kumbuka, kuwa na kikundi kilicho na uwezo tofauti tofauti wa kuongea Kiingereza ni kawaida na inaweza kuwa nafasi nzuri kwa ajili ya wanafunzi kufaidika kutokana na kusaidiana.
Je, nitafanya nini wakati mwanafunzi anauliza maswali kuhusu sarufi?
Badala ya kutoa maelekezo marefu ya sarufi au kutumia muda mwingi kuongea kuhusu kanuni, waelekeze wanafunzi tena kwenye mipangilio. Wanafunzi wanaweza kuepuka kufanya makosa mengi kwa kufuata mipangilio. Kuna ufanisi sana katika kujifunza kwa kufanya mazoezi ya lugha badala ya kuongea kuhusu lugha. Ufafanuzi wowote kuhusu sarufi unapaswa kuwa rahisi, mfupi na wa matendo. Kama unafundisha kanuni, toa mfano wa sentensi na uwaalike wanafunzi kufanya mazoezi ya kutumia kanuni hii. Wanafunzi wanafaidika sana kutokana na kusikia na kufanya mazoezi ya Kiingereza.
Je, ninapaswa kusahihisha matamshi?
Usitumie muda mwingi kusahihisha matamshi? Wakumbushe wanafunzi kwamba kuelewa ni muhimu sana kuliko kuwa na matamshi kamili. Wahimize wanafunzi kufanya mazoezi ya matamshi wakati wa kujifunza kwao binafsi ili waweze kufanya mazoezi katika mwendo wao wenyewe. Kumbuka kwamba kama wanafunzi watajali sana kuhusu matamshi yao wanaweza kusita kufanya mazoezi ya mazungumzo. Wahimize wanafunzi kutumia mada za matamshi mtandaoni kwenye englishconnect.org/learner/resources
Ni kwa jinsi gani nitasajili na kusimamia kikundi changu cha EnglishConnect?
Tumia QuickReg (quickreg.englishconnect.org) ili kusajili kikundi chako cha EnglishConnect. QuickReg ni chombo cha usajili wa kikundi kinachotolewa na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Unaweza kutumia QuickReg:
-
Kutengeneza kikundi: Chagua siku, saa na mahali pa kikundi chako.
-
Kusimamia kikundi: Angalia habari za mshiriki na usasishe habari za kikundi.
-
Kualika watu kushiriki: Kikundi chako kitaorodheshwa mtandaoni kwenye englishconnect.org/join. Unaweza kushiriki kiungo cha kuwaalika watu kujisajili katika kikundi chako.
-
Utoaji vyeti: Mwisho wa kikundi chako, unaweza kupata na kupiga chapa vyeti.
Ni kwa jinsi gani wanafunzi watapokea vyeti vyao vya EnglishConnect?
EnglishConnect 1 na 2: Kwenye hitimisho la kikundi, wanafunzi wanaweza kupokea vyeti vya kushiriki. Viongozi, wataalamu au walimu wanaweza kusambaza vyeti. Baadhi ya nchi zinaweza kuwa haziidhinishi kusambazwa kwa vyeti vya EnglishConnect. Tafadhali pitia tena mahitaji ya kisheria ya nchi husika kabla ya kutoa vyeti (ona englishconnect.org/leader/approved-locations).
Muhimu: Ili kupata na kusambaza vyeti, kikundi chako lazima kisajiliwe katika QuickReg kwenye quickreg.englishconnect.org. (Ona “Ni kwa jinsi gani nitasajili na kusimamia kikundi changu cha EnglishConnect?’ katika sehemu hii ya Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara.)
EnglishConnect 3: Wanafunzi wanaweza kupokea vyeti vya kuhitimu wakati wamemaliza daraja zinazohitajika katika kozi. Kuhitimu EnglishConnect 3 kunawaruhusu wanafunzi kutopitia upimaji wa Kiingereza wakati wa kutuma maombi ya BYU–Pathway Worldwide.