“Mei 4–10. ‘Msimwasi Bwana, Wala Msiogope,’”Hesabu 11–14;20–24; 27,” Njoo ,Unifuate—Kwa Ajili ya nyumbani na Kanisa: Agano la Kale 2026 (2026)
“Mei 4–10. ‘Msimwasi Bwana, Wala Msiogope’” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026
Jangwa karibu na Rasi ya Sinai
Mei 4-10: “Msimwasi Bwana, Wala Msiwaogope”
Hesabu 11–14; 20–24:27
Hata kwa miguu, isingechukwa miaka 40 kusafiri kutoka nyika za Sinai kwenda nchi ya ahadi Kanaani. Lakini huo ndio muda ambao wana wa Israeli walihitaji—sio kukamilisha umbali wa kijiografia bali kukamilisha umbali wa kiroho: umbali kati ya wao walikuwa kina nani na wangeweza kuwa kina nani kama watu wa agano wa Mungu.
Kitabu cha Hesabu kinaelezea baadhi ya kile kilichotokea wakati wa miaka hiyo 40, ikijumuisha masomo ambayo wana wa Israeli walihitaji kujifunza kabla ya kuingia nchi ya ahadi. Walijifunza kuhusu kuwa waaminifu kwa watumishi wa Bwana (ona Hesabu 12). Walijifunza kuhusu kuamini nguvu za Bwana, hata wakati siku za baadae zilipoonekana hazina tumaini (ona Hesabu 13–14). Na walijifunza kwamba kutokuwa na imani huleta hatari ya kiroho, kama wangeweza kutubu na kumtegemea Mwokozi kwa ajili ya uponyaji (ona Hesabu 21:4–9).
Sote tuko kama Waisraeli katika baadhi ya njia. Sote tunafahamu inavyokuwa kuwa katika nyika ya kiroho, na masomo waliyojifunza yanaweza kutusaidia kujiandaa kuingia katika nchi yetu ya ahadi: uzima wa milele pamoja na Baba yetu wa Mbinguni.
Kwa ajili ya muhtasari wa kitabu cha Hesabu, ona “Hesabu” katika Kamusi ya Biblia.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Hesabu 11:11–17, 24–29; 12
Ufunuo unapatikana kwa kila mtu, lakini Mungu analiongoza Kanisa Lake kupitia nabii Wake.
Katika Hesabu 11:11–17, 24–29, tazama tatizo Musa alilokabiliana nalo na suluhisho alilopendekeza Mungu. Unafikiri Musa alimaanisha nini aliposema alitamani “kwamba watu wote wa Bwana wangekuwa manabii”? (mstari wa 29). Unapotafakari swali hili, tafuta majibu yamkini katika ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Ufunuo kwa ajili ya Kanisa, Ufunuo kwa ajili ya Maisha Yetu” (Liahona, Mei 2018, 93–96).
Kusema sote tunaweza kupokea ufunuo, hata hivyo, haimaanishi kwamba sote tunaweza kuwaongoza watu wa Mungu kama alivyofanya Musa. Tukio katika Hesabu 12 linaweka wazi jambo hili. Je, ni tahadhari zipi unazipata katika mlango huu? Unahisi Bwana anakutaka wewe kufahamu nini kuhusu ufunuo binafisi na kumfuata nabii Wake?
Ona pia 1 Nefi 10:17; Mafundisho na Maagano 28:1–7; Dallin H. Oaks, “Njia Mbili za Mawasiliano,” Liahona, Nov. 2010, 83–86.
Zingatia kile kilicho muhimu zaidi. Baadhi ya watu huzidiwa na mapendekezo ya kusoma kila wiki katika Njoo, Unifuate. Unaporejelea mihutasari, fuata Roho. Fikiria mahitaji yako mwenyewe na mahitaji ya watu unaoweza kuwa unawafundisha. Kuelewa na kutumia kikamilifu kanuni moja katika wiki kunaweza kuwa na msaada zaidi kuliko kusoma sura kadhaa kijuu juu.
Hesabu 12:3.
“Musa alikuwa mpole sana.”
