EnglishConnect kwa ajili ya Wamisionari
Faida za Kujifunza Kiingereza ni Nini?


“Manufaa ya Kujifunza Kiingereza ni Nini?,” EnglishConnect kwa ajili ya Mwongozo wa Kujifunza kwa Wamisionari

“Faida za Kujifunza Kiingereza ni Nini?,” EC kwa ajili ya Mwongozo wa Kujifunza kwa W

wazee wamisionari wawili wakijifunza pamoja

Faida za Kujifunza Kiingereza ni Nini?

Kujifunza Kiingereza kunaweza kukubariki wewe kama mmisionari na kuongeza fursa zako za baada ya misheni kwa ajili ya huduma, elimu na ajira.

7:9

Huduma

“Kama huzungumzi Kiingereza, unapaswa kujifunza kama mmisionari. Hii itakubariki wakati wa misheni yako na kote katika maisha yako” (Hubiri Injili Yangu, 140). Kujifunza Kiingereza wakati wa misheni yako kunaweza kutoa fursa kwako na kwa mwenza wako za kuimarishana na kusaidiana. “Wasaidieni wenza wenu wapate mafanikio na wapate kujiamini katika kujifunza lugha ya misioni au kujifunza Kiingereza. Kwa dhati na mara kwa mara wapongezeni wenza wenu na wamisionari wengine kwa maendeleo yao” (Hubiri Injili Yangu, 142). Unaporejea nyumbani, unaweza kutumia ujuzi wako wa Kiingereza kuwasaidia wengine. “Endelea kutumia lugha yako ya misheni baada ya kurudi nyumbani. Bwana amewekeza sana ndani yako, na Yeye anaweza kuwa na matumizi ya uwezo wako wa lugha hapo baadaye katika maisha yako” (Hubiri Injili Yangu, 140).

Elimu

Wamisionari vijana wote wanao maliza huduma yao ya misheni (ikijumuisha wale wanaopumzishwa mapema na wamisionari watoa huduma) wana idhini ya awali kwa ajili ya BYU–Pathway Worldwide na hupokea punguzo la ada. Wakati wamisionari wanapokamilisha kozi ya mtandaoni ya EnglishConnect 3 au wamepata maksi ya kufuzu kwenye tathmini ya lugha ya Kiingereza, wanaweza kuondolewa tathmini ya Kiingereza ya kujiunga BYU–Pathway Worldwide. BYU–Pathway ni programu ya chuo kikuu inayotoa vyeti vya mtandaoni na shahada.

Ajira

Kujifunza Kiingereza kunaweza kuongeza fursa za ajira. Fursa hizi zinaweza kupatikana katika maeneo yako husika au za mtandaoni. Katika nchi ambazo Kiingereza sio lugha ya msingi, watu wanaoongea Kiingereza wametanua machaguzi yao ya ajira na wanaweza kupokea asilimia 30–50 za mshahara mkubwa kuliko mtu wa wastani asiyeongea Kiingereza.

Tembelea missionary.englishconnect.org ili kujifunza zaidi na kufikia nyenzo za ziada.