“Machi 30–Aprili 5. ‘Atakimeza Kifo katika Ushindi’: Pasaka” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)
“Machi 30–Aprili 5. “Atakimeza Kifo katika Ushindi,’” Njoo, Unifuate Agano la Kale2026
Kielelezo cha kaburi tupu
Machi 30–Aprili 5: “Atakimeza Kifo katika Ushindi”
Pasaka
Maisha ya Yesu Kristo “ni kitovu kwa historia yote ya mwanadamu” (“Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Mitume,” Maktaba ya Injili) Hiyo inamaanisha nini? Kwa sehemu, inamaanisha kwamba maisha ya Mwokozi yanagusa hatima ya milele ya kila mwanadamu ambaye amewahi kuishi au atakuja kuishi duniani. Ungeweza pia kusema kwamba Ufufuo wa Yesu Kristo, siku ile ya kwanza ya Jumapili ya Pasaka unawaunganisha watu wote wa Mungu katika historia yote: Wale waliozaliwa kabla ya kufufuka Kwake walikutazamia kwa imani (ona Yakobo 4:4), na wale waliozaliwa baada Yake wanaangalia nyuma kwa imani. Tunaposoma hadithi za Agano la Kale na unabii, hatuoni tu jina Yesu Kristo, lakini tunaona ushahidi wa imani ya waaminio wa kale na hamu yao ya Masiya na Mkombozi wao. Hivyo sisi ambao tunaalikwa kumkumbuka Yeye tunaweza kuhisi muunganiko na wale ambao walimtazamia Yeye. Kwani hakika Yesu Kristo amebeba “maovu yetu sisi sote” (Isaya 53:6; msisitizo imeongezwa), na “katika Kristo wote watahuishwa” (1 Wakorintho 15:22; msisitizo imeongezwa).
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Manabii wa kale na wa sasa wanashuhudia juu ya dhabihu ya Mwokozi ya kulipia dhambi.
Vifungu vingi katika Agano la Kale vinaelekeza juu ya huduma ya Msssssssssssswokozi na dhabihu ya kulipia dhambi Jedwali la hapo chini limeorodhesha baadhi ya vifungu hivyo. Unaposoma mistari hii, je, ni misukumo gani inakuja kwako kuhusu Mwokozi?
|
Agano la Kale |
Agano Jipya |
|---|---|
Agano la Kale Zekaria 9:9 | Agano Jipya Mathayo 21:1–11 |
Agano la Kale Zekaria 11:12–13 | Agano Jipya Mathayo 26:14–16; 27:3–8 |
Agano la Kale Isaya 53:4 | Agano Jipya Mathayo 8:16–17; 26:36–39 |
Agano la Kale Isaya 53:7 | Agano Jipya Marko 14:60–61 |
Agano la Kale Zaburi 22:16; | Agano Jipya Yohana 19:17–18; 20:25–27 |
Agano la Kale Zaburi 22:18 | Agano Jipya Mathayo 27:35 |
Agano la Kale Zaburi 69:21 | Agano Jipya Mathayo 27:34, 48 |
Agano la Kale Zaburi 118:22 | Agano Jipya Mathayo 21:42 |
Agano la Kale Isaya 53:9, 12 | Agano Jipya Mathayo 27:57–60; Marko 15:27–28 |
Agano la Kale Isaya 25:8 | Agano Jipya Marko 16:1–6; Luka 24:6 |
Agano la Kale Danieli 12: 2 | Agano Jipya Mathayo 27:52–53 |
Unabii ambao unafundisha kuhusu Mwokozi ni hata mwingi mno na wa wazi zaidi katika Kitabu cha Mormoni. Fikiria jinsi gani imani yako inaimarishwa na vifungu kama hivi: 1 Nefi 11:31–33; 2 Nefi 25:13; Mosia 3:2–11; Alma 7:10–13.
Manabii wa siku za mwisho wanaendelea kutoa ushahidi maalum juu ya Yesu Kristo na misheni Yake ya kulipia dhambi. Unaposikiliza mkutano mkuu wikiendi hii ya Pasaka, andika muhtasari wa shuhuda juu ya Kristo ambao unasikia. Zinakufundisha nini kuhusu Mungu?
