EnglishConnect kwa ajili ya Wamisionari
Karibuni kwenye EnglishConnect kwa ajili ya Wamisionari


“Karibuni kwenye EnglishConnect kwa ajili ya Wamisionari,” EnglishConnect kwa ajili ya Mwongozo wa Kujifunza kwa Wamisionari

“Karibuni,” Mwongozo wa Kujifunza kwa ajili ya ECW

Karibuni kwenye EnglishConnect kwa ajili ya Wamisionari

“Kama huzungumzi Kiingereza, unapaswa kujifunza ukiwa kama mmisionari. Hii itakubariki wakati wa misheni yako na kote katika maisha yako. Kujifunza Kingereza pia kutabariki familia yako” (Hubiri Injili Yangu, 140).

wazee wamisionari wawili wakijifunza pamoja

Dhumuni

EnglishConnect kwa ajili ya Wamisionari hutolewa ili kukusaidia wewe kujifunza Kiingereza “kwa kujifunza na pia kwa imani” (Mafundisho na Maagano 88:118). EnglishConnect inaweza kukusaidia:

  • Kuongeza imani katika Yesu Kristo na Baba wa Mbinguni.

  • Kutumia kanuni za kiroho za kujifunza lugha.

  • Kukuza ujuzii wa Kiingereza.

Kujifunza Kiingereza kunaweza kukubariki wewe kama mmisionari na kuongeza fursa zako za baada ya misheni kwa ajili ya huduma, ajira na elimu—ikijumuisha BYU–Pathway Worldwide.

Ona “Faida za Kujifunza Kiingereza Ni Nini?” ili kujifunza zaidi.

Madaraja ya EnglishConnect

EnglishConnect kwa ajili ya Wamisionari ina Madaraja kadhaa ili kukusaidia kupiga hatua: EnglishConnect kwa ajili ya Wanaoanza, EnglishConnect 1, EnglishConnect 2 na EnglishConnect 3. Kila daraja lina nyenzo kwa ajili ya kujifunza binafsi na mazoezi na mwenza. Ikiwa hujapokea nyenzo zako, tafadhali wasiliana na kiongozi wako wa misioni.

mchoro wa grafu ukionyesha mtiririko kutoka EnglishConnect 1 hadi EnglishConnect 2 hadi EnglishConnect 3 na hatimaye BYU–Pathway Worldwide

Kujifunza Lugha Kila Siku

Wamisionari wana dakika 30–60 kwa ajili ya muda wa kujifunza lugha katika ratiba zao (ona Viwango vya Wamisionari kwa ajili ya Wanafunzi wa Yesu Kristo, 2.4.2). Kwa kuongezea, unaweza kufanyia mazoezi lugha ya misioni yako na Kiingereza pamoja na mwenza wako katika siku nzima.

Unaweza kutumia EnglishConnect kwa ajili ya Wamisionari wakati wa muda wa kujifunza lugha ili kukubariki wakati wa misioni yako na katika maisha yako yote.

Ona “EnglishConnect kwa ajili ya Uzoefu wa Wamisionari

akina dada wamisionari wakijifunza pamoja

Tumia kanuni katika Hubiri Injili Yangu, sura ya 7, ili kufanya mazoezi kila siku na tafuta kipawa cha ndimi.

“Kuwa na subira unapojifunza kwa sala na kufanyia mazoezi lugha. Amini kwamba Roho atakusaidia kadiri unavyoweka bidii ya dhati. Kuwa na imani kwamba unaweza kuwa na kipawa cha ndimi” (Hubiri Injili Yangu,143).