Kujifunza Kiingereza
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara


“Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara,” Mwongozo wa Utekelezaji wa EnglishConnect (2022)

“Maswali,” Mwongozo wa Utekelezaji wa EnglishConnect

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Ni marekebisho gani ninaweza kufanya kwenye nyenzo za kujifunzia na za matangazo?

Ninahitaji walimu wangapi?

Nyenzo gani ni za mwanafunzi na mwalimu kwa ajili ya EnglishConnect?

Ni kwa jinsi gani ninajua kwamba makundi haya yana mafanikio?

Ni kwa jinsi gani nitajua kama mwanafunzi anatakiwa kuwa kwenye EnglishConnect 1 au 2?

Ni marekebisho gani ninaweza kufanya kwenye nyenzo za kujifunzia na za matangazo?

Nyenzo za EnglishConnect zinalindwa na sheria ya haki miliki na hazipaswi kurekebishwa pasipo ruhusa. Ona sehemu ya “Kiambatisho A: Taarifa ya Kisheria” kwa taarifa juu ya kuomba ruhusa ya kurekebisha nyenzo.

Ninahitaji walimu wangapi?

Inapendekezwa kwamba kila kikundi kiwe na angalau walimu wawili. Kwa njia hiyo wanaweza kufundisha kama timu au kusaidiana kama mmoja hatokuwepo au ataugua.

Muhimu: Makundi ya EnglishConnect lazima yafuate sera ya Kanisa ambayo angalau watu wazima wawili wenye kuwajibika daima wanapaswa kuwepo wakati wa mkutano wa kila kikundi. Kama kuna mwalimu mmoja tu, basi mpange mwanakikundi mmoja mtu mzima kuhudhuria kila somo. Usifanye mkutano wa makundi kama angalau watu wazima wawili wenye kuwajibika hawatahudhuria.

Nyenzo gani ni za mwanafunzi na mwalimu kwa ajili ya EnglishConnect?

Nyenzo za Mwanafunzi

Wanafunzi watahitaji kupata EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi au EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi. Nyenzo za ziada pia zinapatikana ili kuboresha kujifunza. Ona orodha hapa chini kwa ajili ya maelezo ya nyenzo zote zinazopatikana kwa ajili ya wanafunzi:

  • EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi na EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi: Wanafunzi wanatumia vitabu hivi vya kiada ili kujiandaa na kushiriki katika kikundi cha mazungumzo. Kila kitabu cha kiada cha mwanafunzi kinagawanyika katika sehemu sita za masomo manne hadi matano. Kila somo linajumuisha sehemu za “Kujifunza Binafsi” na “Kikundi cha Mazungumzo.” Wanafunzi wanahimizwa kukamilisha shughuli za “Kujifunza Binafsi” kabla hawajaja kwenye kikundi cha mazungumzo. Unaweza kukipata kitabu cha kiada cha mwanafunzi na nyenzo ya sauti inayoambatana nayo katika Maktaba ya Injili au unaweza kuagiza kwenye store.ChurchofJesusChrist.org (bidhaa na. 18489 & 19563).

  • Kitabu cha kazi cha EnglishConnect 1 na Kitabu cha kazi cha EnglishConnect 2: Makundi haya ya EnglishConnect 1 na 2 kila moja kina kitabu chake cha kazi. Wanafunzi wanatumia shughuli zilizoko katika vitabu hivi vya kazi kwa ajili yao binafsi au pamoja na mwenza kama mazoezi ya ziada nje ya kikundi cha mazungumzo. Unaweza kukipata kitabu cha kazi katika Maktaba ya Injili au kukiagiza kwenye store.ChurchofJesusChrist.org (nambari ya bidhaa 17140 & 17323).

  • EnglishConnect.org: Tovuti ya EnglishConnect inajumuisha shughuli za mazoezi za kuchangamana kwa kila somo.

  • App ya Maktaba ya Injili: Wanafunzi wanaweza kusoma au kusikiliza mahubiri ya mkutano mkuu, Kitabu cha Mormoni na Nyimbo za Dini.

  • App Zinginezo na Vitabu Vinginevyo: Kuna nyenzo nyingi zilizoanzishwa ili kuwasaidia watu kujifunza Kiingereza. Wanafunzi wanapaswa “kutafuta … kutoka kwenye vitabu bora maneno ya hekima; tafuta kujifunza, hata kwa kusoma na pia kwa imani” (Mafundisho na Maagano 88:118).

Walimu wanapaswa kuwahimiza wanafunzi kujaribu aina tofauti za nyenzo na kutathmini jinsi gani kila moja inawasaidia.

Namba za Bidhaa za Duka la Kanisa

EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi

18489

EnglishConnect 2 kwa ajili ya Wanafunzi

19563

Kitabu cha Kazi cha EnglishConnect 1

17140

Kitabu cha Kazi cha EnglishConnect 2

17323

Nyenzo za Walimu

Walimu wanapaswa kujifunza EnglishConnect kwa ajili ya Walimu katika Maktaba ya Injili pamoja na nyenzo nyingine za mafunzo kwenye englishconnect.org/teacher/training. Walimu wanaweza kutumia nyenzo za uwasilishaji za EnglishConnect ili kuongoza shughuli za vikundi vya mazungumzo. Nyenzo za uwasilishaji zinapatikana kwenye englishconnect.org/resources/teaching-materials.

Ni kwa jinsi gani ninajua kwamba makundi haya yana mafanikio?

Dhumuni la EnglishConnect ni kuwasaidia wanafunzi kuongeza kujitegemea kiroho na kimwili wanapotafuta msaada wa Bwana ili kujifunza Kiingereza. Kujifunza Kiingereza kunaweza pia kupanua fursa zao za kielimu na kazi. Kozi za EnglishConnect zimesanifiwa ili kuwasaidia wanafunzi kutumia kanuni za injili wanapofanya kazi kwa pamoja ili kufikia malengo yao ya kujifunza.

Utajua walimu wanafanikiwa wakati wanapo:

  • Mwalike Roho kupitia shuhuda, sala na kuonyesha upendo na kutia moyo.

  • Toa dakika 20 hadi 30 za muda wa kikundi ili kujadili kanuni ya kujifunza kutoka katika somo.

  • Tumia muda mwingi wa kikundi kuwasaidia wanafunzi kujishughulisha katika shughuli changamani za mazoezi ya maongezi.

Utajua wanafunzi wanafanikiwa wakati wanapo:

  • Kuhudhuria bila kukoma na kushiriki kikamilifu katika vikao vya kikundi vya kila wiki.

  • Fundishaneni mmoja na mwingine, onyesheni imani na toa ushuhuda.

  • Tenda kwa imani ili kujifunza na kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku nje ya kikundi.

Ni kwa jinsi gani nitajua kama mwanafunzi anapaswa kufanya EnglishConnect 1 au 2?

Unaweza kutumia upimaji mfupi wa kuongea katika “Kiambatisho B: Usaili wa Ustadi wa Kuzungumza kwa ajili ya Kuwekwa katika Makundi ya EnglishConnect” ili kuamua kama mwanafunzi anapaswa kuwekwa katika EnglishConnect 1 au EnglishConnect 2. Kama kuna kundi moja tu, wanafunzi kutoka madaraja yote mawili wanaweza kufanya kazi pamoja kutoa na kupokea msaada.