Baadhi ya watu wanashangaa kujifunza kwamba Musa, kiongozi mkuu aliyesimama mbele ya Farao na kufanya miujiza ya kushangaza kwa nguvu za Bwana, pia alikuwa “mpole sana” (Hesabu 12:3). Je, inamaanisha nini kuwa mpole? Fikiria kujifunza ufafanuzi wa Mzee David A. Bednar katika “Mpole na Mnyenyekevu wa Moyo” (Liahona, Mei 2018, 30–33) au “Mpole, Upole” katika Mwongozo wa Maandiko (Gospel Library).
Unajifunza nini kutokana na mifano ya Musa ya upole katika Kutoka 18:13–25; Hesabu 11:26–29; Hesabu 12; Waebrania 11:24–27; na Musa 1:10–11? Unaweza pia kutafakari jinsi Mwokozi alivyoonyesha upole (ona Mathayo 11:29; 27:11–14; Luka 22:41–42; Yohana 13:4–5). Mifano hii inakufundisha nini wewe?
Hesabu 13–14
Kwa imani katika Bwana, naweza kuwa na tumaini la siku za baadaye.
Unaposoma Hesabu 13–14, jaribu kujiweka mwenyewe katika nafasi ya Waisraeli. Kwa nini unafikiri walitaka “kurudi Misri”? (Hesabu 14:3). Je, ni kwa jinsi gani ungelezea “roho” nyingine aliyokuwa nayo Kalebu Hesabu 14:24. Ni nini kinakufurahisha kuhusu imani ya Kalebu na Yoshua, na unawezaje kutumia mifano yao katika hali unazokabiliana nazo?
Kumi kati ya wapelelezi wa Waisraeli waliogopa; Yoshua na Kalebu walikuwa na imani. Yoshua na Kalebu: Wapelelezi Watiifu, na Douglas Klauba. © Lifeway Collection/licensed from goodsalt.com
Hesabu 21:4–9
Ikiwa nitamtegemea Yesu Kristo kwa imani, Yeye anaweza kuniponya kiroho.
Manabii wa Kitabu cha Mormoni walijua hadithi iliyopatikana katika Hesabu 21:4–9 na walielewa umuhimu wake kiroho. Soma mafundisho yao kuhusu hadithi hii katika 1 Nefi 17:40–41; Alma 33:18–22; na Helamani 8:13–15. Hapa kuna baadhi ya maswali ya kutafakari wakati unapofanya hivyo
-
Je, nyoka wa shaba angeweza kuwakilisha nini?
-
Kungatwa na nyoka inaweza kuwakilisha nini?
-
Waisraeli walipaswa “[kumtazama] yule nyoka wa shaba” (Hesabu 21:9) ili kuponywa. Kwa nini unafikiri baadhi ya watu walikataa kutazama? Je, kuna kitu kinachofanana na hicho kilichowahi kutokea kwako?
-
Unahisi msukumo wa kufanya nini ili kwa ukamilifu zaidi “umtazame Mwana wa Mungu kwa imani” na huponywe. (Helamani 8:15).
Kusoma vifungu hivi kunaweza kukukumbusha juu ya nyakati zingine katika maandiko wakati watu walihitaji kuweka fokasi yao kwa Kristo. Kwa mfano, linganisha ujumbe wa Hesabu 21:4–9 na Mathayo 14:25–31 na 1 Nefi 8:24–28 (ona pia picha mwishoni mwa muhtasari wa wiki hii). Ni nini huelekea kutuvuta mbali kutoka kwa Kristo? Ni kwa jinsi gani Yeye anawabariki watu wanaobaki wakifokasi Kwake?
Ona pia “Jesus, the Very Thought of Thee” (Nyimbo za Dini, no. 141).
Hesabu 22–24
Naweza kufuata mapenzi ya Mungu, hata kama wengine wanajaribu kunishawishi mimi nisifanye hivyo.