Yesu Kristo hutoa kwangu amani na shangwe.
Pasaka ni wakati wa furaha, kwa sababu ni wakati wa kusherehekea Upatanisho na Ufufuko wa Mwokozi. Na bado, hata wakati wa Pasaka, kuna watu wengi ambao hawahisi furaha kwa sababu mbalimbali. Unaweza kufanya nini ili kueneza amani na shangwe ya Mwokozi Pasaka hii?
Wazo mojawapo ni kutafuta jumbe katika maandiko kuhusu amani na shangwe ambayo Yesu Kristo anatoa, kama hizi: Zaburi 16:8–11; 30:2–5; Isaya 12; 25:8–9; 40:28–31; Yohana 14:27; 16:33; Alma 26:11–22. Fikiria jinsi unavyoweza kushiriki jumbe hizi na wengine. Kwa mfano, pengine ungeweza kutengeneza kadi za Pasaka ili kushiriki, kulingana na jumbe hizi. Kuwa mwenye kuomba kuhusu nani anahitaji kupokea salamu zako za Pasaka. Unaweza pia kuamua kushiriki jumbe zako kwenye mitandao ya kijamii, ambako watu wengi wanaweza kuziona.
Nyimbo kuhusu Kristo na Ufufuko, kama vile “Kafufuka!” (Nyimbo za Dini, na. 199), zinaweza pia kutusaidia kuhisi amani na furaha katika Pasaka. Tafuta virai katika wimbo ambao, kwa maoni yako, vinaleta furaha ya Pasaka.
Ona pia Jeffrey R. Holland, “Si kama Ulimwengu Utoavyo,” Liahona, Mei 2021, 35–38; Mark S. Palmer, “Huzuni Yetu Itageuzwa kuwa Shangwe,” Liahona, Mei 2021, 88–90.
Kwa Nini Unalia, na Simon Dewey (maelezo)
Kwa sababu ya Upatanisho Wake,Yesu Kristo anao uwezo wa kunisaidia mimi kushinda dhambi, kifo, majaribu, na madhaifu.
Hapa kuna shughuli ambayo inaweza kukusaidia kuona baraka nyingi zinazokuja kupitia Yesu Kristo na Upatanisho Wake. Soma maandiko hapa chini kuhusu kile Yesu Kristo anachotusaidia kushinda. Jaribu kupanga vifungu katika makundi haya: dhambi, kifo, majaribu, na madhaifu (baadhi ya vifungu vinaweza kutosheleza katika zaidi ya aina moja). Unaposoma, ni misukumo ipi unayo kuhusu nguvu ya Mwokozi?
-
Isaya 61:1–3
-
Ezekieli 36:26–28.
-
Mathayo 11:28–30
-
Luka 1:46–55
-
Warumi 8:35–39
Ni kwa jinsi gani unaweza kumwelezea rafiki ambaye si Mkristo kwa nini Yesu Kristo ni muhimu kwako? Ujumbe wa Mzee Ahmad S. Corbitt “Je, Unajua Kwa Nini Mimi kama Mkristo Ninaamini katika Kristo?” Liahona, Mei 2023, 119-21, 97–101.) inaweza kusaidia
Ona pia Reyna I. Aburto, “Kaburi Halina Ushindi,” Liahona, Mei 2021, 85–87; Mada na Maswali, “Upatanisho wa Yesu Kristo,” “Ufufuko,” Maktaba ya Injili.
Yesu Kristo alilipa gharama ya mwisho kwa ajili ya dhambi zangu.
Tunajifunza nini kutoka mistari ifuatayo kuhusu gharama ambayo Yesu Kristo alilipa kwa ajili ya wokovu wako: Isaya 53:3–5; Mosia 3:7; Mafundisho na Maagano 19:16–19? Ni gharama gani Baba wa Mbinguni alilipa? (Ona Yohana 3:16).
Kwa ajili ya zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Yesu Kristo aliteseka na alikufa kwa ajili yangu.
