“Mwongozo wa Ziada,” Mwongozo wa Utekelezaji wa EnglishConnect (2023)
“Mwongozo wa Ziada,” Mwongozo wa Utekelezaji wa EnglishConnect
Mwongozo wa Ziada
Imani, Ushirika na Ukuaji
Kuza Imani, ushirika na ukuaji. Saidia kutengeneza mazingira ambapo wanafunzi wanaweza kuongeza imani, kupata uzoefu wa ushirika na kukuza uwezo wao. Unaweza kufanya hili kwa kuita walimu, kutoa vifaa na kuhakikisha kwamba wanafunzi na walimu wanazo nyenzo muhimu. Ungeweza pia kuratibu pamoja na wengine ambao wanaweza kutoa usaidizi kwa wanafunzi, kama vile wamisionari na makundi mengine ya elimu ya kujitegemea.
Viongozi wa Ukuhani
Shauriana na viongozi wa ukuhani. Hakikisha kwamba programu yako inayo idhini na usimamizi wa viongozi wa ukuhani. Viongozi wa ukuhani hujumuisha wale wanaosimamia maswala ya kujitegemea, seminari na chuo, na jitihada za umisionari. Shauriana na viongozi wa ukuhani juu ya:
-
Kuweka na kufuatilia malengo na mafanikio (ona “EnglishConnect Inasaidia Kazi ya Mungu ya Wokovu na Kuinuliwa”).
-
Kuboresha matokeo ya programu.
-
Kuita walimu wapya (ona “Walimu”).
-
Kualika wanafunzi zaidi ili kushiriki (ona “Kualika na Ufahamu”).
-
Kupanua ufikiaji (ona “Mahali na Mzunguko”).
-
Kualika wanafunzi kuchunguza nyenzo za ziada za Kanisa (ona “Kujiunga na Nyenzo Zingine za Kanisa”).
Kuripoti kwa viongozi wa ukuhani. Toa ripoti kwa viongozi wa ukuhani juu ya mafanikio na changamoto za makundi ya EnglishConnect.
Hakikisha utii wa sheria. Hakikisha kwamba programu hii ya EnglishConnect inaenda sambamba na matakwa ya kisheria ya eneo husika yanayopatikana kwenye englishconnect.org/leader/approved-locations.
Kumbuka: Nyenzo za EnglishConnect zinalindwa na sheria ya haki miliki na hazipaswi kurekebishwa pasipo ruhusa.
Ubia na Misheni
Panga kutumia EnglishConnect ili kushiriki injili. EnglishConnect inaweza kuwa sehemu muhimu ya mpango wa umisionari wa kata. Makundi ya EnglishConnect yanaweza:
-
Kuongeza fursa za kutafuta na kufundisha kwa ajili ya wamisionari.
-
Kuimarisha uhusiano kati ya waumini, marafiki wa Kanisa na wamisionari.
-
Kuwasaidia waumini wanaorudi au watu wanaofundishwa na wamisionari kuchangamana katika kata.
-
Kuwasaidia waumini kutumia kanuni za kupenda, kushiriki na kualika (ona Kitabu cha Maelezo Jumla, 23.1).
Juhudi za kuongozwa na muumini zikisaidiwa na mmisionari zitasaidia vyema zaidi kukamilisha matokeo haya. Wakati waumini wanapoongoza makundi ya EnglishConnect, washiriki wanakuwa na uwezekano mkubwa wa kujenga urafiki na waumini na kushiriki matukio ya kujenga imani. Wamisionari, viongozi wa misheni na kamati za kujitegemea wanapaswa kushauriana pamoja ili kutengeneza makundi ya EnglishConnect mahali ambapo kushiriki na kuishi injili kunakuwa rahisi na kawaida.
Waalike wamisionari kusaidia. Katika mahali ambapo vigingi au kata vinatoa makundi ya EnglishConnect, waalike wamisionari ili wasaidie kwa:
-
Kuhudhuria kwenye makundi na kufanya mazoezi wakati wa shughuli.
-
Kufanya mazoezi pamoja na wanafunzi baina ya mazungumzo ya vikundi.
-
Kufundisha baadhi ya masomo kadiri inavyohitajika.
Walimu
Jukumu la Walimu
Walimu wana jukumu muhimusana katika kumwalika Roho na kukuza imani, ushirika na ukuaji katika vikundi vya EnglishConnect. Hawahitaji kuwa wabobezi katika Kiingereza au uzoefu wa kufundisha. Hawahitaji kuzungumza lugha moja na wanafunzi. Masomo ya EnglishConnect yamesanifiwa kwa kutumia kanuni zilizothibitishwa za kujifunza lugha, na walimu watafanikiwa wanapowaongoza wanafunzi kwa upendo katika masomo haya. Walimu wanawasaidia wanafunzi kuja karibu zaidi na Mungu kupitia kujifunza Kiingereza.
Sifa za Mwalimu
Walimu wazuri wana:
-
Shauku, msisimko na mapenzi ya kufundisha Kiingereza.
-
Upendo na uvumilivu kwa wanafunzi na hamu imara ya kuona wakifanikiwa.
-
Mtazamo chanya na wa matumaini mema.
-
Wenye kutegemewa na wanapatikana ili kuongoza vikundi.
Ita walimu. Kwa sababu wanafunzi wa EnglishConnect wanaweza kujumuisha watoto wadogo, viongozi wa ukuhani wenyeji wanapaswa kuhoji kila mtu anayetazamiwa kuwa mwalimu na kurejelea kumbukumbu ya uumini wake kwa maelekezo kabla ya kutoa wito. Makundi ambayo yana watoto lazima wawepo watu wazima wawili wanaohudhuria na kufuata sera za Kanisa za kuwalinda vijana Inapendekezwa pia kwamba makundi yasiyo na watoto yawe na walimu wawili ili waweze kufundisha kama timu au kusaidiana kama mmoja hatokuwepo au ataugua.
Kuwafunza Walimu. Unaweza kuwafundisha walimu ukitumia EnglishConnect kwa ajili ya Walimu na nyenzo kwenye englishconnect.org/teacher. Unapaswa pia kumpatia mwalimu nakala ya kitabu cha kiada cha mwanafunzi na kitabu cha kazi (ona “Nyenzo”). Walimu pia wanahimizwa kukutana mara kwa mara kujadiliana pamoja, kushiriki uzoefu, kujibu maswali miongoni mwao na kurejelea nyenzo za mafunzo.
Kuwasaidia wanafunzi kuendelea hadi kuwa walimu. Walimu wanaweza kuwatambua wanafunzi katika kikundi ambao wangeweza kuandaliwa kufundisha kikundi katika siku zijazo. Kufundisha kunawasaidia wanafunzi kuendelea kukua na hupanua upatikanaji wa programu
Nyenzo
Wapatie wanafunzi nyenzo. Wanafunzi watahitaji kupata EnglishConnect 1 kwa Wanafunzi au EnglishConnect 2 kwa Wanafunzi ama kidijitali katika Maktaba ya Injili au chapisho kupitia duka la Kanisa la mtandaoni kwenye store.ChurchofJesusChrist.org. Nyenzo za ziada pia zinapatikana ili kuboresha kujifunza kwao, ikijumuisha kitabu cha kazi na shughuli za mtandaoni. Kwa maelezo juu ya nyenzo zote zinazopatikana kwa wanafunzi, ona “Zipi ni nyenzo kwa mwanafunzi na mwalimu kwa ajili ya EnglishConnect?” katika sehemu ya “Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara”.
Nyenzo Zilizopigwa Chapa
Kama unatoa nyenzo zilizopigwa chapa, kata au tawi la mahali husika linasaidia juhudi hizi kwa kutumia bajeti yao iliyopo. Kama unahitaji msaada wa fedha, marais wa vigingi wanapaswa kufuata mchakato ulioruhusiwa wa kuomba fedha. Usilipishe ada ya ushiriki kwa wanafunzi. Kama wanafunzi wanatarajiwa kununua nyenzo iliyopigwa chapa wao wenyewe, wanaweza kufanya hivyo kupitia kituo cha usambazaji cha eneo husika au duka la Kanisa la mtandaoni.
