Njoo, Unifuate
Februari 23–Machi 1. “Kuna Kitu Chochote Kilicho Kigumu Kwa Bwana?”: Mwanzo 18–23


“Februari 23–Machi 1. ‘Kuna Kitu Chochote Kilicho Kigumu Kwa Bwana?’: Mwanzo 18–23,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)

“Februari 27–Machi 1. ‘Kuna Kitu Chochote Kilicho Kigumu Kwa Bwana?’,” Njoo, Unifuate: 2026

Sara amembeba mtoto Isaka

Sara na Isaka, na Scott Snow

Februari 23–Machi 1: “Kuna Kitu Chochote Kilicho Kigumu Kwa Bwana?”

Mwanzo 18–23

Maisha ya Ibrahimu na Sara, yalijaa matukio yenye kuvunja moyo na ya kufurahisha, ni ushahidi wa ukweli Ibrahimu alijifunza katika ono—kwamba tuko duniani ili kujaribiwa, “ili kuona kama [sisi] tutafanya mambo yote ambayo Bwana Mungu [wetu] ataamuru” (Ibrahimu 3:25). Je, Ibrahimu na Sara wangethibitisha kuwa waaminifu? Je, wangeendelea kuwa na imani katika ahadi ya Mungu ya kuwa na uzao mkubwa, hata wakati walikuwa bado hawana watoto katika umri wao wa uzee? Na mara Isaka alipozaliwa, je,imani yao ingestahimili lisilofikirika—amri ya kumtoa dhabihu mwana huyo wa pekee ambaye kupitia yeye Mungu aliahidi kutimiza agano lile?

Ibrahimu na Sara walimwamini Mungu, na Yeye aliwaamini (ona Mwanzo 15:6; Warumi 4:3). Katika Mwanzo 18–23, tunapata hadithi kutoka katika maisha ya Ibrahimu, Sara na wengine ambazo zinaweza kutushawishi sisi kufikiria kuhusu utayari wetu wenyewe wa kuamini ahadi za Mungu, kuukimbia uovu na kamwe tusiangalie nyuma, na kumwamini Mungu pasipo kujali dhabihu tutakayoitoa. Katika kututhibitisha sisi, Mungu pia anatuboresha.

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Mwanzo 18:9–14; 21:1–7

Bwana anatimiza ahadi Zake katika wakati Wake mwenyewe.

Bwanna amefanya ahadi tukufu kwa walio waaminifu, lakini nyakati zingine hali katika maisha yetu zinaweza kusababisha sisi kujiuliza jinsi gani ahadi hizo zinawezekana kutimia. Ibrahimu na Sara yawezekana nao walihisi hivyo. Je, unajifunza nini kutokana na uzoefu wao? Inaweza kuwa vyema kuanza kujifunza kwa kurejelea kile ambacho Bwana alimeahidi katika Mwanzo 17:4, 15–22. Je, Ibrahimuna Sara walifanyaje? (Ona Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 17:23 [katika Mwanzo 17:17, tanbihi b]; Mwanzo 18:9–12). Je, ni kwa jinsi gani Bwana alijibu ili kuwasaidia wao kuwa na imani kubwa zaidi katika ahadi Zake? (ona Mwanzo 18:14).

Je, wewe unapata nini katika mistari hii ambacho kinajenga imani yako? Je, ni uzoefu gani mwingine—katika maisha yako au ya mtu mwingine—yameimarisha imani yako kwamba Bwana atatimiza ahadi Zake katika wakati Wake na njia Yake? Unaweza pia kutafakari jinsi unavyoweza kuidhinisha imani yako wakati baraka zilizoahidiwa hazipokelewi katika maisha haya. Ni ushauri gani unaupata katika Waebrania 11:8–13 na ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Kristo Amefufuka; Imani Kwake Itahamisha Milima”? (Liahona, Mei 2021, 101–4).

Ona pia Mafundisho na Maagano 88:68.

Mwanzo 19:12–29

Bwana ananiamuru nikimbie uovu na nisitazame nyuma.

Ni masomo gani unajifunza kuhusu kuukimbia uovu unaposoma kuhusu Lutu na familia yake? Kwa mfano, ni kitu gani kinachokuvutia kuhusu kile malaika walichosema na kufanya ili kumsaidia Lutu na familia yake kuepuka kuangamia? (Ona Mwanzo 19:12–17). Je, ni kwa jinsi gani Bwana anakusaidia wewe na familia yako kukimbia na kutafuta ulinzi kutokana na vishawishi viovu katika ulimwengu? Fikiria kuhusu hali ambazo unaweza kujaribiwa “[kutazama] nyuma” (mstari wa 26) wakati unapaswa kutazama mbele kwa imani katika Mwokozi. Luka 9:62 inaongeza nini kwenye uelewa wako juu ya wazo hili?

Ona pia Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 19:9-15 (katika Kiambatisho cha Biblia).

Mwanzo 19:26

Je,ni kitu gani kisichosahihi alichofanya mke wa Lutu?

Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha:

“Ni dhahiri kabisa, kitu ambacho hakikuwa sahihi kwa mke wa Lutu kilikuwa kwamba hakuwa tu anaangalia nyuma; katika moyo wake alitaka kurudi nyuma. Ilionekana kwamba hata kabla yeye hajavuka mipaka ya jiji lile, yeye tayari alikuwa anakikosa kile ambacho Sodoma na Gomora ilikuwa imempatia. …

“Inawezekana kwamba mke wa Lutu aliangalia nyuma akiwa na chuki kwa Bwana kwa kile Yeye alichokuwa anamtaka kuacha nyuma. … Kwa hiyo si tu kwamba aliangalia nyuma; aliangalia nyuma kwa kutamani. Kwa kifupi, upendo wake kwa yaliyopita ulizidi kujiamini kwake kwa siku za baadaye. Hiyo, inaonekana, angalau ilikuwa ndio sehemu ya dhambi yake.

“… Ninawasihi nyinyi, msiwepo kwenye siku zilizopita wala kutamani bure kwa siku za jana, hata kama jana hizo mzuri zilikuwa za kupendeza sana. Yaliyopita ni ya kujifunza kutokana nayo lakini siyo ya kuyaishi. Tunatazama nyuma kudai kaa la moto kutoka kwenye uzoefu unaowaka na si majivu. Na tunapookuwa tumejifunza kile tunachokihitaji kujifunza na tumeleta pamoja nasi ubora ambao tumepata uzoefu, hivyo tunatazama mbele na kukumbuka kwamba imani siku zote imeelekezwa kuelekea siku za badaaye .. …

“… kuishi kwenye maisha ya zamani, ikijumuisha makosa yaliyopita, kwa kweli sio sahihi! Sio injili ya Yesu Kristo.”

“Kwa [watu] wote wa kila kizazi, ninakuombeni, ‘Mkumbukeni mke wa Lutu’ [Luka 17:32]. Imani ni kwa ajili ya wakati ujao. Imani hujenga juu ya yaliyopita lakini kamwe haitamani kukaa hapo. Imani huamini kwamba Mungu ana mambo makuu ghalani kwa ajili ya kila mmoja wetu na kwamba hakika Kristo ni ‘kuhani mkuu wa mambo mema yajayo’ (Waebrania 9:11)” (“Yaliyo Bora Bado Hayajakuwa,” Ensign, Jan. 2010, 24, 26).

Ibrahimu akitazama kuelekea mbinguni na kisu mkononi mwake na Isaka akiwa amelala juu ya madhabahu

Ibrahimu na Isaka, na Harold Copping

Mwanzo 22:1–19

ikoni ya seminari
Utayari wa Ibrahimu wa kumtoa dhabihu Isaka ni mfano wa Mungu na Mwanawe.

Ingawa hatujui sababu zote za Mungu kumwamuru Ibrahimu kumtoa Isaka kama dhabihu; tunajua ilikuwa ni jaribio la imani yake kwa Mungu. Pia tunajua ilikuwa “mfano wa Mungu na Mwanawe wa Pekee” (Yakobo 4:5). Unaposoma Mwanzo 22:1–19, ungeweza kutafuta ishara au mifanano kati ya toleo la Ibrahimu la Isaka na toleo la Baba la Mwanawe, Yesu Kristo. Fikiria kuandika kile unachokipata katika chati kama hii:

Ibrahimu na Isaka

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo

Ibrahimu na Isaka

Isaka alikuwa mwana pekee wa Ibrahimu na Sara (Mwanzo 22:2; ona pia Waebrania 11:17)

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo

Yesu ndiye Mwana Pekee wa Baba (Yohana 3:16)

Ibrahimu na Isaka

Isaka alipaswa kutolewa mahali pa mwanakondoo (Mwanzo 22:7–9)

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo

Yesu Kristo ni Mwanakondoo wa Mungu (Yohana 1:29)

Ni ishara au mifanano ipi ya dhabihu ya Mwokozi ya kulipia dhambi unayoipata kuwa ya maana zaidi? Fikiria kuimba au kusoma mashairi ya wimbo ambao unaonyesha upendo wa Baba wa Mbinguni kwetu, kama vile “Mungu Alitupenda Sisi, Hivyo Alimtuma Mwanawe,” Nyimbo za Dini, na. 187. Unaweza pia kuandika hisia zako kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo na dhabihu Yao kwa ajili yako.

Kama unataka kujifunza zaidi kuhusu dhabihu ya Mwokozi wetu, fikiria kusoma ujumbe wa Rais Jeffrey R. Holland “Tazama Mwanakondoo wa Mungu” (Liahona, Mei 2019, 44–46). Kwa nini mwanakondoo ni ishara yenye nguvu sana ya Mwana wa Mungu? Ni nini Rais Holland alifundisha ambacho kinaongeza staha yako kwa zawadi ya Baba wa Mbinguni?

Ona pia “Akedah (The Binding)” (video), Maktaba ya Injili

12:57

Akedah (The Binding)

Tumia vielelezo vyo kuona ili kufundisha. Kuongeza aina mbalimbali katika kufundisha na kujifunza, unaweza kutumia moja au zaidi ya picha katika muhtasari huu unapojifunza hadithi katika Mwanzo 18–23. Kwa mfano, wewe na familia yako au darasa lako mngeweza kuandika maelezo kwa kina katika picha za Ibrahimu na Isaka. Zungumza kuhusu kwa nini maelezo haya ya kina ni muhimu kwa hadithi, na utafute maelezo haya ya kina katika maandiko. Ni kwa jinsi gani zinaonyesha ishara ya hadithi ya dhabihu ya Mwana wa Mungu?

Kwa ajili ya zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .

ikoni ya 01 ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Mwanzo 17: 5:15 PM-21; 18:14; 21:1–7

Ninaweza kumuamini Mungu kutimiza ahadi Zake.

  • Kujifunza kuhusu uaminifu wa Ibrahimu na Sara katika ahadi za Mungu, wewe na watoto wako mngeweza kuzungumza kuhusu wakati ambapo iliwabidi wasubiri kitu fulani walichokitaka sana. Kisha ungeweza kuangalia picha ya Sara na Isaka mwanzoni mwa muhtasari huu na kuzungumza kuhusu ahadi Mungu aliyoitoa kwake na ibrahimu (ona pia ona pia “Ibrahimu na Sara,” katika Hadithi za Agano la Kale, 28–31). Wasaidie watoto wako kufikiria vitu ambavyo Mungu ametuahidi ikiwa tutakuwa waaminifu. Wahimize kuwa wavumilivu na kuamini kwamba Mungu atatimiza ahadi Zake.

    2:20

    Abraham and Sarah

  • Ili kuwasaidia watoto wako wajifunze ukweli muhimu katika Mwanzo 18:14, ungeweza kuandika kila neno kutoka sentensi ya kwanza ya mstari huo kwenye vipande tofauti vya karatasi. Kisha changanya karatasi, na waalike watoto wako wapange maneno haya katika utaratibu sahihi. Wewe na watoto wako mngeweza kisha kusoma Mwanzo 17:15–21; 21:1–7 kupata mfano wa kitu ambacho Bwana alifanya ambacho kilionekana hakiwezekani. Shiriki na watoto wako imani yako ambayo Bwana atatimiza ahadi Zake, hata kama zinaonekana haziwezekani au kuchukua muda mrefu.

Mwanzo 19:15–26

Naweza kuukimbia uovu.

  • Waulize watoto wako kuhusu hali ambazo mtu anaweza kuwaalika kufanya kitu wanachojua si sahihi. Je, tunawezaje “kukimbia” hali hizi? Fupisha Mwanzo 19:15–26 na uelezee kwamba familia ya Lutu iliishi katika mji mwovu sana, na malaika wakawaonya waondoke. Wakati wewe na watoto wako mkisoma pamoja mstari wa 15–17, 26, waulize kile inachoweza kumaanisha kwetu leo “kuepuka” uovu na “msiangalie nyuma” (mstari wa 17).

mwanaume na wanawake wakikimbia kutoka Sodoma na Gomora

Sodoma, na Julius Schnorr von Carolsfeld

Mwanzo 22:1–14

Ibrahimu alimtii Bwana.

  • Kutumia picha za Ibrahimu na Isaka na ya Kusulubiwa (ona Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 957) inaweza kuwasaidia watoto wako kulinganisha hadithi katika Mwanzo 22 pamoja na dhabihu ya Mwokozi (ona Mathayo 27:26–37). Je, Tunaweza kujifunza nini juu ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kutoka kwa simulizi za Ibrahimu na Isaka na ya Kusulubiwa? (Ona pia “Ibrahimu na Isaka,” katika Hadithi za Agano la Kale, 34–37.)

    2:0

    Abraham and Isaac

  • Je, unaweza kufikiria mchezo rahisi wa kucheza na watoto wako ambao unawahitaji kufuata maelekezo? Labda maelekezo yangeweza kuongoza kwenye picha iliyofichwa ya Mwokozi. Mchezo ungeweza kuchochea mazungumzo kuhusu mambo ambayo Baba wa Mbinguni ametuamuru kufanya ili tuweze kuishi Naye na Yesu Kristo tena. Fikiria kuimba pamoja wimbo kama vile “Keep the Commandments” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146–47). Ukurasa wa shughuli ya wiki hii pia unaweza kusaidia.

Kwa ajili ya zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .

Ibrahimu akimwangalia Isaka akiwa amebeba mzigo wa kuni

Ibrahimu na Isaka, na Jeff Ward

ukurasa wa shughuli ya Msingi: Ibrahimu alimtii Bwana