Kujifunza Kiingereza
Mifano kwa ajili ya Marejeleo


“Mifano kwa ajili ya Marejeleo,” Mwongozo wa Utekelezaji wa EnglishConnect (2023)

“Mifano kwa ajili ya Marejeleo,” Mwongozo wa Utekelezaji wa EnglishConnect

Mifano kwa ajili ya Marejeleo

Hapa chini kuna baadhi ya mifano ambayo inaweza kurejelewa na mafaili mengine na kupakiwa kwa ujumla—katika “droo” za Maktaba ya Injili.

Mfano wa Seti ya 1

Hadithi ya 1—Maria

Maria alijifunza jinsi ya kupokea msaada wa Mungu ili kujifunza Kiingereza. Imani yake na matumaini yake katika Mungu yamekua na hutafuta msaada wa Wake katika vipengele vingine vya maisha yake. Sasa anatumia kanuni hizo za kujifunza ili kuboresha kujifunza kwake injili.

Hadithi ya 2—Koffi

Koffi hakuwa akihudhuria kikamilifu katika Kanisa hadi pale muumini alipomwalika kwenye kikundi cha EnglishConnect. Uzoefu alioupata akiwa pamoja na washiriki wengine ulisaidia kuwasha moto upya wa hamu yake ya kuja karibu zaidi kwa Kristo. Yeye sasa anahudhuria kanisani kila mara, anahudumu kwa uaminifu katika wito wake na anawatumikia wengine.

Mfano wa Seti ya 2

Hadithi ya 1—Excellent

Excellent huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo alimaliza EnglishConnect 2 na akapanua biashara yake ya kuwahudumia watalii wa kimataifa, ambayo iliongeza mapato yake. Excellent pia anasaidia kwa kuwatunza wengine kwa kuhudumu kama mwalimu wa EnglishConnect.

Hadithi ya 2—Zheng Min

Zheng Min aliboresha uwezo wake wa Kiingereza kupitia EnglishConnect na akajiandikisha katika BYU–Pathway Worldwide. Kwa sababu yeye anajua Kiingereza, aliweza kupata kazi yenye malipo mazuri zaidi wakati akiwa anajifunza kwenye BYU–Pathway Worldwide.

Mfano wa Seti ya 3

Hadithi ya 1—Lucas

Lucas aliwaalika marafiki zake wa mitandao ya kijamii kujiunga na kikundi cha EnglishConnect pamoja na yeye. Maria aliona posti yake na akaamua kwenda pamoja naye. Maria alivutiwa na imani na ushirika aliouhisi na kuamua kujifunza zaidi kuhusu Kanisa kutoka kwa wamisionari. Aliamua kubatizwa na sasa anahudumu kama mwalimu kwa EnglishConnect 1.