Kujifunza Kiingereza
Viongozi


“Viongozi,” Mwongozo wa Utekelezaji wa EnglishConnect (2023)

“Viongozi,” Mwongozo wa Utekelezaji wa EnglishConnect

viongozi wakizungumza na kucheka pamoja

Viongozi

EnglishConnect inafanya kazi chini ya maelekezo ya ukuhani ili kusaidia katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. EnglishConnect inaweza kutekelezwa na kata, vigingi, mabaraza ya uratibu, misheni na maeneo.

Kanuni zifuatazo zitakusaidia kuanza:

  • Weka ono. Katika mabaraza, amueni jinsi gani mtatumia EnglishConnect ili kuwasaidia watu binafsi na familia katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa.

  • Gawa majukumu EnglishConnect inaweza kuundwa kama vile programu za kujitegemea au za kielimu. Utekelezaji wa EnglishConnect unaweza kugawa majukumu yake kwa washauri wa baraza au mtaalamu wa mambo ya kujitegemea.

  • Hakikisha uwajibikaji. Ratibu usasisho wa mara kwa mara kuhusiana na matokeo ya programu. Fokasi juu ya watu binafsi na familia.

Viongozi wa Misheni.

Katika maeneo ambayo vigingi na kata hazina makundi ya EnglishConnect, viongozi wa misheni wanaweza kupanga na viongozi wa ukuhani wenyeji wa maeneo husika ili wamisionari wafundishe makundi hayo wakati viongozi wa Kanisa wenyeji wanawaandaa waumini kuuchukua jukumu hilo. Viongozi wa misheni na wamisionari wanapaswa kutumia taarifa iliyomo katika mwongozo huu na kuunganisha jitihada zao pamoja na zile za viongozi wenyeji na waumini (ona “Ubia na Misheni”).