“Dhumuni,” Mwongozo wa Utekelezaji wa EnglishConnect (2023)
“Dhumuni,” Mwongozo wa Utekelezaji wa EnglishConnect
Dhumuni
EnglishConnect ni programu ya kujifunza Kiingereza inayotolewa na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Dhumuni la EnglishConnect ni kuwasaidia watu binafsi kuongeza kujitegemea kiroho na kimwili kupitia ujuzi wa Kiingereza katika mazingira ya imani, ushirika na ukuajii.
EnglishConnect Inasaidia Kazi ya Mungu ya Wokovu na Kuinuliwa
EnglishConnect inaweza kuwasaidia watoto wa Mungu:
-
Kuishi Injili ya Yesu Kristo. Katika EnglishConnect, washiriki wanatumia kanuni za kujifunza “kwa kujifunza na pia kwa imani” (Mafundisho na Maagano 88:118). Walimu na wanafunzi wanaimarisha imani yao wanapotafuta na kupokea msaada wa Bwana. (Mifano)
-
Kuwatunza wale wenye mahitaji. Ujuzi wa lugha ya Kiingereza unaweza kupanua fursa za kujitegemea na huduma. EnglishConnect inawasaidia washiriki kujiandaa kwa ajili ya fursa za huduma, ajira na elimu. Kwa nyongeza, washiriki wanahudumiana na kupendana wanapofundishana na kujifunza pamoja. (Mifano)
-
Waalike wote kuipokea injili. Katika vikundi vya EnglishConnect, washiriki wanajifunza na kutumia kanuni za injili na kujenga urafiki. Kote katika EnglishConnect, washiriki wana fursa nyingi za kumfuata Roho wanapopenda, kushiriki na kuwaalika wengine kupata uzoefu wa baraka za injili. (Mifano)