Kujifunza Kiingereza
Kiambatisho A: Taarifa za Kisheria


“Kiambatisho A: Taarifa za Kisheria,” EnglishConnect kwa ajili ya Walimu (2023)

“Kaimbatisho A,” EnglishConnect kwa ajili ya Walimu

Kiambatisho A

Taarifa za Kisheria

Mahitaji ya Jumla ya Kisheria kwa ajili ya Idhinisho la Maeneo

Ofisi ya Ushauri wa Jumla (OGC) imeidhinisha miongozo ya uendeshaji ifuatayo kwa ajili ya mpango wa EnglishConnect. Miongozo hii itatumika ulimwenguni kote kwenye EnglishConnect 1 na 2 kulingana na masharti ya mahitaji ya kisheria ya nchi husika yaliyoainishwa katika muhtasari wa kisheria wa EnglishConnect kwa kila nchi (ona mahitaji mahususi ya nchi kwenye (englishconnect.org/leader/approved-locations).

  • Pata ruhusa ya mzazi kwa kila mshiriki wa umri wa miaka 18 au chini ya hapo ukitumia fomu ya ruhusa ya mzazi. Fomu zinapatikana katika lugha nyingi mtandaoni kwenye englishconnect.org/resources/leader.

    • Pata sahihi za wazazi wote kama inawezekana. Kama mtu ana umri wa miaka 18 au chini ya hapo na anaishi peke yake, ruhusa ya mzazi haihitajiki.

    • Fomu zilizojazwa zinahifadhiwa na viongozi wa eneo husika na zinapatikana kwa ajili ya ukaguzi.

  • Inahitaji walimu wakamilishe mafunzo ya Kanisa “Kuwalinda Watoto na Vijana.” Fuata viwango vyote vya nchi kwa ajili ya upimaji na kuwaita walimu wa vijana kwa ajili ya mwalimu yeyote wa EnglishConnect ambaye anamfundisha mtu yeyote aliye chini ya umri wa miaka 21.

  • Usilipishe ada au gharama yoyote kwa washiriki kwa ajili kushiriki katika mpango huu.

    • Washiriki wa EnglishConnect wanaweza kupakua nyenzo za mpango huu mtandaoni bila malipo, au matawi/kata husika zinaweza kununua nyenzo kwa ajili ya kikundi kupitia mkondo uliozoeleka wa usambazaji kwenye store.churchofjesuschrist.org. Washiriki wanaweza pia kununua nyenzo kupitia mkondo huu kama wanapenda.

    • Walimu wa EnglishConnect hawapaswi kutoa au kupokea fedha au zawadi kama sehemu ya mahusiano ya ukufunzi au ufundishaji wao kwa washiriki wa EnglishConnect.

  • Inajumuisha maudhui mengi mno ya kidini katika angalau theluthi moja ya ufundishaji wote. (Maudhui ya kidini yanapaswa kuchukua dakika 20 za kila saa la mafunzo au dakika 30 za kila dakika 90 za mafunzo.) Muhimu: Kama masomo yanatolewa kama ilivyokusudiwa na mwalimu daima anajumuisha shughuli “Jadili Kanuni ya Kujifunza” wakati wa kikundi cha mazungumzo, hili hitaji litatimizwa.

  • Fuata miongozo yote ya mpango iliyopo katika Mwongozo wa Utekelezaji kwa ajili ya EnglishConnect na kitabu cha kiada cha mwalimu, ikijumuisha kutumia usajili wa mtandaoni wa mfumo wa QuickReg (quickreg.englishconnect.org) ili kuhakikisha faragha ya data.

  • Ili kuepuka kuhatarisha viza za wamisionari au hali ya uhalali wa Kanisa katika nchi, misheni yoyote ambayo kamwe haijatumia ufundishaji Kiingereza kama mbinu ya kuwasiliana lazima kupata idhini mahususi ya OGC kabla ya kutumia nyenzo za EnglishConnect.

EnglishConnect 3 inaendeshwa na kutekelezwa na BYU-Pathway Worldwide. Kwa jinsi hiyo, inaendeshwa chini ya masharti sawa kisheria kama ya BYU–Pathway.

