“Aprili 27–Mei 3. ‘Utakatifu kwa Bwana: Kutoka 35–40; Mambo ya Walawi 1; 4; 16; 19,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)
“Aprili 27–Mei 3. ‘Utakatifu kwa Bwana,’” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026
Hekalu la Rio de Janeiro, Brazil
Aprili 27–Mei 3: “Utakatifu kwa Bwana”
Kutoka 35–40; Mambo ya Walawi 1; 4; 16; 19
Kuondoka Misri—muhimu kama ilivyokuwa—haikukamilisha kikamilifu nia ya Mungu kwa wana wa Israeli. Hata maisha ya faraja katika nchi ya ahadi haikuwa kilele cha malengo ya Mungu kwa ajili yao. Hizi zilikuwa ni hatua tu kuelekea kwenye kile Mungu haswa alichotaka kwa ajili ya watu Wake: “Mtakuwa watakatifu: kwani Mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu” (Mambo ya Walawi 19:2). Ni kwa namna gani Mungu alipanga kuwafanya watu Wake kuwa watakatifu baada ya kuwa waliishi utumwani kwa vizazi vingi? Yeye aliwaamuru kutengeneza mahali pa utakatifu nyikani—tabernakulo. Yeye aliwapa maagano na sheria ili kuongoza matendo yao na, kubadili mioyo yao. Na Yeye aliwaamuru kufanya dhabihu za wanyama ili kuwafundisha kuhusu upatanisho kwa ajili ya dhambi zao. Haya yote yalikusudiwa kuelekeza akili zao, mioyo, na maisha kwa Mwokozi. Yeye ni njia ya kweli ya utakatifu, kwa Waisraeli na kwetu sisi. Sisi sote tumetumia muda fulani katika utumwani wa dhambi, na sote tunaalikwa kuacha dhambi nyuma na kumfuata Yesu Kristo, ambaye ameahidi, “ninaweza kuwafanya muwe watakatifu” (Mafundisho na Maagano 60:7).
Kwa ajili ya muhtasari wa kitabu cha Mambo ya Walawi, ona “Mambo ya Walawi” katika Kamusi ya Biblia.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Kutoka 35–40; Mambo ya Walawi 19
Bwana ananitaka niwe mtakatifu.
Kutoka 35-40 inaelezea juhudi za Waisraeli kujenga tabernakulo, mahali ambapo ibada takatifu zingewasaidia kuwa watu watakatifu. Unaposoma sura hizi, tafuta vitu ambavyo Bwana aliwataka watu Wake waweke katika tabernakulo. Je, vitu hivi vinaweza kuwakilisha nini? Vinapendekeza nini kwako kuhusu kuongezeka katika utakatifu? Hususani fikiria ni kwa namna gani vitu hivi hugeuza fikra zako kumwelekea Mwokozi. Jedwali kama hili linaweza kukusaidia:
|
Ni kitu gani ulichopata? |
Hiki kinaweza kuwakilisha nini? |
|---|---|
Ni kitu gani ulichopata? Sanduku la agano (Kutoka 37:1–9; 40:20–21) | Hiki kinaweza kuwakilisha nini? (Ona Kutoka 25:20–22; Mwongozo wa Maandiko, “Sanduku la Agano”) |
Ni kitu gani ulichopata? Madhabahu ya uvumba (Kutoka 40:26–27; ona pia Kutoka 30:1, 6–8) | Hiki kinaweza kuwakilisha nini? (Ona Ufunuo 8:3-4) |
Ni kitu gani ulichopata? Kinara cha mshumaa au kinara cha taa (Kutoka 37:17–24) | Hiki kinaweza kuwakilisha nini? (Ona Mathayo 5:14-16; Yohana 8:12.) |
Ni kitu gani ulichopata? Madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa (Kutoka 38:1–7; ona pia Kutoka 27:1; 29:10–14) | Hiki kinaweza kuwakilisha nini? (Ona Mwongozo kwenye Maandiko, “Dhabihu”) |
Ni kitu gani ulichopata? Birika (beseni) la maji (Kutoka 30:17–21) | Hiki kinaweza kuwakilisha nini? (Ona 2 Mambo ya Nyakati 4:6; Isaya 1:16; Yeremia 33:8) |
Bila shaka, kuwa tu katika sehemu takatifu haitufanyi sisi kuwa watakatifu. Mambo ya Walawi 19 inaelezea sheria na amri Bwana alizowapa Waisraeli ili kuwasaidia kuongeza utakatifu. Unapata nini katika amri hizi ambacho kinaweza kukusaidia kuwa mtakatifu zaidi? Je, unahisi kutiwa msukumo kufanya nini ili kuishi kanuni hizi kwa ukamilifu zaidi?
