“Je, Ninaanzaje?,” EnglishConnect kwa ajili ya Mwongozo wa Kujifunza kwa Wamisionari
“Anza,” EC kwa ajili ya Mwongozo wa kwa Kujifunza kwa W
Je, Ninaanzaje?
Kamilisha “Hatua za Mafanikio” kwenye missionary.englishconnect.org/missionary. Hatua hizi zitakusaidia kuweka malengo, kuchagua daraja lako na kujifunza kutumia nyenzo za kujifunzia.
Chagua Daraja Lako
Soma kuhusu madaraja ya EnglishConnect na chagua unapotaka kuanzia.
-
EnglishConnect kwa Wanaoanza: Ninajua maneno machache au sijui neno lolote katika Kiingereza.
-
EnglishConnect 1: Nina ufahamu wa herufi za Kiingereza na naweza kusema maneno ya msingi au kukariri vifungu.
-
EnglishConnect 2: Ninaweza kutunga sentensi za msingi lakini wakati mwingine napata shida kufanya maongezi rahisi.
-
EnglishConnect 3: Naweza kufanya mazungumzo ya kawaida na naweza kusoma na kuandika sentensi za msingi.
Fuata Mpango wa Kujifunza kwa daraja lako
Tumia kanuni za kujifunza lugha katika Hubiri Injili Yangu, sura ya 7, unapofanya mazoezi na kutafuta kipawa cha ndimi.
“Sehemu ya kutafuta kipaji cha ndimi ni kufanya kazi na kufanya yale yote unayoweza ili kujifunza lugha. Kuwa na subira unapojifunza kwa sala na kufanyia mazoezi lugha. Amini kwamba Roho atakusaidia kadiri unavyoweka bidii ya dhati” (Hubiri Injili Yangu, 143).