“Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuboresha Ufundishaji Wangu?,” EnglishConnect kwa ajili ya Walimu (2023)
“Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuboresha Ufundishaji Wangu?,” EnglishConnect kwa ajili ya Walimu
Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuboresha Ufundishaji Wangu?
Kama vile tu wanafunzi watavyoboreka baada ya muda, wewe pia utaongezeka katika kujiamini na kuwa bora baada ya muda. Bwana atakuhimili unapowatumikia na kuwasaidia wanafunzi katika kikundi chako. Yeye atakufundisha “mstari juu ya mstari, amri juu ya amri” (2 Nefi 28:30). Amini kwamba Baba wa Mbinguni atakusaidia kadiri unavyomtafuta Roho na kufanya bidii kuwa bora.
Mikakati kwa ajili ya Kufundisha Lugha
Hapo chini kuna baadhi ya mikakati kwa ajili ya kufundisha Kiingereza. Tofauti na madarasa mengine ya lugha ambayo huzingatia kwenye maelekezo ya sarufi, mazoezi mengi ya msamiati au mazoezi ya matamshi, makundi ya mazungumzo ya EnglishConnect yanafokasi kwenye kuwasaidia wanafunzi kutumia lugha katika njia ya zenye maana. Kadiri unavyotumia mikakati hii, utaweza kuwasaidia vyema wanafunzi.
Zungumza Kiingereza
Kuzungumza Kiingereza huwasaidia wanafunzi kupiga hatua na ni njia muhimu ya kutafuta kipawa cha ndimi. Fanya vyema uwezavyo kuzungumza Kiingereza pekee na waalike wanafunzi wafanye vivyo hivyo. Tumia msamiati rahisi na sentensi fupi. Zungumza polepole na urudie maneno na virai kama inavyohitajika. Baada ya kuuliza swali, wape wanafunzi muda wa kufikiria na kujibu. Tumia maneno na mipangilio ambayo wanafunzi wanafanyia mazoezi kwa sasa. Unapoongoza shughuli, unaweza kuwaelekeza wanafunzi kwenye maelekezo ya shughuli iliyotafsiriwa iliyotolewa katika kitabu cha kiada cha mwanafunzi wa EnglishConnect.
Fanya Onyesho la Shughuli
Kuwaonyesha wanafunzi kile cha kufanya mara zote ni msaada mkubwa kuliko kuwaambia wao kile cha kufanya Tumia mazungumzo ya mifano mwanzoni wa kila shughuli ili kuonyesha mfano wa kile wanafunzi watafanya wanapofanya mazoezi. Unaweza kucheza nafasi zote mbili katika mazungumzo, au unaweza kuwaomba wanafunzi kukusaidia katika kufanya onyesho.
Himiza Mazungumzo
Wanafunzi watapa kujiamini na kujifunza haraka zaidi wanapofanya mazoezi wakitumia lugha hii. Usijali kuhusu kusahihisha kila kosa; wasaidie wanafunzi tu kujihusisha na mazungumzo. Simamia muda ili kwamba muda mwingi wa kikundi unatumika katika mazungumzo na mwenza.
Kubali kuwe na Marudiorudio
Mazoezi ya marudiorudio hujenga kujiamini na ufasaha. Wahimize wanafunzi kubadilisha wenza na kufanya zoezi tena. Kubadilisha wenza huwapa wanafunzi nafasi zaidi za kusikiliza na kusema vitu vipya. Wakati wanafunzi wanatumia kile wanachojua na watu tofauti, huwasaidia wao kuimarisha kile wanachojifunza. Pia huongeza kujiamini kwao na kudumisha urafiki.
Wawezeshe Wanafunzi
Wanafunzi wanahitaji kuhisi upendo wako na uhamasisho wako. Wasaidie wanafunzi kushinda hofu kwa kusherekea kila juhudi ya kuzungumza Kiingereza. Angalia na jishughulishe na kila kikundi na usikilize wakati wanafunzi wanafanya mazoezi mmoja na mwingine. Wapongeze kila mara. Fanya mazoezi pamoja nao na wasaidie wao kupata uzoefu wa ufanisi. Taja njia zote wanazojifunza na kuwa bora. Unapowapenda na kuwahimiza wanafunzi, unajenga mazingira ya imani, urafiki na ukuaji.
Kuwa Mwalimu Bora kama Kristo
Kama mwalimu wa EnglishConnect, una fursa ya kipekee ya kuwahudumia wengine. Kanuni za ufundishaji wa kama Kristo zinatumika kwako. Unaweza kujifunza na kutumia kanuni kutoka kwenye nyenzo (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi ( 2022). Chini ya maelekezo ya kiongozi wako wa ukuhani, unaweza kuhudhuria mikutano ya baraza la walimu. Unaweza pia mara kwa mara kutathmini jinsi unavyoendelea na kubainisha maeneo ambayo unaweza kuboresha kwa kutumia “Kuwa Mwalimu Bora kama kama Kristo—Tathmini ya Kibinafsi” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 37). Tambua kile unachofanya vyema. Tambua maeneo unayotaka kuwa bora na kufanya mipango mahususi ya kutumia kile unachojifunza.
Kumbuka, kitu kilicho muhimu sana unachoweza kufanya ni kuwapenda wanafunzi na kutafuta kuongozwa na Roho unapodumisha imani, urafiki na ukuaji.