Kumbuka: vitabu vya kiada vinaweza kuchukua hadi wiki sita kufikia.
Wape walimu nyenzo. Walimu wanapaswa kujifunza EnglishConnect kwa ajili ya Walimu katika Maktaba ya Injili vile vile nyenzo nyinginezo za mafunzo kwenye englishconnect.org/teacher.
Uwasilishaji Somo kwa Njia ya Mtandao
Walimu wanaweza kutumia nyenzo za uwasilishaji wa EnglishConnect ili kusaidia kuongoza vikundi mazungumzo vya mtandaoni. Uwasilishaji wa masomo unapatikana kwenye englishconnect.org/resources/teaching-materials.
Mahali na Mara Ngapi
Amua kama utafundisha uso kw uso au kwa njia ya mtandao. Makundi ya uso kwa uso katika majengo ya Kanisa yanapendekezwa kutoa fursa za ushirika. Kama ufikiaji wa majengo ya Kanisa ni changamoto kwa washiriki, fikiria kutoa makundi ya mtandaoni. Huu “Mwongozo wa Kuongoza Makundi Mtandaoni” na “Mwongozo wa Mshiriki wa Kikundi cha Mtandaoni” unaweza kuwasaidia viongozi, walimu na wanafunzi kutengeneza mazingira ya kuvutia mtandaoni. Uwasilishaji masomo mtandaoni unapatikana kwenye englishconnect.org/resources/teaching-materials.
Amua ni mara ngapi makundi yatakutana. Makundi mengi yanakutana mara moja au mara mbili kwa wiki, lakini masomo yanaandikwa ili makundi yaweze kukutana mara nyingi zaidi kama watataka. Kumbuka kwamba wanafunzi wanahitaji muda wa kumaliza shughuli za mafunzo binafsi kabla ya kila darasa.
Amua lini na kwa muda gani makundi yatakutana. Chagueni siku na muda ambao utafaa vyema kwa wanafunzi na walimu. Makundi mengi yanakutana kwa dakika 90, lakini makundi yanaweza kukutana kwa urefu wa muda tofauti kama wanataka.
Amua muda wa vikundi na mada watakazosoma. Makundi mengi ni endelevu, ikimaanisha wanaanza tena na somo la 1 wanapomaliza kitabu cha kiada. Makundi mengine yanapitia kitabu chote cha kiada mara moja au wanasoma sehemu kadhaa tu katika kitabu hicho cha kiada.
Ona sehemu ya “Mifano” kwa ajili ya njia ambayo viongozi wanaunda makundi.
Usajili na Vyeti (QuickReg)
Kuunda na kusimamia vikundi katika QuickReg. QuickReg ni chombo kilichoidhinishwa na Kanisa ili kusimamia makundi yahusianayo na kujitegemea. Unda makundi katika QuickReg kwa kwenda kwenye quickreg.englishconnect.org. Kisha endelea kutumia QuickReg ili:
-
Kutangaza vikundi.
-
Kubadili tarehe, muda na mahali pa makundi.
-
Kuchapisha vyeti vya washiriki.
-
Badilisha hali ya mwanafunzi.
-
Hitimisha Kundi.
Tazama ukufunzi wa QuickReg kwenye englishconnect.org/leader kwa ajili ya mafunzo.
Kumbuka: Ili kutumia QuickReg, muumini lazima (1) awe na wito wa Kanisa na (2) wito wao uwe umerekodiwa katika Leader and Clerk Resources.
Kuchapisha na kutunuku vyeti kutoka QuickReg. Walimu na wataalamu wa elimu ya kujitegemea wanaweza kuchapisha na kutunuku vyeti vya ushiriki kwa wanafunzi ambao wameandikishwa katika QuickReg.
