April 20–26. ‘Hayo Yote Aliyoyanena Bwana Tutayatenda’: Kutoka 19–20; 24; 31–34,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)
April 20–26. ‘Hayo Yote Aliyoyanena Bwana Tutayatenda,’” Njoo, Unifuate Agano la Kale 2026
Musa na Vibao, na Jerry Harston (maelazo ya kina)
Kutoka 20–26: “Hayo Yote Aliyoyanena Bwana Tutayatenda”
Kutoka 19–20; 24; 31–34
Hata kama watoto wa Israeli walinung’unika na kuyumba hapo nyuma, wakatiMusa aliposoma sheria chini ya Mlima Sinai, walifanya agano hili: “Hayo yote aliyoyanena Bwana tutayatenda, nasi tutatii.” (Kutoka 24:7). Mungu kisha alimwita Musa mlimani, akimwambia kujenga hema ili “nipate kukaa miongoni mwao”(Kutoka 25:8).
Lakini wakati Musa akiwa juu ya mlima akijifunza ni kwa namna gani Waisraeli wangeweza kuwa na uwepo wa Mungu miongoni mwao, Waisraeli walikuwa chini ya mlima wakitengeneza sanamu ya dhahabu ili kuiabudu badala Yake. Mara baada ya kuahidi “kutokuwa na miungu wengine,” “waligeuka pembeni haraka,” kutoka kwenye ahadi yao (Kutoka 20:3; 32:8; ona pia Kutoka 24:3). Ilikuwa ni geuko la kushangaza, lakini tunajua kutokana na uzoefu kwamba imani na ahadi vinaweza wakati mwingine kuzidiwa na kutokuwa na uvumilivu, woga, au mashaka. Tunapoutafuta uwepo wa Bwana katika maisha yetu, inatia moyo kujua kwamba Bwana hajawahi kukata tamaa kwa Israeli ya kale na hatakata tamaa kwetu sisi na watu tunaowapenda— kwani Yeye ni “mwingi wa huruma, na mwenye fadhila , si mwepesi wa hasira, mvumilivu mwingi wa rehema na kweli” (Kutoka 34:6).
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Kutoka 19:3–6
Watu wa agano wa Mungu ni hazina Kwake.
Rais Russell M. Nelson alifundisha “Katika Agano la Kale, neno la Kiebrania ambako neno kipekee lilitafsiriwa ni segullah,, ambalo linamaanisha ‘mali iliyothaminiwa,’ au ‘hazina.’ … Kwa sisi kutambuliwa na watumishi wa Bwana kama watu Wake wa kipekee ni sifa ya kiwango cha juu sana” (“Children of Covenant,” Ensign, Mei 1995, 34). Ni kwa jinsi gani maneno ya Rais Nelson yanaathiri jinsi unavyoelewa Kutoka 19:3–6? Ni kwa jinsi gani Bwana ameonesha kwamba Yeye anakuthamini wewe?
Kutoka 19:10–11, 17
Uzoefu mtakatifu unahitaji maandalizi.
Bwana alimwambia Musa kwamba wana wa Israeli walihitaji kuandaliwa kabla ya kuweza “kukutana na Mungu” (Kutoka 19:10–11, 17) na kushika agano na Yeye (ona Kutoka 19:5). Ni kwa jinsi gani unajiandaa kwa ajili ya uzoefu wa kiroho, ikijumuisha sakramenti na ibada za hekaluni? Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia wengine kujiandaa? Unajifunza nini kuhusu maandalizi kutoka Luka 6:12–13; Enoshi 1:2–6; Alma 17:2–3?
Mlima huu huko Misri kwa asili unaaminika kuwa Mlima Sinai.
Kutoka 20:1–17
Utiifu kwa amri za Mungu huleta baraka.
Wakati Waisraeli walipokuwa wamekusanyika chini ya Mlima Sinai, walisikia sauti ya Mungu ikitoa hizo Amri Kumi (ona Kumbukumbu ya Torati 4:12–13). Hizi, bila shaka, siyo amri pekee za Mungu—zipo zingine nyingi katika maandiko. Kwa hiyo unaposoma Kutoka 20:1–17, jiulize mwenyewe kwa nini Mungu alisisitiza hizi kumi hasa. Hapa kuna sampuli ya jedwali unaloweza kutumia unapotafakari umuhimu wa Amri Kumi katika maisha yako:
|
Amri |
Kwa maneno mengine, Bwana ananiomba mimi … |
Baraka ambazo huja kutokana na kuishi amri hii |
|---|---|---|
-
Ni kwa jinsi gani kutii amri hizi kumi kunakusaidia kutii amri kuu mbili ambazo Yesu alitoa kat\ika Mathayo 22:34–40?
-
Ni vitu gani ambavyo unaweza kujaribiwa kuviweka mbele ya Mungu? Ni baraka zipi umeziona kwa kumweka Mungu kwanza?
-
Ni kwa jinsi gani ungemjibu mtu ambaye anasema Amri Kumi zilitolewa muda mrefu uliopita na hazitumiki leo? Ni mifano gani kutoka katika maisha yako ambayo ungeshiriki kama sehemu ya majibu yako? Ni kwa jinsi gani wimbo “Amri Zake Mungu” (Nyimbo za Dini, na. 71) unaweza kuathiri jinsi unavyoelezea amri za Mungu kwa wengine?
-
Ni kwa jinsi gani Bwana ametimiza ahadi katika Kutoka 20:6 kwenye maisha yako?
Ona pia “The Great Commandment—Love the Lord,” katika Teachings of Presidents of the Church: Ezra Taft Benson (2014), 37–45; Dallin H. Oaks, “Hakuna Miungu Mingine,” Liahona, Nov. 2013, 72–75; Mada na Maswali, “Amri,” Maktaba ya Injili.
Kutoka 24:1–11
Maagano yangu yanaonyesha utayari wangu wa kutii amri za Mungu.
Unaposoma Kutoka 24:3–8, fikiria maagano uliyofanya na Mungu. Wakati agano la Israeli lilijumuisha mila za matambiko ambazo ni tofauti na zile Mungu anazohitaji leo, unaweza kuona baadhi ya mifanano. Kwa mfano, mstari wa 4, 5, na 8 inataja madhabahu, sadaka ya wanyama, na damu. Mambo haya yanaweza kuwakilisha nini, na yanahusiana vipi na maagano yako?
Kutoka 32–34
Dhambi ni kugeuka mbali na Mungu; toba ni kumgeukia Yeye na kugeuka mbali na uovu.
Jaribu kujiweka katika mahali pa Waisraeli—uko nyikani, Musa ameondoka kwa siku 40, na makabiliano na Wakanaani juu ya nchi ya ahadi yapo katika siku zako zijazo (ona Kutoka 32:1–8). Unafikiri ni kwa nini Waisraeli walitaka sanamu ya dhahabu? Ni nini kinakutia msukumo kuhusu ombi la Musa kwa Bwana katika Kutoka 33:11–17?
Ingawa dhambi ya Waisraeli ilikuwa kubwa mno, hadithi hii inajumuisha pia ujumbe wa huruma ya Mungu na msamaha. Ni nini Kutoka 34:1–10 inakufundishakuhusu Mwokozi? (ona Kutoka 32:30–32; Mosia 14:4–8; 15:9; Mafundisho na Maagano 45:3–5).
Kutoka 31:13–16
Sabato ni ishara.
Rais Russell M. Nelson alielezea: “Katika miaka ya ujana wangu, nilijifunza kazi za wengine ambazo ziliorodhesha vitu vya kufanya na vya kutofanya katika Sabato. Haikuwa hadi baadaye ndipo nikajifunza kutoka katika maandiko kwamba mwenendo wangu na mtazamo wangu juu ya Sabato ilikuwa ishara kati yangu mimi na Baba yangu wa Mbinguni [ona Kutoka 31:13; Ezekieli 20:12, 20]. Kwa uelewa huo, sikuhitaji tena orodha ya vya kufanya na kutofanya. Nilipohitaji kufanya maamuzi ya kujua kama shughuli ilikuwa au haikuwa sahihi kwa ajili ya Sabato, nilijiuliza mwenyewe tu, ‘Ni ishara gani ninataka kumwonyesha Mungu?’ Swali hilo lilifanya uchaguzi wangu kuhusu siku ya Sabato kuwa dhahiri zaidi” (“Sabato ni Siku ya Furaha,” Liahona, Mei 2015, 130). Tafakari ishara gani unataka kumpa Mungu na kuitii Sabato.
Kutoka 34:1– 4
Ni nini ilikuwa tofauti kati ya seti mbili za vibao vya mawe alizotengeneza Musa?
Musa aliposhuka chini kutoka mlimani, alileta sheria iliyoandikwa kwenye vibao vya mawe. Baada ya kugundua kwamba Waisraeli walikuwa wamevunja agano lao, Musa alivunja vile vibao (ona Kutoka 31:18; 32:19). Baadae, Mungu alimwamuru Musa kutengeneza seti nyingine ya vibao vya mawe na kuzipeleka tena mlimani (ona Kutoka 34:1–4). Tafsiri ya Joseph Smith, Kutoka 34:1–2 (katika kiambatisho cha Biblia) inafafanua kwamba seti ya kwanza ya vibao vya mawe ilijumuisha ibada za Mungu za “utaratibu mtakatifu,” au Ukuhani wa Melkizedeki. Seti ya pili ilijumuisha “amri ya sheria ya kimwili.” Hii ilikuwa sheria ndogo iliyosimamiwa na “ukuhani mdogo” (ona Mafundisho na Maagano 84:17–27), iliyokuwa imekusudiwa kuwaandaa Waisraeli kwa ajili ya sheria ya juu na ukuhani mkubwa ili waweze kuingia katika uwepo wa Mungu.