Ona pia Henry B. Eyring, “Utakatifu na Mpango wa Furaha,” Liahona, Nov. 2019, 100–103; “The Tabernacle” (video), Maktaba ya Injili.
The Tabernacle
Tumia muziki mtakatifu. Muziki una uwezo mkubwa wa kualika ushawishi wa Roho na kujenga imani katika Yesu Kristo. Jumbe zilizopo katika nyimbo zinaweza kuimarisha mafundisho katika maandiko. Kwa mfano, kuimba wimbo kama “Nipe Uongofu” (Nyimbo za Dini, na. 64) kunaweza kuimarisha baadhi ya jumbe zinazofundishwa katika Mambo ya Walawi 19. Inaweza pia kukusaidia kufikiria kuhusu kile inachomaanisha kuwa mtakatifu zaidi kama Mwokozi na kutafakari jinsi Yeye anavyokusaidia kuongezeka katika utakatifu.
Kutoka 35:4–35; 36:1–7
Bwana ananitaka mimi kutoa matoleo yangu kwa moyo wa kupennda.
Katika mwaka baada ya kutoka Misri, uhusiano wa wana wa Israeli na Yehova ungeweza kuelezewa kama usio na thabiti. Na bado, unaposoma Kutoka 35:4– 35 na 36:1–7, tazama jinsi gani Waisraeli walivyoitikia amri ya kujenga tabernakulo. Unajifunza nini kutoka kwa Waisraeli ambacho kingeweza kukusaidia kumtumikia Bwana vizuri zaidi?
Huenda asikuombe vyuma vya thamani, nguo za kitani, au mbao kwa ajili ya tabernakulo. Je, Bwana amekupa nini, na ni nini Yeye anakuomba utoe? Ni lini “moyo wako umekuchochea [wewe] kuja kwenye kazi”?
Ona pia Mada na Maswali, “Dhabihu,” Maktaba ya Injili.
Wana wa Israeli walitoa matoleo kwa ajili ya tabernakulo wakiwa na “moyo wa kupenda” (Kutoka 35:5). Kielelezo na Corbert Gauthier, © Lifeway Collection/licensed from goodsalt.com
Kutoka 40:12–14
Ibada za hekaluni zilitolewa hapo kale.
Kutoka 40:12–14 inahusu ibada za kale ambazo pia hutolewa katika siku yetu katika nyumba ya Bwana. Hapa kuna baadhi ya mistari ya ziada ambayo inaweza kukusaidia kujifunza kuhusu jinsi ibada hizi zinavyoshuhudia juu ya Yesu Kristo:
-
Kuosha: Zaburi 51:2; Ezekieli 36:25–27
-
Mavazi katika mavazi matakatifu: Isaya 61:10; Mathayo 22:11–14; Ufunuo 19:7–8
-
Kupaka mafuta: Luka 4:18–19; Matendo ya Mitume 10:38
Walawi 1:1–9; 4; 16
Kwa sababu ya dhabihu ya Yesu Kristo, ninaweza kusamehewa.
Mengi katika kitabu cha Mambo ya Walawi yanaweza kuonekana mageni kwetu—dhabihu za wanyama, matambiko yaliyohusisha damu na maji, na sheria zinazotawala mambo madogo madogo ya maisha. Ila mila hizi za matambiko na sheria vilinuiwa kufundisha kanuni zinazofahamika—toba, utakatifu, na Upatanisho wa Mwokozi. Ili kupata kanuni hizi unaposoma Mambo ya Walawi 1:1–9; 4; 16, fikiria maswali kama haya:
-
Ni maneno au virai gani ninavyopata ambavyo vinanikumbusha juu ya Yesu Kristo na dhabihu Yake ya kulipia dhambi?
