Kujifunza Kiingereza
EnglishConnect ni Nini?


“EnglishConnect ni Nini?,” EnglishConnect kwa ajili ya Walimu (2023)

“EnglishConnect ni Nini?,” EnglishConnect kwa ajili ya Walimu

wavulana watatu wakizungumza na kucheka

EnglishConnect ni Nini?

EnglishConnect ni mpango wa kujifunza Kiingereza unaotolewa na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Madhumuni ya EnglishConnect ni kuwasaidia wanafunzi kukuza ujuzi wa Kiingereza katika mazingira ya imani, urafiki na ukuaji.

EnglishConnect inajumuisha daraja nyingi. EnglishConnect 1 na 2 inawasaidia wanafunzi kukuza ujuzi wa msingi wa lugha ya Kiingereza. Ona “Utangulizi” katika vitabu vya kiada vya mwanafunzi wa EnglishConnect kwa maelezo zaidi. EnglishConnect 3 inawaandaa wanafunzi kwa ajili ya nafasi za masomo—hasa BYU-Pathway Worldwide. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu BYU–Pathway Worldwide kwenye byupathway.org/englishconnect.

tepe nne zinazoonyesha maendeleo kupitia EnglishConnect 1, 2 na 3 hadi BYU–Pathway Worldwide

EnglishConnect inatoa njia ya kuwasaidia wanafunzi kuendelea wanapojiandaa kwa ajili ya ajira, elimu na huduma. Jifunze zaidi kwenye englishconnect.org.