Kwa ajili ya zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Kutoka 20:3–17
Mungu hunipa amri kwa sababu anataka niwe na furaha.
-
Ni kwa jinsi gani unaweza kufanya kujifunza kuhusu Amri Kumi kuwa jambo la kufurahisha kwa ajili ya watoto wako? Mnaposoma Kutoka 20:3–17 pamoja, waache watoto wako wakusaidie kupata au wachore picha yenye kuwakilisha kila moja ya Amri Kumi. Kisha watoto wako wangeweza kufanya zamu kuchagua picha na kuzungumza kuhusu jinsi wanavyoweza kuishi amri hiyo. Shiriki na kila mmoja jinsi kuishi amri hiyo kunavyokuletea wewe furaha.
-
Mngeweza pia kuimba wimbo kama vile “Keep the Commandments” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146–47). Wasaidie watoto wako watafute maneno katika wimbo ambayo yanawafundisha kwa nini Mungu anatutaka tutii amri Zake.
Wakati watoto wanaposhiriki uzoefu wa kiroho, ushuhuda wao unakua. Maswali utakayouliza yanaweza kuwatia moyo watoto kushiriki jinsi wanavyohisi kuhusu Mwokozi na jinsi kuishi injili kulivyowabariki.(ona Kufundisha katika njia ya Mwokozi,32) Wanapofanya hivi, wanatoa ushuhuda. Fikiria jinsi unavyoweza kufanya hili unapojadili baraka ambazo huja kutokana na kuishi Amri Kumi.
Kutoka 20:12
Bwana ananitaka mimi kuheshimu wazazi wangu.
-
Wasaidie watoto wako kujifunza kirai ‘“waheshimu baba yako na mama yako” (Kutoka 20:12). Unaweza kutaka, kufafanua kwamba “kumheshimu” mtu kunaweza kumaanisha kuwaonyesha heshima au kuwaletea furaha. Yesu alifanya nini kumheshimu mama Yake wa duniani na Baba Yake wa Mbinguni? (ona Luka 2:48–51; Yohana 19:26–27). Pengine watoto wako wangeweza kufanya zamu kuigiza mambo wanayoweza kufanya ili kuwaheshimu wazazi wao, wakati watoto wengine wakibahatisha kile wanachofanya.
Kutoka 31:13, 16–17
Kuitukuza Sabato ni ishara ya upendo wangu kwa Bwana.
-
Watoto wako wangeweza kufurahia kuangalia mifano ya ishara—kama vile alama za barabarani au ishara kwenye jengo. Nini kusudi ya ishara? Watoto wako kisha wangeweza kupata neno “ishara” katika Kutoka 31:13, 16–17. Ni nini Bwana alisema ndiyo ishara kati yetu na Yeye? Shiriki na kila mmoja wenu baadhi ya njia wewe na familia yako mnjaribu kuonesha upendo wako kwa ajili ya Bwana siku ya Sabato.
Kielelezo cha Musa ameshika Amri Kumi, na Sam Lawlor (utondoti)
Kutoka 32:1–8, 19–24; 34:6–7
“Sitageuka pembeni” kutoka kwenye njia za Mungu.
-
Fikiria kutumia “Musa juu ya Mlima Sinai” (katika Hadithi za Agano la Kale, 77–82) ili kuwasaidia watoto wako kujifunza hadithi katika Kutoka 32:1–8, 19–24. Kwa nini ilikuwa makosa kwa Waisraeli kuabudu sanamu badala ya Mungu?
2:55Moses on Mount Sinai
-
Inaweza kuwa ya kufurahisha kutengeneza njia sakafuni (au kupata moja karibu na nyumba yako) kuonyesha maneno haya kutoka Kutoka 32:8: “Wamegeuka upesi kutoka njiani.” Wakati ukitembea kwenye njia, watoto wako wangeweza kuzungumza kuhusu majaribu tunayokabiliana nayo ili kugeuka kutoka kwa Mungu. Ni nini hutusaidia kubaki kwenye njia ya Mungu—na kurudi kwenye njia ikiwa tumepotea? (ona Kutoka 34:6–7).
Kwa ajili ya zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .