“EnglishConnect kwa ajili ya Uzoefu wa Wamisionari,” EnglishConnect kwa ajili ya Mwongozo wa Kujifunza kwa Wamisionari
“Uzoefu,” EC kwa ajili ya Mwongozo wa Kujifunza W
EnglishConnect kwa ajili ya Uzoefu wa Wamisionari
EnglishConnect inaweza kukusaidia kujifunza Kiingereza “kwa kujifunza na pia kwa imani” (Mafundisho na Maagano 88:118).
Kuanza
-
Uwapo MTC: Hudhuria kikao cha kukupa utambuzi na kupokea vitabukazi vya EnglishConnect 1 na 2. Kama bado hujapokea vitabukazi, wasiliana na kiongozi wako wa misioni.
-
Wiki 12 za Mwanzo Ukiwa Misioni: Kamilisha “Hatua za Mafanikio” za mmisionari kwenye missionary.englishconnect.org/missionary.
Kujifunza Lugha
Tumia muda wako wa kujifunza lugha ili kujifunza Kiingereza kwa muda wako na pamoja na mwenza wako. Unaweza kutumia EnglishConnect pamoja na mwenza anayezungumza Kiingereza ama la.
-
Tumia vitabu vya kiada na nyenzo ili kukamilisha shughuli za mazoezi binafsi na pamoja na mwenza. Ona “Ninafanya Nini Wakati wa Kujifunza Lugha Kila Siku?”
-
Fanyia mazoezi Kiingereza kwa siku nzima na katika makazi yako.
Fuatilia Maendeleo
-
Kamilisha tathmini iliyopangwa ya kujifunza lugha.
-
Tumia tathmini hizi kupima maendeleo yako na kubainisha maeneo ya kurekebisha.
Uthibitishaji
-
Uhamisho wa Mwisho: Kamilisha tathmini ya mwisho, pokea cheti chako cha daraja la Kiingereza na, kama unapenda, tuma maombi BYU–Pathway Worldwide.
-
Kurejea Nyumbani: Tumia cheti kwenye wasifu na katika usaili wa kazi.