-
Ninajifunza nini kutokana na dhabihu hizi kuhusu dhabihu ya Mwokozi?
-
Ni kwa jinsi gani niko kama watu hawa walifanya dhabihu hizi?
Bwana hahitaji dhabihu za wanyama tena. Lakini dhabihu bado ni kanuni muhimu ya injili. Ili kujifunza kuhusu aina ya dhabihu ambayo Bwana anahitaji, jifunze 3 Nefi 9:19–20; Mafundisho na Maagano 64:34. Ni kwa jinsi gani wewe unatoa aina hii ya dhabihu? Ni nini Musa 5:7 inakufundisha kuhusu jinsi unapaswa kutazama dhabihu zako?
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Kutoka 3:20–29; 36:1
Mungu amenipa vipaji vya kunisaidia kufanya kazi Yake.
-
Mwishoni mwa muhtasari huu kuna picha ya tabernakulo la Waisraeli nyikani. Ungeweza kutaka kuiangalia pamoja na watoto wako na uwaulize ni vifaa gani vingehitajika ili kujenga tabernakulo. Kisha mngeweza kusoma pamoja Kutoka 35:20–29 ili kujua ni kwa jinsi gani nyenzo hizi zilitolewa. Ni kwa jinsi gani Bwana ametualika kuchangia kujenga ufalme Wake?
-
Fikiria kusoma pamoja nao Kutoka 36:1 ili kujua kile Bwana alichompa Bezaleli na Aholiabu ili kusaidia kujenga tabernakulo. Kisha ungeweza kuzungumza na watoto wako kuhusu kile unachohisi Bwana amewapa ili kusaidia kujenga ufalme Wake. Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia vitu hivi kuwabariki wengine?
Hekalu la Rome Italy
Kutoka 40:17–34
Ninaweza kuhisi uwepo wa Bwana katika sehemu takatifu.
-
Kutoka 40:17–34 orodhesha vitu ambavyo vilikuwa sehemu ya hema ya Waisraeli. Pengine wewe na watoto wako mngeweza kuvipata katika mistari hii na katika picha ya tabernakulo mwishoni mwa muhtasari huu. Zungumza kuhusu jinsi kila sehemu ya tabernakulo ingeweza kufunza kuhusu Mwokozi au Baba wa Mbinguni. Kwa mfano, sanduku la ushuhuda lingeweza kutukumbusha juu ya amri za Mungu, madhabahu yanaweza kutukumbusha juu ya dhabihu ya Yesu Kristo, na kadhalika.
-
Ni sehemu gani takatifu tulizonazo leo ambazo zinatusaidia kuhisi karibu zaidi Yesu Kristo? Kama sehemu ya mazungumzo haya, mngeweza kutazama pamoja video “Temples” (Maktaba ya Injili). Mngeweza pia kuimba wimbo kama “Holy Places” (Maktaba ya Injili). Shirikini jinsi mnavyohisi kuhusu maeneo matakatifu kama hekalu.
What Is a Temple?
Mambo ya Walawi 1:1–4
Kwa sababu ya dhabihu ya Yesu Kristo, ninaweza kusamehewa.
-
Dhabihu za wanyama zilizoelezewa katika Agano la Kale zilikusudiwa kuwafundisha wana wa Israeli kuhusu msamaha kupitia Yesu Kristo. Fikiria jinsi kusoma kuhusu dhabihu hizi kunaweza kufanya vivyo hivyo kwa watoto wako. Ungeweza kuonesha picha za Yesu Kristo akiwa Gethsemane na juu ya msalaba (ona Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 56, 57) unaposoma pamoja na watoto hao Walawi 1:1–4. Wasaidie watafute maneno au virai ambavyo vinawakumbusha dhabihu ya Yesu Kristo.
-
Mngeweza pia kusoma pamoja 3 Nefi 9:19–20 ili kujua kile ambacho tumeamriwa kutoa dhabihu badala ya wanyama. Inamaanisha nini kutoa moyo uliovunjika na roho iliyopondeka kwa Bwana? Ona Mwongozo wa Maandiko, “Moyo Uliovunjika” (Maktaba ya Injili) kwa ajili ya msaada wa kujibu swali hili.
Kwa ajili ya zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .