“Muhtasari,” Mwongozo wa Utekelezaji wa EnglishConnect (2023)
“Muhtasari,” Mwongozo wa Utekelezaji wa EnglishConnect
Muhtasari
EnglishConnect ina ngazi nyingi za kuwasaidia wanafunzi kuendelea. EnglishConnect 1 na 2 huwasaidia wanafunzi kukuza ustadi wa msingi wa lugha ya Kiingereza. EnglishConnect 3 huwasaidia wanafunzi kukuza ujuzi wa lugha ya Kiingereza kwa ajili ya fursa za ajira, huduma na elimu—hususani BYU–Pathway Worldwide.
EnglishConnect ni yenye ufanisi zaidi ngazi zote zinapokuwa zinapatikana kwa wanafunzi.
Masharti ya Kushiriki
Wanafunzi lazima wawe na elimu ya lugha yao ya asili na angalau wawe na umri wa miaka 11 ili kujiunga na makundi ya EnglishConnect.
Hapa chini ni uwezo wa Kiingereza mwanafunzi anahitaji kuwa nao ili kuanza kila ngazi.
EnglishConnect 1: Kusoma alfabeti na kusema maneno ya msingi
EnglishConnect 2: Kujenga sentensi za msingi
EnglishConnect 3: Kufanya mazungumzo ya kawaida, kusoma na kuandika sentensi za msingi*
*Wanafunzi wanahitaji kufaulu upimaji wa lugha ya Kiingereza ili kujiunga na EnglishConnect 3.