Njoo, Unifuate
Mei 11–17. “Jihadhari Usije Ukamsahau Bwana”: Kumbukumbu la Torati 6–8; 15; 18; 29–30; 34


“Mei 11–17. ‘Jihadhari Usije Ukamsahau Bwana’: Kumbukumbu la Torati 6–8; 15; 18; 29–30; 34,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)

“Mei 11–17. ‘Jihadhari Usije Ukamsahau Bwana,’” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026

Musa juu ya Mlima Nebo

Musa juu ya Mlima Nebo, na John Steel, © Providence Collection/licensed from goodsalt.com

Mei 11–17: “Jihadhari Usije Ukamsahau Bwana”

Kumbukumbu la Torati 6–8; 15; 18; 29–30;34

Huduma ya Musa ya duniani ilianzia mlimani, wakati Mungu alipozungumza naye kutoka kwenye kichaka kinachoteketea (ona Kutoka 3:1–10). Pia iliishia mlimani, zaidi ya miaka 40 baadae, wakati Mungu alipompa yeye mtazamo kidogo tu wa nchi ya ahadi kutoka juu ya Mlima Nebo (ona Kumbukumbu la Torati 34:1–4). Musa alikuwa ametumia maisha yake akiwaandaa wana wa Israeli kuingia ile nchi ya ahadi, na kitabu cha Kumbukumbu la Torati husema maelekezo yake ya mwisho, ukumbusho, ushauri, na kusihi kwa Waisraeli. Kusoma maneno yake huweka wazi kwamba malengo halisi ya huduma ya Musa—maandalizi ambayo watu waliyahitaji—hayakuwa tu kuhusu kunusurika nyikani, kuwashinda maadui, au kujenga taifa. Ilikuwa ni kuhusu kujifunza kumpenda Mungu, kumtii Yeye, na kubaki waaminifu Kwake. Hayo ndiyo maandalizi sisi wote tunayahitaji ili tuweze kuingia kwenye nchi ya ahadi ya uzima wa milele. Kwa hiyo ingawa Musa hakuwahi kukanyaga kwa miguu katika “nchi itiririkayo maziwa na asali” (Kutoka 3:8), kwa sababu ya imani yake na uaminifu, yeye aliingia kwenye nchi ya ahadi ambayo Mungu ameiandaa kwa ajili ya wote wanaomfuata Yeye.

Kwa ajili ya muhtasari wa Kumbukumbu la Torati, ona “Kumbukumbu la Torati” katika Kamusi ya Biblia.

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Kumbukumbu la Torati 6:4–7; 8:2–5, 11–17; 29:18–20; 30:6–10, 14–20

ikoni ya seminari
“Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote.”

Sheria ya Musa ilijumuisha sherehe nyingi za nje na matambiko. Utakapoona katika ushauri wa Musa katika Kumbukumbu la Torati, Bwana pia alikuwa na wasiwasi kuhusu hali ya ndani ya watu Wake—hali ya kiroho ya mioyo yao.

Katika vifungu hapa chini, tafuta neno moyo, na utafakari kile linachoweza kuashiria. Unaweza kufikiria juu ya vifungu hivi kama aina ya ukanguzi wa kiroho kwenye moyo wako. Ni utambuzi gani ungeweza kujipatia wewe mwenyewe? Ni matibabu gani ungeweza kujiaandikia ili kuboresha afya ya kiroho ya moyo wako? Andika misukumo yako.

  • Kumbukumbu la Torati 6:4–7:

  • Kumbukumbu la Torati 8:2–5:

  • Kumbukumbu la Torati 8:11–17:

  • Kumbukumbu la Torati 29:18–20:

  • Kumbukumbu la Torati 30:6–10:

  • Kumbukumbu la Torati 30:14–20:

Njia moja ya kupanga mawazo yako ingeweza kuwa kuchora moyo na kuandika ndani yake mambo ambayo Bwana anasema unapaswa kuwa nayo moyoni mwako. Kisha ungeweza kuandika nje yake mambo ambayo unapaswa kuyaweka nje ya moyo wako.

Ni kwa jinsi gani unaonyesha kwamba unampenda Mungu kwa moyo wako wote? Kwa ajili ya mawazo, ona “Mpende Mungu, mpende jirani yako,” katika Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi, 10-12.

Ona pia M. Russell Ballard, “Je, Wanipenda Mimi Zaidi ya Hawa?,” Liahona, Nov. 2021, 51–53.

Tafuta umaizi wako mwenyewe wa kiroho. Njoo,Unifuate inapendekeza vifungu na kanuni unazoweza kuzifokasi juu yake, katika maandiko, lakini usiruhusu hilo likuwekee mipaka kwenye kujifunza kwako. Unaposoma Kumbukumbu la Torati, unaweza kugundua kanuni ambayo haijaangaziwa hapa. Acha Roho Mtakatifu akuongoze kwenye kile unachohitaji kujifunza.

Kumbukumbu la Torati 6:4–13, 20–25

“Ujihadhari, Usije Ukamsahau Bwana.”

Wengi wa Waisraeli ambao wangeingia katika nchi ya ahadi hawakuwahi kushuhudia yale mapigo ya Misri au kuvuka Bahari ya Shamu. Musa alijua kwamba wao—na vizazi vya baadae—wangehitaji kukumbuka miujiza ya Mungu na sheria za Mungu ili wabaki kuwa watu wa Mungu.

Ni ushauri gani Musa anautoa katika Kumbukumbu la Torati 6:4–12, 20–25 ambao ungeweza kukusaidia kukumbuka mambo makubwa ambayo Mungu amekufanyia? Unapata ushawishi wa kufanya nini ili kwamba neno la Bwana daima litakuwa “ndani ya moyo wako”? (mstari wa 6).

Unaweza pia kujifunza ujumbe wa Kaka Jan E. Newman “Kuhifadhi Sauti ya Watu wa Agano katika Kizazi Kinachoinukia” (Liahona, Nov. 2023, 36–38) na fikiria jinsi utakavyopitisha imani yako katika Kristo kwa vizazi vijavyo.

Ona pia Kumbukumbu la Torati 11:18–21; Dale G. Renlund, “Fikiria Wema na Ukuu wa Mungu,” Liahona, Mei 2020, 41–44; Kamusi ya Biblia, “Frontlets au phylacteries.”

Kumbukumbu la Torati 15:1–15

Kuwasaidia wenye uhitaji kunahusisha mikono ya ukarimu na moyo wa utayari.

Bado hatujafika katika siku “ambayo hakutakuwa na maskini kati yenu” (Kumbukumbu la Torati 15:4), kwa hivyo kanuni kuhusu kuwasaidia maskini katika Kumbukumbu la Torati 15 bado ni muhimu, hata kama mazoea fulani yamebadilika. Tambua nini mstari 1–15 inafundisha kuhusu kwa nini tunawasaidia watu wenye uhitaji na mtazamo wetu unapaswa kuwa nini juu ya hili.

Inamaanisha nini “kufungua mkono wako kwa upana” kwa watu wenye shida? (mstari wa 8, 11). Unajifunza nini kutokana na mfano wa Bwana kuhusu kuwasaidia watu wenye uhitaji? (ona mstari wa 15).

Ona pia “Kuna Lo lote Jema Nimefanya?,” Nyimbo za Dini, no. 128.

Kumbukumbu la Torati 18:15–19

Musa alikuwa “kama” Yesu Kristo.

Petro, Nefi, Moroni, na Mwokozi mwenyewe wote walisifu juu ya unabii katika Kumbukumbu la Torati 18:15–19 (ona Matendo ya Mitume 3:20–23; 1 Nefi 22:20–21; Joseph Smith—Historia ya 1:40; 3 Nefi 20:23). Unajifunza nini kuhusu Mwokozi kutoka kwenye mistari hii? Fikiria kuhusu kile ulichosoma kuhusu Musa katika wiki chache zilizopita. Ni kwa jinsi gani Musa “ni kama” Yesu Kristo?

Yesu akiwafundisha Wanefi

Yesu Kristo aliwaambia watu Wake katika Amerika ya kale, “Mimi ni yule ambaye nabii Musa alimzungumzia” (3 Nefi 20:23).

Kumbukumbu la Torati 29:9; 30:15–20

Bwana ananialika nichague kati ya mema na maovu.

Iinaweza kuwa ya kuvutia kufananisha maneno ya Musa katika Kumbukumb ya Torati 29:9; 30:15–20 na baadhi ya mafundisho ya mwisho ya Lehi kwa familia yake katika 2Nefi 2:26–29; 4:4. Je, Lehi alipanua vipi yale yaliyofundishwa na Musa? Unapata nini katika mistari hii ambacho kinakushawishi kuchagua uzima? (Kumbukumbu la Torati 30:19).

ikoni ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Kumbukumbu ya Torati 6:5

Ninaweza kumpenda Mungu kwa moyo wangu wote.

  • Ili kuwasaidia watoto wako waelewe Kumbukumbu la Torati 6:5, ungeweza kuchora moyo, mstari wa umbo la mwili, na mkono wenye nguvu. Watoto wako wangeweza kuonesha picha wakati unaposoma maneno “moyo,” “nafsi,” na “nguvu” katika mstari huu. Ni kwa jinsi gani tunamwonyesha Bwana kwamba tunampenda kwa moyo, roho, na nguvu zetu zote?

Kumbukumbu la Torati 6:6–15

Ninaweza kuliweka neno la Mungu katika moyo wangu.

  • Soma pamoja na watoto wako ushauri wa Bwana kwa Waisraeli ili waweke vifungu vya maandiko mahali ambapo wangeviona kila siku (ona Kumbukumbu la Torati 6:6–9). Hii inaweza kukupa msukumo wewe na watoto wako kufikiria njia za kuhakikisha kuwa “haumsahau Bwana” (mstari wa 12) na kukumbuka kile ambacho Yeye amekufanyia.

  • Ungeweza kuonyesha kwamba Kumbukumbu la Torati 6:13, 16 na 8:3 ilimsaidia Mwokozi katika wakati muhimu katika maisha Yake. Ili kuona jinsi gani, someni pamoja Mathayo 4:1–10. Kisha mngeweza kushiriki na kila mmoja baadhi ya vifungu vya maandiko ambavyo vimekusaidia katika nyakati za uhitaji.

Kijana akisoma maandiko

Kumbukumbu la Torati 18:15–18

Manabii hutufundisha kuhusu Yesu Kristo.

  • Mnaposoma Kumbukumbu la Torati 18:18 pamoja, wasaidie watoto wako waelewe kwamba Nabii kama Musa katika mstari huu ni Yesu Kristo. Pengine ungeweza kuangalia picha za vitu ambavyo Musa alivifanya na vitu ambavyo Yesu Kristo alivifanya, na waache watoto wako wavilinganishe (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 15, 16, 38,39). Je, nabii wetu aliye hai amefundisha nini leo kuhusu Mwokozi?

Kumbukumbu la Torati 29: 12–13; 30:8–10

Kwa sababu ya maagano yangu, mimi ni sehemu ya watu wa Mungu.

  • Kuzungumzia kuhusu Kumbukumbu la Torati 29:12–13 kunatoa nafasi kwako na wanafamilia wako kujadiliana maagano watakayofanya au ambayo wamefanya na Baba wa Mbinguni. Inamaanisha nini kuwa watu wa Mungu? Je, ni kwa jinsi gani ahadi zetu zinatufanya sisi kuwa watu wa Mungu? (ona mstari wa 13;ona pia Mosia 18:8–10).

  • Kama watoto wako wanahitaji msaada kuelewa agano ni nini, pendekeza kwamba wapate maana katika “Agano” katika Mwongozo wa Maandiko (Maktaba ya Injili). Ni ahadi gani Mungu na Waisraeli walifanya kwa kila mmoja katika Kumbukumbu la Torati 30:8–10? Je, ni ahadi gani sisi tumefanya na Mungu? (ona Mafundisho na Maagano 20:37, 77). Je, ni kwa jinsi gani ahadi hizi zinatuunganisha Naye? Fikiria kuimba pamoja wimbo kuhusu maagano, kama vile “Standing on the Promises” (Maktaba ya Injili).

Kwa ajili ya zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .

Musa akitazama kuelekea nchi ya ahadi

Bwana Alimwonyesha Yeye Nchi Yote, na Walter Rane

Ukurasa wa shughuli za Msingi: Ninaweza kuliweka neno la Mungu katika moyo wangu.