Utangazaji

Katika nchi ambazo utangazaji wa EnglishConnect 1 na 2 umeruhusiwa, vigingi, kata husika na misheni zinaweza kutangaza vikundi vya EnglishConnect 1 na 2 kwa jamii yote kulingana miongozo mahususi ya nchi ya matangazo (ona mahitaji mahususi ya nchi kwenye englishconnect.org/leader/approved-locations). Matangazo yanapaswa kuwa na yafuatayo:

  1. Jina la Kanisa kuwekwa kwa njia wazi.

  2. Kauli kwamba hakuna malipo kwa ajili ya EnglishConnect 1 na 2.

  3. Kauli kwamba EnglishConnect 1 na 2 hazitoi utambulisho wowote rasmi.

Haki miliki na Leseni

EnglishConnect ni mpango unaotolewa na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Haki zote za nyenzo za EnglishConnect zinamilikiwa au zina leseni ya Intellectual Reserve, Inc. kwa matumizi ya vitengo vya Kanisa kama vile vigingi, wilaya na misheni. Matumizi yoyote ya nyenzo za EnglishConnect yanahitaji ruhusa ya maandishi. Ili kuomba ruhusa ya kutumia nyenzo za EnglishConnect, tafadhali jaza fomu ya maombi kwenye Permissions.ChurchofJesusChrist.org.

Wadogo

Vikundi vya EnglishConnect lazima daima vifuate Sera za Kanisa za kuwalinda vijana (ambazo zinajumuisha washiriki wa umri wa miaka 18 au chini ya hapo. Vijana wadogo lazima wapate ruhusa ya mzazi iliyotiwa sahihi kabla ya kuhudhuria kikundi cha EnglishConnect Fomu zinapatikana katika lugha nyingi mtandaoni kwenye englishconnect.org/resources/leader. Fomu zilizojazwa lazima zihifadhiwe na viongozi wa eneo husika na zipatakane kwa ajili ya ukaguzi.

Kwa sababu wanafunzi wa EnglishConnect wanaweza kuwa vijana wadogo, viongozi wa dini wanapaswa kumsaili kila mwalimu mtarajiwa na kupitia kumbukumbu za mtahiniwa kwa ajili ya maelezo kabla ya kutoa wito. Cha ziada, angalau watu wawili wazima wenye kuwajibika wanapaswa kuwepo wakati wote wa mikutano ya kikundi. Walimu hawapaswi kufanya kazi na kijana mdogo katika faragha. Lazima ufuate sera hizi hata kama kikundi kinakutana mtandaoni.

Ushiriki wa Vijana Wadogo katika Vikundi vya Mazungumzo Mtandaoni

Vijana wadogo wanaweza kujiunga na vikundi vya mazungumzo vya EnglishConnect 1 na 2 mtandaoni tu kwa ruhusa ya mzazi na wakati kikundi kinaendeshwa na angalau walimu wawili.

Ili kuupa usalama kipaumbele, vikundi vya mazungmzo mtandaoni vinavyojumuisha vijana wadogo lazima vipangwe ili kuepuka miingiliano ya binafsi ya mtandaoni kati ya vijana wadogo na walimu. Vijana wadogo wanaweza kushiriki katika vikundi vya mazungumzo mtandaoni pale tu kama kuna walimu wawili au zaidi katika mkutano wa kikundi.

Kwa kuongezea, hakuna mkufunzi wa EnglishConnect anapaswa kutuma ujumbe, barua pepe au kuwasiliana na vijana wadogo bila kutuma nakala ya mawasiliano kwa mtu mwingine. Kwa ajili ya mazungumzo binafsi au simu, mtu mzima anapaswa kuwepo. Pale inapowezekana, mkufunzi anapaswa kusimamia miingiliano ya kikundi wakati wa kikundi cha mazungumzo mtandaoni.

Faragha

EnglishConnect ni mpango unaotolewa na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Kwa maelezo juu ya jinsi data zako binafsi zinavyochakatwa, tafadhali tembeleaChurchofJesusChrist.org na bonyeza Notisi ya Faragha chini ya ukurasa.

Washiriki wote sharti wakubali masharti ya kushiriki, ambayo yanaweza kupatikana kwenye ChurchofJesusChrist.org/legal/englishconnect-terms-of-participation. Washiriki wanaweza kukubali masharti ya kushiriki kielektroniki wakati msaidizi wa EnglishConnect anawasajili katika QuickReg.

Walimu wa EnglishConnect hawapaswi kuposti picha za wale wanaowafunza kwenye mitandao ya kijamii.

Utambulisho

EnglishConnect haitoi aina yoyote ya utambulisho rasmi, shahada au maksi kwa mpango wowote wa elimu au mafunzo au taasisi ya mafunzo. Ushiriki ni wa hiyari. Washiriki wanaweza kuacha mpango huu au kuacha kuhudhuria wakati wowote.