Wakati Balaki, mfalme wa Moabu, alipojua kuwa Waisraeli walikuwa wanakaribia, alimwita Balaamu, mtu aliyejulikana kwa kutamka baraka na laana. Balaki alimtaka awalaani Waisraeli. Tazama jinsi Balaki alivyojaribu kumshawishi Balaamu (ona Hesabu 22:5–7, 15–17), na fikiria kuhusu majaribu ungeweza kukabiliana nayo kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Nini kinakupa hamasa kuhusu mwitikio wa Balaamu katika Hesabu 22:18, 38; 23:8, 12, 26; 24:13? Cha kisikitisha, Balaamu hatimaye alishindwa kwa shinikizo na kuisaliti Israeli (ona Hesabu 31:16; Yuda 1:11). Tafakari ni kwa namna gani unaweza kuendelea kuwa mwaminifu kwa Bwana bila kujali shinikizo kutoka kwa wengine.
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Hesabu 11:4–10
Ninaweza kuwa na shukrani kwa ajili ya kile Mungu amenipa.
-
Waulize watoto wako kama wanakumbuka baadhi ya miujiza Bwana aliyoifanya kuwasaidia Waisraeli (ona “Mapigo ya Misri” na “Pasaka” katika Hadithi za Agano la Kale, 67–74). Kisha ungeweza kufupisha kwa ajili yao Hesabu 11:4–10, ukisisitiza kwamba Waisraeli walikuwa wamesahau baraka zao na walikuwa wakilalamika. Ni baraka zipi wakati mwingine tunazisahau?
-
Kama unapoimba au kusikiliza wimbo kuhusu shukrani, kama vile “Hesabu Baraka” (Nyimbo za Dini, no. 137), watoto wako wangeweza kuchora picha za baraka Bwana alizowapatia.
Hesabu 12
Bwana ananitaka nimfuate nabii Wake.
-
Ili kutambulisha Hesabu 12, ungeweza kuwaambia watoto wako kwamba Bwana hakuwa na furaha na Haruni na Miriam, kaka na dada wa Musa. Waalike wasome Hesabu 12:1–8 ili kujua kwa nini. Fikiria kutumia Kitabu cha Sanaa ya Injili ili kuwasaidia watoto wako watafute mifano ya watu katika maandiko ambao walimheshimu nabii wa Bwana na walibarikiwa. Ni kwa jinsi gani tunabarikiwa tunapomfuata nabii wa Bwana?
Hesabu 21:6–9
Ninaweza kumtegemea Yesu Kristo.
-
Ungeweza kutumia “Musa na Nyoka wa Shaba” katika Hadithi za Agano la Kale, 83–84, ili kuwasaidia watoto wako wajifunze kile kilichotokea katika Hesabu 21:6–9. Ni kwa jinsi gani nyoka wa shaba ni kama Yesu Kristo? (ona Yohana 3:14–15). Watoto wako wangeweza kufurahia kutengeneza nyoka wa karatasi na kuandika juu yake baadhi ya vitu rahisi wanavyoweza kufanya “kumtegemea Mwana wa Mungu kwa imani” (Helamani 8:15).
1:2Moses and the Brass Serpent
-
Watoto wakubwa wangeweza kuchagua mojawapo ya maandiko yafuatayo na kushiriki kile yanachoongeza katika uelewa wa hadithi hiyo: 1 Nefi 17:41; ; Alma 33:18–20; Helamani 8:13–15; Mafundisho na Maagano 6:36.
Nyoka wa Shaba, na Brent Evans
Hesabu 22–24
Ninaweza kufuata mapenzi ya Mungu, hata kama wengine wanajaribu kunishawishi nisifanye hivyo.
-
Fanyamuhtasari wa Hesabu 22:1–18 kwa ajili ya watoto wako, ukisisitiza jinsi Balaamu alivyokataa kuwalaani watu wa Mungu, hata ingawa Balaki, mfalme wa Moabu, alitaka kumpa hadhi na utajiri. Kisha ungeweza kuwasaidia watoto wako kupekua mistari ifuatayo kwa ajili ya virai ambavyo wanahisi vinaonyesha dhamira ya Balaamu ya kumfuata Mungu: Hesabu 22:18; 23:16; 24:13. Pengine watoto wako wangeweza kuchagua kirai kimoja wanachokipenda na kuandika kwenye kadi ili kuwasaidia wao kukumbuka kumtii Bwana.
Kwa ajili ya zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .