Kujifunza Kiingereza
Wataalamu wa Kujitegemea na Kamati


“Wataalamu wa Kujitegemea na Kamati,” Mwongozo wa Utekelezaji wa EnglishConnect (2023)

“Kujitegemea,” Mwongozo wa Utekelezaji wa EnglishConnect

watu wakizungumza na kucheka

Wataalamu wa Kujitegemea na Kamati

EnglishConnect inawasaidia watu binafsi kuongeza kujitegemea kiroho na kimwili kupitia kuendeleza ujuzi wa Kiingereza katika mazingira ya imani, ushirika na ukuaji. Kwa sala fikiria ni nani angeweza kufaidika kutokana na kushiriki kama mtaalamu, mwalimu au mwanafunzi.

Unaweza kutumia EnglishConnect ili kukidhi mahitaji ya wale ulioitwa kuwahudumia. Kwa sala fikiria mahitaji ya wale unaowahudumia unapokamilisha hatua za hapo chini.

Kuunda Makundi ya EnglishConnect 1 na 2

Makundi ya EnglishConnect yanaweza kuundwa na kusimamiwa kama vile makundi mengine ya kujitegemea. Hii kwa kawaida humaanisha kwamba usimamizi wa EnglishConnect 1 na 2 umekabidhiwa kwa kamati ya kujitegemea au kamati nyingine teule.

Mtazamo wa Haraka

EnglishConnect 1 na 2 unajiunga bila malipo na hujumuisha:

  • Kikundi cha mazungumzo ya kila wiki kinachoongozwa na waumini wenyeji au wamisionari.

  • Masomo ya dakika 90.

  • Masomo 25 yaliyopangwa katika vitengo.

  • Kanuni za kujifunza “kwa kusoma na pia kwa imani” (Mafundisho na Maagano 88:118).

  • Nyenzo za kufanyia mazoezi kila siku.

  • Ufikiaji wa sauti na tafsiri katika Maktaba ya Injili.

Urefu na kasi ya masomo vinaweza kutoholewa kulingana na hali za eneo husika (ona “Mifano”).

Kabla ya Kuanzisha Kikundi

  • Shauriana na viongozi wa ukuhani juu ya ono na malengo (zaidi).

  • Ita na kuwapa mafunzo walimu (zaidi).

  • Toa nyenzo (zaidi).

  • Amua juu ya mahali na mara ngapi (zaidi).

  • Andikisha kikundi katika QuickReg (zaidi).

  • Waalike na kuwakaribisha washiriki (zaidi).

Wakati wa Kikundi

  • Kuza mazingira ya imani, ushirika na ukuaji (zaidi).

  • Saidia ukuaji wa mwalimu (zaidi).

  • Wasaidie wanafunzi kujiandaa kwa ajili ya ngazi nyingine ya EnglishConnect (zaidi).

  • Tambulisha nyenzo nyingine za Kanisa (zaidi).

  • Simamia kikundi katika QuickReg (zaidi).

Kuhitimisha Kikundi

  • Chapisha na gawa vyeti mwishoni mwa kikundi (zaidi).

  • Wasaidie wanafunzi katika kipindi cha mpito kwenda ngazi nyingine ya EnglishConnect au BYU–Pathway Worldwide (zaidi).

  • Watambue wanafunzi ambao wanaweza kuitwa kama walimu (zaidi).

  • Waalike wanafunzi kushiriki katika programu nyingine za Kanisa (zaidi).

  • Hitimisha kikundi katika QuickReg (zaidi).

  • Ripoti kwa viongozi wa ukuhani (zaidi).

Kuwaunganisha Wanafunzi kwenye Makundi ya EnglishConnect 3

EnglishConnect 3 inasaidia wanafunzi kukuza lugha ya Kiingereza cha wastani kwa ajili ya fursa za kazi na za kielimu—hasa BYU–Pathway Worldwide. Wamisionari wa huduma wa Kanisa huwezesha makundi ya EnglishConnect 3.

Kuna njia mbili za kuweza kuwasaidia wanafunzi kufikia EnglishConnect 3:

  1. Wasaidie wanafunzi kujiunga katika makundi yaliyopo sasa. EnglishConnect 3 ina makundi karibu maeneo mengi ulimwenguni. Wewe unaweza kuwasaidia wanafunzi kujiandikisha katika kikundi cha EnglishConnect 3 kwa kuwaongoza kupitia mchakato wa uombaji kwenye englishconnect.org/join. Warejelee wanafunzi walio na maswali ya ziada au masuala ya uandikishaji kwenye byupathway.org/help/contact-us.

  2. Anzisha kikundi cha EnglishConnect 3. Kama ungetaka kuanzisha kikundi cha EnglishConnect 3, tuma barua pepe kwenye learn@englishconnect.org. Mmisionari wa huduma wa Kanisa kisha atawasiliana na wewe.