Njoo, Unifuate
Mawazo ya Kuweka Akilini: Tabenakulo na Dhabihu


“Mawazo ya Kuweka Akilini: Tabenakulo na Dhabihu,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani; Agano la Kale 2026 (2026)

“Tabenakulo na Dhabihu,” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026

ikoni ya mawazo

Mawazo ya Kuweka Akilini

Tabenakulo na Dhabihu

Tunaposoma Agano la Kale, wakati mwingine tunakuta vifungu virefu kuhusu mambo ambayo yalikuwa muhimu hasa kwa Bwana lakini yaweza kuwa hayana umuhimu wa moja kwa moja kwetu leo. Kutoka 25–30; 35–40 na Mambo ya Walawi 1–9; 16–17 ni mifano. Sura hizi zinaelezea kwa undani tabenakulo la Israeli katika nyika na dhabihu za wanyama iliyopaswa kufanyika humo. Tabenakulo lilikuwa hekalu dogo lililoweza kubebeka, mahali pa makazi ya Bwana kukaa kati ya watu Wake.

Mahekalu yetu ya kisasa yana mifanano na tabenakulo la Waisraeli, ila kiuhalisia hayafanani na maelezo katika Kutoka. Na hatuui wanyama katika mahekalu yetu—Upatanisho wa Mwokozi ulimaliza dhabihu za wanyama zaidi ya miaka 2,000 iliyopita. Bado licha ya tofauti hizi, kuna thamani kubwa leo katika kusoma kuhusu aina za kuabudu za Israeli ya kale, hususani kama tunawaona wao ni kama watu wa Mungu katika Kitabu cha Mormoni walivyowaona—kama njia ya “kuimarisha imani yao katika Kristo” (Alma 25:16). Tunapoelewa ishara ya tabenakulo na dhabihu ya wanyama, tunaweza kupata umaizi wa kiroho ambao pia utaimarisha imani yetu katika Kristo.

Waisraeli wakileta mwanakondoo kwenye tabenakulo

Dhabihu ya Mwanakondoo, na Robert T. Barrett

Tabenakulo Huimarisha Imani katika Yesu Kristo.

Wakati Mungu alipomwamuru Musa kujenga tabenakulo katika kambi ya Waisraeli, Yeye alieleza kusudi lake: “ili nipate kukaa kati yao” (Kutoka 25:8). Ndani ya tabenakulo, uwepo wa Mungu uliwakilishwa na sanduku la agano—sanduku la mbao, lililofunikwa kwa dhahabu, likiwa na kumbukumbu ya maandishi yaliyoandikwa ya agano la Mungu na watu Wake, Sanduku lilikuwa linatunzwa katika mahali patakatifu sana, chumba cha ndani kabisa, kilichotengwa na vingine vya tabenakulo kwa pazia. Pazia hili linaweza kuashiria kutengwa kwetu kutoka kwenye uwepo wa Mungu kwa sababu ya Anguko, vile vile njia yetu ya kurudi Kwake—kupitia Kwa Mwokozi.

Isipokuwa Musa, tunamjua mtu mwingine mmoja tu ambaye angeweza kuingia “mahali patakatifu sana” (Kutoka 26:34)—kuhani mkuu. Kama makuhani wengine, kwanza alipaswa kuoshwa na kupakwa mafuta na kuvikwa mavazi matakatifu kama ishara ya ofisi yake. Mara moja kwa mwaka, katika siku iliyoitwa Siku ya Upatanisho, kuhani mkuu angetoa dhabihu kwa niaba ya watu kabla ya kuingia peke yake kwenye tabenakulo Kwenye pazia, angechoma uvumba. Harufu ya moshi inayopaa mbinguni iliwakilisha sala za watu zikipaa kwa Mungu. Kisha kuhani mkuu, akibeba damu kutoka kwenye dhabihu ya mnyama, angepita kwenye pazia na kukaribia kiti cha enzi cha Mungu, kilichoashiriwa na sanduku la agano.

Ukijua kile unachojua kumhusu Yesu Kristo na wajibu Wake katika mpango wa Baba wa Mbinguni, je, unaweza kuona jinsi tabenakulo inavyotuelekeza sisi kwa Mwokozi? Kama vile tabenakulo, na sanduku la agano ndani yake, ilivyowakilisha uwepo wa Mungu miongoni mwa watu Wake, Yesu Kristo alikuwa uwepo wa Mungu kati ya watu Wake. Kama vile kuhani mkuu, Yesu Kristo ni Mpatanishi kati yetu sisi na Mungu Baba. Alipita kwenye pazia kufanya maombezi kwa ajili yetu kwa fadhili ya dhabihu ya damu Yake mwenyewe.

Baadhi ya vipengele vya tabenakulo la Israeli vinaweza kuwa vya kawaida kwako, hususani kama umewahi kuwa hekaluni kupokea ibada zako mwenyewe. Hekalu ni nyumba ya Bwana—mahali pake pa makao miongoni mwa watu Wake. Kama mahali patakatifu sana pa tabenakulo, chumba cha selestia katika hekalu huwakilisha uwepo wa Mungu. Ili kuingia, lazima kwanza tuoshwe na kupakwa mafuta. Tunavaa mavazi matakatifu. Tunafanya maagano. Tunasali katika madhabahu ambapo kutoka hapo sala hupanda kwa Mungu. Na mwishowe tunapita kwenye pazia na kwenda katika uwepo wa Mungu.

Labda ufanano wa muhimu sana kati ya mahekalu ya kisasa na tabenakulo la kale ni kwamba yote, kama itaeleweka vizuri, huimarisha imani yetu katika Yesu Kristo na kutujaza na shukrani kwa ajili ya dhabihu Yake ya kulipia dhambi. Mungu anataka watoto Wake wote kuingia katika uwepo Wake; Yeye anataka “ufalme wa makuhani” na makasisi wa kike (Kutoka 19:6). Lakini dhambi zetu hutuzuia sisi kupata baraka hiyo, kwani “hakuna kitu kichafu chaweza kuishi na Mungu” (1 Nefi 10:21). Kwa hiyo Mungu Baba alimtuma Yesu Kristo, “kuhani wetu mkuu wa mambo mazuri yajayo” (Waebrania 9:11). Yeye hufunua pazia kwa ajili yetu na kuwapa uwezo watoto wote wa Mungu “kuja kwa ujasiri kwenye kiti cha neema, ili tuweze kupata rehema” (Waebrania 4:16).

Leo, madhumuni ya mahekalu ni zaidi ya kupata kuinuliwa kwetu sisi wenyewe. Baada ya kupokea ibada zetu wenyewe na kufanya maagano na Mungu, tunaweza kusimama katika nafasi ya wahenga wetu na kupokea ibada kwa niaba yao. Katika maana, tunaweza kuwa kitu kama kuhani mkuu wa kale—na Kuhani Mkuu—tukifungua njia ya uwepo wa Mungu kwa ajili ya wengine.

Dhabihu Huimarisha Imani katika Yesu Kristo.

Kanuni za upatanisho na kupatanishwa zinafundishwa kwa nguvu katika matendo ya kale ya dhabihu za wanyama, ambazo zilikuwapo mapema sana kabla ya sheria ya Musa. Adamu na Hawa walitoa dhabihu. Walielewa marejeleo yake ya kiishara ya dhabihu ya Mwokozi. Na walifundisha hili kwa watoto wao.

Ishara ya dhabihu ya wanyama yawezekana ilionekana hususani yenye ukali katika Siku za Upatanisho wa Waisraeli wa kale (“Yom Kippur” kwa Kiebrania). Uhitaji wa sherehe hii ya mwaka ulielezewa katika Mambo ya Walawi 16:30: “Katika siku hiyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yenu, kuwatakasa, ili muweze kusafishwa kutokana na dhambi zenu zote mbele ya Bwana.” Hii iliruhusu uwepo wa Mungu kubaki miongoni mwa watu. Upatanisho huu ulikamilishwa kupita sherehe za aina mbalimbali. Katika mojawapo ya hizi, mbuzi aliuawa kama matoleo kwa ajili ya dhambi za watu, na kuhani mkuu alichukua damu hiyo ya mbuzi ndani ya mahali patakatifu sana. Baadae, kuhani mkuu aliweka mikono yake juu ya mbuzi aliye hai na kuungama dhambi za wana wa Israeli—kuashiria kuhamisha dhambi hizo kwa yule mbuzi. Baadae mbuzi alifukuzwa nje ya kambi ya Israeli.

Katika ibada hizi, mbuzi waliashiria Yesu Kristo, akichukua nafasi ya watu wenye dhambi. Dhambi haipaswi kuruhusiwa katika uwepo wa Mungu. Lakini badala ya kuwateketeza au kuwafukuza nje wenye dhambi, Mungu alitoa njia mbadala—badala yake mbuzi angeuawa au kufukuzwa nje. “Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote,” (Mambo ya Walawi 16:22).

Ishara hizi za ibada ilionyesha njia ambayo Mungu ametoa ili kutuleta sisi tena kwenye uwepo Wake—Yesu Kristo na Upatanisho Wake. Mwokozi “ameyachukua masikitiko yetu, na amejitwika huzuni zetu,” hata “maovu yetu sisi sote”(Isaya 53:4, 6). Alisimama katika nafasi yetu, alitoa maisha Yake kulipia adhabu ya dhambi, na kisha kukishinda kifo kupitia Ufufuko Wake. Dhabihu ya Yesu Kristo ilikuwa “dhabihu kuu na ya mwisho; ndio, sio dhabihu ya mtu, wala ya mnyama” badala yake “dhabihu isiyo ya mwisho na ya milele” (Alma 34:10). Yeye alikuwa ni ukamilisho wa kila kitu dhabihu ya kale ilichoelekeza.

Yesu akibeba msalaba.

Kwa sababu hii, baada ya dhabihu Yake kukamilika, Alisema, “Na hamtatoa kwangu tena kumwagwa kwa damu; ndio, dhabihu zenu … zitakomeshwa. … Na mtatoa kwangu dhabihu ya moyo uliopondeka na roho iliyovunjika” (3 Nefi 9:19–20).

Kwa hiyo unapopata vifungu katika Agano la Kale kuhusu dhabibu na tabenakulo (au baadae, hekalu)—na utayaona mengi—kumbuka kwamba sababu ya msingi ya yote haya ni kuimarisha imani yako katika Masiya, Yesu Kristo. Unganisha kile ulichosoma na kujifunza pamoja na kuabudu kwako katika nyumba Yake. Acha moyo wako na akili zako zimgeukie Yeye. Tafakari aliyoyafanya ili kukurudisha katika uwepo wa Mungu—na wewei utafanya nini kumfuata Yeye.

Mihutasari

  1. Kutoka 33:7–11 inataja “tabenakulo la kusanyiko,” ambapo Musa aliwasiliana na Bwana, ila huu haukuwa mpangilio wa dhabihu ulioelezwa katika Kutoka na Mambo ya Walawi. Dhabihu hizo zilifanywa katika tabenakulo lililoelezwa katika Kutoka 25–30, ambalo Mungu alimuamuru Musa na wana wa Israeli kujenga (ona Kutoka 35–40). Tabenakulo hili, ambamo Haruni na wanawe walitoa dhabibu za wanyama, mara nyingi lilirejelewa kama “tabenakulo la kusanyiko”(ona, kwa mfano, Kutoka 28:43; 38:30; Mambo ya Walawi 1:3).

  2. Ona pia Yakobo 4:5; Yaromu 1:11.

  3. Ona Kutoka 25:10–22.

  4. (ona Waebrania 10:19–20).

  5. Ona Kutoka 40:12–13.

  6. Ona Kutoka 28.

  7. Ona Mambo ya Walawi 16:12.

  8. Ona Zaburi 141:2.

  9. Ona Mathayo 16:14-15.

  10. Ona Yohana 1:14.

  11. Ona Waebrania 8–10.

  12. Ona Musa 5:4–12; ona pia Mwanzo 4:4.

  13. Ona Mosia 15:8–9.