Kualika na Uhamasishaji
Tumia nyenzo za uhamasishaji. Nyenzo za uhamasishaji zinapatikana kwenye duka la Kanisa la mtandaoni kwenye store.ChurchofJesusChrist.org na kwenye englishconnect.org/resources/leader#publicity.
Alika wanafunzi. Unaweza kutumia vyanzo vilivyozoeleka vya mawasiliano ili kutangaza makundi ya EnglishConnect, kama vile akina dada na akina kaka wahudumu, wamisionari, mbao za matangazo za kata, vipeperushi na vinginevyo. Pale inaporuhusiwa na kulipiwa na tawi/kata ya eneo husika, makundi yanaweza pia kufikiria kutangaza kwenye mitandao ya kijamii au ukurasa wa tovuti wa kigingi. Kabla ya kuanzisha mbinu yoyote ya utangazaji, rejelea miongozo ya kisheria ya mahali husika kwenye englishconnect.org/leader/approved-locations.
Wakaribishe wanafunzi. Weka mpango wa jinsi gani wewe utawakaribisha wanafunzi wanapojisajili kwa ajili ya kikundi.
Waalike marafiki wa imani zingine. Unahimizwa kuwajumuisha watu kutoka hasili zingine. Siku zote onyesha heshima kwa imani za wengine wakati huo kwa uwazi ukishiriki imani yako kwamba Mungu anaweza kuwasaidia washiriki kujifunza Kiingereza.
Fikiria kuwaalika vijana. Unaweza kuunda makundi kwa ajili ya vijana tu, au unaweza kuwaalika vijana kuhudhuria pamoja na watu wazima. Katika EnglishConnect, kizazi kinachoinukia kinajifunza jinsi ya kupokea msaada wa Mungu ili kujifunza Kiingereza. Masomo haya yanaweza kuwasaidia kuwa na imani kwamba Mungu atawasaidia katika vipengele vyote vya maisha yao.
Fuata Sera za Kanisa kwa ajili ya kumlinda kijana. Watoto wadogo (wale wa umri wa miaka 18 au wadogo zaidi na wanaishi nyumbani kwa wazazi) lazima wawe na fomu ya ridhaa ya maandishi iliyosainiwa na mzazi kabla ya kuhudhuria katika kikundi. Fomu zinapatikana katika lugha nyingi kwenye englishconnect.org/resources/leader. Kwa ziada, makundi ya EnglishConnect lazima siku zote yafuate sera za Kanisa ambazo angalau watu wazima wawili wenye kuwajibika wawepo wakati wote wa mikutano ya kikundi. Sera hizi lazima zifuatwe hata kama kikundi kinakutana mtandaoni.
Kuendelea hadi Ngazi Inayofuata
Kuwaelimisha wanafunzi kwenye EnglishConnect na elimu ya BYU–Pathway Worldwide pamoja na ajira. EnglishConnect na BYU–Pathway Worldwide vinatoa njia kwa wanafunzi kupata ujuzi mpya katika mazingira ya ushirika na imani. Unaweza kupata nyenzo kwenye byupathway.org/englishconnect.
Wasaidie wanafunzi kujiandikisha katika EnglishConnect 3. Ona sehemu ya “Kuunganisha Wanafunzi na Makundi ya EnglishConnect 3.”
Jiunganishe na wamisionari watoa huduma ya BYU–Pathway Worldwide. Jadili njia za kuwasaidia wanafunzi wanapokuwa katika kipindi cha mpito kutoka EnglishConnect 3 kwenda BYU–Pathway Worldwide.
Kujiunganisha na Nyenzo Nyingine za Kanisa
Kuuganishwa na nyenzo zingine za Kanisa. Fanya mpango wa kuwaunganisha washiriki na nyenzo nyingine za ziada za Kanisa, kama vile makundi mengine ya elimu ya kujitegemea, shughuli za vijana, na fursa za kujifunza zaidi kuhusu injili ya Yesu Kristo. Ona ukurasa wa “Emotional, Educational, and Employment Resources” at ChurchofJesusChrist.org kwa taarifa zaidi.