Njoo, Unifuate
Aprili 6–12. “Kumbukeni Siku hii, Mliyotoka Nchi ya Misri”: Kutoka 7–13


“April 6–12. ‘Kumbukeni Siku Hii, Mliyotoka Nchi ya Misri’: Kutoka 7–13,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)

“April 6–12. ‘Kumbukeni Siku hii, Mliyotoka Nchi ya Misri,’” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026

Musa na Haruni katika baraza la Farao

Mchoro wa Musa na Aaron katika baraza la Farao, na Robert T. Barrett

Kutoka 6–12: “Kumbukeni Siku hii, Mliyotoka Nchi ya Misri”

Kutoka 7–13

Tauni baada ya tauni iliitesa Misri, lakini Farao alikataa kuwaachilia Waisraeli. Na bado Mungu aliendelea kuonyesha uwezo Wake na kumpa fursa Farao ya kukubali “kwamba Mimi ndimi Bwana” na “hapana mmoja mfano wa mimi ulimwenguni mwote” (Kutoka 7:5; 9:14). Wakati huo, Musa na wana wa Israeli lazima walikuwa wakiangalia kwa mshangao maonyesho haya ya uwezo wa Mungu kwa niaba yao. Hakika ishara hizi za mwendelezo zilithibitisha imani yao kwa Mungu na ziliimarisha utayari wao wa kumfuata nabii wa Mungu Hata hivyo, baada ya tauni tisa za kutisha kushindwa kuwaachia huru Waisraeli, ilikuwa tauni ya kumi—kifo cha mzaliwa wa kwanza, ikijumuisha mzaliwa wa kwanza wa Farao—ambayo mwishowe ilimaliza ufungwa. Hii ilionekana kutosheleza kwa sababu kwa namna yoyote ile kifungo cha kiroho, hakika kuna njia moja tu ya kuepuka. Ni kwa dhabihu ya Yesu Kristo pekee, Mzaliwa wa Kwanza—damu ya Mwana Kondoo asiye na doa—ndiyo itakayotuokoa sisi.

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Kutoka 7–11

Ninaweza kuchagua kulainisha moyo wangu.

Kwa matumaini, mapenzi yako kamwe hayatapingana na mapenzi ya Mungu kama yalivyokuwa ya Farao. Bado, sote tuna nyakati ambazo mioyo yetu si laini kama inavyopaswa kuwa. Nini kinajitokeza kwako kuhusu majibu ya Farao kwa mapigo katika Kutoka 7:14–25; 8:5–32; 9:1–26; 10:12–29; 12:29–33? Tazama ufafanuzi katika Tafsiri ya Joseph Smith ya Kutoka 7:3, 13; 9:12.

Kwa nini “mgumu” ni maelezo mazuri ya moyo wa Farao? Fikiria kile unachojifunza kutoka kwenye mistari hii kuhusu kuwa na moyo laini: 1 Nefi 2:16; Mosia 3:19; Alma 24:7–8; 62:41; Etheri 12:27. Unaposoma kuhusu matokeo ya ugumu wa moyo wa Farao, tafakari hali ya moyo wako. Ni mabadiliko gani unahisi kuongozwa kuyafanya?

Kutoka 12:1–42

ikoni ya seminari
Yesu Kristo anaweza kuniokoa kwa sababu ya Upatanisho Wake.

Njia pekee kwa ajili ya Waisraeli kuepushwa na tauni ile ya kumi, iliyoelezwa katika Kutoka 11:4–5, ilikuwa ni kufuata kwa usahihi maelekezo ambayo Bwana alimpatia Musa katika Kutoka 12, tambiko linalojulikana kama Pasaka. Pasaka inatufundisha kupitia alama kwamba kama vile Bwana alivyowakomboa Waisraeli kutoka utumwani Misri, Yeye anaweza pia kutukomboa sisi kutoka kwenye utumwa wa dhambi. Ili kuchunguza ishara hii katika Kutoka 12:1–42, ungeweza kutumia chati kama hii:

Alama

Maana yamkini

Ujumbe wa Mungu kwangu

Alama

Mwanzo wa miezi (mstari wa 2; Bwana aliwaamuru Waisraeli kutumia tukio hili kuweka alama mwanzo wa kalenda yao).

Maana yamkini

Huu ulikuwa mwanzo mpya kwa Israeli. Walikuwa “wazaliwe tena.”

Alama

Mwana kondoo (mistari 3–5)

Maana yamkini

Ona Yohana 1:29; 6:54; 1 Petro 1:19.

Alama

Damu ya mwanakondoo kwenye miimo ya mlango (mistari 7, 13, 23).

Maana yamkini

Ona Mosia 4:2; Alma 12:11.

Alama

Mkate usiotiwa chachu (mstari wa 8, 15, 19–20).

Maana yamkini

Chachu, au hamira, inaweza kuwa ishara ya uharibifu kwa sababu huharibika kwa urahisi. Ona Mathayo 16:6–12; Marko 6:35.

Alama

Mboga chungu (mstari wa 8).

Maana yamkini

Ukumbusho wa uchungu wa dhambi na utumwa. Ona Kutoka 1:14; Musa 6:55.

Alama

Kula kwa haraka, kuvaa kwa kuondoka (mstari wa 11).

Maana yamkini

Ishara ya uharaka wa kuacha utumwa wa dhambi. Ona Mwanzo 39:12; 2 Timotheo 2:22

Alama

Mharibifu (mstari 13, 23)

Maana yamkini

Ona Mafundisho na Maagano 89:18–21.

Alama

Waisraeli waliwekwa huru (mistari 29–32).

Maana yamkini

Ona 2 Nefi 2:26; Mafundisho na Maagano 138:15–19, 31.

Je, unapata nini kingine katika maelekezo na alama za Pasaka ambazo hukukumbusha juu ya Yesu Kristo na Upatanisho Wake? Je, alama hizi zinapendekeza nini kwako kuhusu jinsi ya kupokea baraka za Upatanisho Wake?

Njoo kwa Kristo kwa kutambua ishara ambazo zinamshuhudia Yeye. “Vitu vyote,” Bwana alitangaza, “vimeumbwa na vimefanywa ili vinishuhudie mimi” (Musa 6:63; ona pia 2 Nefi 11:4). Katika Kutoka 12, ishara kama mwanakondoo, damu, mkate usiotiwa chachu, miujiza, na ukombozi vyote vinaelekezwa kwa Kristo. “Mara tunapokuwa tumeelewa jinsi gani vitu hivi vinahusiana na Mwokozi, vinaweza kutufundisha juu ya nguvu Zake na sifa Zake.” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,7).

Yesu akitoa sakramenti kwa Mitume Wake.

Kwa Ukumbusho Wangu, na Walter Rane

Kutoka 12:14–17, 24–27; 13:1–16

Sakramenti hunisaidia kukumbuka kukombolewa kwangu kupitia Yesu Kristo.

Mwokozi aliwaamuru Waisraeli kuadhimisha Pasaka kila mwaka ili kuwasaidia kukumbuka Yeye alikuwa amewakomboa, hata baada ya utumwa wao kuwa kumbukumbu ya mbali. Unaposoma maelekezo Yake katika Kutoka 12:14–17, 24–27; 13:1–16, fikiria kuhusu kile unachokifanya ili kukumbuka baraka za Mungu kwa ajili yako. Je, ni kwa jinsi gani wewe unaweza kuhifadhi kumbukumbu hiyo “kwa vizazi vyako vyote”? (ona Kutoka 12:14, 26–27).

Ni mifanano gani unayoiona kati ya karamu ya Pasaka na sakramenti? Unaweza kufanya nini ili “daima kumkumbuka” Yesu Kristo? (Moroni 4:3; 5:2).

Ungeweza pia kutafakari vitu vingine ambavyo Bwana anakutaka uvikumbuke; ona, kwa mfano, Helamani 5:6–12; Moroni 10:3; Mafundishon na Maagano 3:3–5, 10; 18:10; 52:40.

Ona pia Kevin W. Pearson, “Je, Bado Uko Radhi?,” Liahona, Nov. 2022, 67–69; “Always Remember Him” (video), Gospel Library; “Kwa Ukumbusho wa Kristo,” Nyimbo za Dini. na. 105.

5:27

Always Remember Him

Kwa ajili ya zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .

ikoni ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Kutoka 7–11

Bwana ana nguvu juu ya vitu vyote.

  • Mapigo yaliyoelezewa katika Kutoka 7–11 yaliwaonyesha Wamisri na Waisraeli kwamba Bwana ana nguvu kubwa. Bwana atawasaidia watoto wako maisha yao yote watakapokuwa na imani katika nguvu Zake. Ili kuwasaidia kujifunza kutoka kwenye hadithi hii, ungeweza kumpa kila mtoto karatasi iliyogawanyika katika sehemu 10, na waalike wachore picha za mapigo yaliyoelezewa katika mistari hii: Kutoka 7:17–18; 8:1–4; 8:16–17; 8:20–22; 9:1–6; 9:8–9; 9:22–23; 10:4–5; 10:21–22; 11:4–7 (ona pia “Mapigo ya Misri” katika Hadithi za Agano la Kale, 67–69). Someni pamoja Kutoka 7:5 na 9:14 elezea ni kwa nini Bwana alituma mapigo.

    2:3

    The Plagues of Egypt

  • Shiriki na watoto wako jinsi gani Bwana amekuonyesha “hapana mmoja mfano wa [Yeye] ulimwenguni mwote” (Kutoka 9:14). Waache washiriki jinsi wanavyojua kwamba Bwana ni mwenye nguvu.

Kutoka 8:28–32; 9:7

Bwana anaweza kunisaidia kuwa na moyo laini.

  • Ili kuwasaidia watoto wako wapate taswira ya kile inachomaanisha kuwa na moyo laini, inaweza kuwa ya kufurahisha kuwaonyesha kitu ambacho ni kigumu, kama vile jiwe, na kingine ambacho ni laini na chenye kufyonza, kama vile sponji. Ungeweza pia kumwaga maji juu ya vitu hivi ili kuonyesha jinsi kwa urahisi moyo laini hupokea neno la Bwana. Kisha mngeweza kusoma pamoja mistari michache inayoelezea jinsi Farao alivyojibu mapigo yaliyotumwa na Bwana (ona Kutoka 8:28–32; 9:7). Ni kipi kati ya vitu vinavyouwakilisha vyema moyo au mtazamo wa Farao? Inamaanisha nini kuwa na moyo laini? (ona Mosia 3:19).

  • Wewe na watoto wako mngeweza kutengeneza orodha ya baadhi ya vitendo ambavyo vinaweza kuonyesha wakati tunapokuwa na moyo mgumu (kwa mfano, kwa kutumia maneno yasiyo ya ukarimu au kutokuwa tayari kushiriki). Je, tunawezaje kumuonyesha Bwana tunataka kuwa na mioyo laini?

Familia ikipokea sakramenti

Kutoka 12:1–13

Sakramenti inanisaidia kumkumbuka Yesu.

  • Pasaka iliwafundisha Waisraeli kumtazamia Mwokozi na dhabihu Yake kwa ajili yetu. Mnapochunguza Kutoka 12:1–13 pamoja, wasaidie watoto wako waone uhusiano kati ya maelezo ya Pasaka na Upatanisho wa Yesu Kristo (ona pia “Pasaka” katika Hadithi za Agano la Kale, 70–74). Kwa mfano, ni kwa jinsi gani Yesu ni kama mwana kondoo aliyeelezewa katika mstari wa 5?

    2:54

    The Passover

  • Leo, tunapokea sakramenti ili kukumbuka dhabihu ya Yesu. Ungeweza kuwaonesha watoto wako picha ya sakramenti na kuzungumza kuhusu jinsi ibada hii inavyotusaidia kumkumbuka Yesu Kristo. Ungeweza kuwasaidia watoto wako watafute neno “kumbuka” katika sala za sakramenti (ona Moroni 4–5). Au imba pamoja wimbo unaopendwa kuhusu sakramenti, na wasaidie watoto wako wagundue hisia za amani walizonazo wakati wanapofikiria kuhusu Mwokozi. Ni kwa jinsi gani tunaweza kutafuta hisia hiyo wakati tunapopokea sakramenti?

Kwa ajili ya zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .

Kielelezo cha karamu ya Pasaka

Karamu ya Pasaka, na Brian Call

Ukurasa wa shughuli ya Msingi: Sakramenti inaweza kunisaidia kumkumbuka Yesu