-
Wiki ya Pasaka ni wakati mzuri wa kuwafundisha watoto wako kuhusu kile Mwokozi alichofanya kwa ajili yetu katika Gethsemane na juu ya msalaba. Unaweza kuanza kwa kuwaonesha picha zilizopo hapa chini na kuwaacha wazungumze kuhusu kile kinachotendeka katika picha. Wakati watoto wako wakiangalia picha, ungeweza kusoma mistari ambayo inaelezea matukio hayo (ona Mathayo 26:36–46; 27:35–50; Luka 22:39–46; Yohana 19:16–30). Watoto wako wangeweza kuonyesha maelezo katika picha ambazo wanazisikia katika mistari.
Kushoto Kristo akiwa Gethsemane, na Harry Anderson Kulia Kusulubishwa, na Harry Anderson
-
Ni kwa jinsi gani tunabarikiwa kwa sababu ya dhabihu ya Yesu kwa ajili yetu? Wasaidie watoto wako watafute maneno na virai ambavyo vinajibu swali hili katika Isaya 53:4–12; Alma 7:11–13; na Mafundisho na Maagano 19:16–19. Shiriki na kila mmoja jinsi unavyohisi kuhusu Mwokozi baada ya kusoma maandiko haya.
Yesu Kristo alifufuka kwa ajili yangu.
-
Ungeweza kutumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii au picha zingine katika muhtasari huu kuwasimulia watoto wako hadithi ya Ufufuko (ona pia “Yesu Amefufuka,” katika Hadithi za Agano Jipya, 139–44). Kisha acha watoto wako wasimulie hadithi hiyo tena kwako.
-
Fikiria jinsi utakavyo wasaidia watoto wako wapate shangwe katika Kristo Pasaka hii. Kwa mfano, mngeweza kuimba pamoja wimbo wa Pasaka unaoupenda zaidi, kama vile “Mwokozi Amefufuka” (Nyimbo za Dini. Kanisa, na. 200) au “Gethsemane” (Gospel Library). Ili kupata nyimbo nyingine kuhusu Ufufuko ungeweza kutafuta katika kiambatisho cha mada za Nyimbo za Dini na Kitabu cha Nyimbo za Watoto. Wewe na watoto wako mngeweza kushiriki na kila mmoja wenu kwa nini mnapenda nyimbo hizi na jinsi mnavyohisi mnapoziimba. Nyimbo hizi zinatufundisha nini juu ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?
Watoto Wanaweza Kumhisi Roho lakini yawezekana wakahitaji msaada wa kutambua ushawishi Wake. “Wafundishe watoto kuhusu njia tofauti Roho anazowasiliana nasi. Wasaidie kutambua sauti Yake wakati Yeye anaposema nao. Hii itawasaidia waokukuza tabia ya kutafuta na kufanyia kazi ufunuo binafsi maisha yao yote” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 32). Kwa mfano, mnapoimba nyimbo kuhusu Mwokozi pamoja na watoto wako, tazameni picha Zake, au someni hadithi kumhusu Yeye, shiriki na kila mmoja hisia za kiroho mlizonazo.
-
Maktaba ya Injili ina mkusanyiko wa video za Pasaka ambazo watoto wako wanaweza kufurahia. Pengine ungeweza kuwaacha wachukue moja kutazama. Waulize kile wanachojifunza kuhusu Yesu Kristo kutoka kwenye video hiyo. Unaweza pia kuwaomba wafupishe ujumbe wa video katika sentensi moja.
Manabii wanashuhudia juu ya Yesu Kristo na Upatanisho Wake.
-
Wakati wewe na watoto mnapotazama mkutano mkuu pamoja wikiendi hii ya Pasaka, wasaidie kutambua wakati mashahidi maalum wa Mwokozi wanapotoa ushuhuda juu ya Ufufuko. Pengine ungeweza kutengeneza mchezo wake—waalike wasimame kila mara wanaposikia maneno kama Pasaka au Upatanisho au Ufufuko. Shiriki na kila mmoja kwa nini mna shukrani kwa shuhuda za manabii walio hai juu ya Mwokozi.
Kwa ajili ya zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .