“Februari 16-22. ‘Kuwa Mfuasi Mkubwa wa Haki’: Mwanzo 12–17; Ibrahimu 1–2,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)
“Februari 16-22. ‘Kuwa Mfuasi Mkubwa wa Haki’,” Njoo, Unifuate: 2026
Melkizedeki Akimbariki Abramu, na Walter Rane (maelezo)
Februari 16–22: “Kuwa Mfuasi Mkubwa wa Haki”
Mwanzo 12–17; Ibrahimu 1–2
Kwa sababu ya agano Mungu alilofanya na yeye, Ibrahimu amekuwa akiitwa “baba wa walio waaminifu” (Mafundisho na Maagano 138:41) na “Rafiki wa Mungu” (Yakobo 2:23). Mamilioni leo wanamheshimu kama babu yao halisi, na wengine wameasiliwa katika familia yake kupitia uongofu katika injili ya Yesu Kristo. Ingawa Ibrahimu mwenyewe amekuja kutoka katika familia iliyokuwa na matatizo—baba yake, ambaye aliitelekeza ibada za kweli za Mungu, alijaribu kumtoa Ibrahimu kuwa dhabihu kwa miungu wa uongo. Licha ya haya, tamaa ya Ibrahimu ni “kuwa mfuasi mkubwa wa haki” (Ibrahimu 1:2), na historia ya maisha yake inaonyesha kwamba Mungu aliheshimu tamaa yake. Maisha ya Ibrahimu yanasimama kama ushuhuda kwamba bila kujali historia ya familia ya mtu ilivyokuwa, hatima yake inaweza kujawa na matumaini.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Mungu atanibariki mimi kwa ajili ya imani yangu na tamaa yangu ya haki.
“Sote tunashawishiwa na familia zetu [na] utamaduni wetu,” Mzee Neil L. Andersen alifundisha, “na bado naamini kuna nafasi ndani yetu ambayo kwa kipekee na kibinafsi tunaidhibiti na kuitengeneza. … Hatimaye, matamanio yetu ya ndani yanapewa uhai na yanaonekana katika chaguzi zetu na matendo yetu” (“Educate Your Desires, Elder Andersen Counsels,” ChurchofJesusChrist.org). Fikiria jinsi Ibrahimu 1:1–19 inavyoonyesha kile Mzee Andersen alifundisha. Maswali kama haya yangeweza kusaidia:
-
Je, Ibrahimu alitamani nini? Ni kwa jinsi gani matamanio yake yalikuwa dhahiri katika matendo yake? Ni kwa jinsi gani Mungu aliunga mkono matamanio yake?
-
Je, wewe tamaa zako ni zipi? Ni kwa jinsi gani ni dhahiri katika matendo yako? Ni kwa jinsi gani Mungu anakusaidia?
-
Je, ni ujumbe gani mistari hii unao kwa ajili ya wale ambao wanafamilia wao hawatamani haki?
Mojawapo ya matamanio makubwa ya Ibrahimu na Sara—kupata mtoto—yalikwenda bila kutimizwa kwa miaka mingi (ona Mwanzo 15:1–6). Unajifunza nini kutoka Waebrania 11:8–13 kuhusu jinsi Ibrahimu na Sara walivyokabiliana na jaribu hili? Ni kwa jinsi gani Mwokozi anakusaidia “kukumbatia” ahadi Zake, hata kama “ziko mbali”?
Ona pia “Deliverance of Abraham” (video), Maktaba ya Injili.
Deliverance of Abraham
Mwanzo 12:1–3; 13:15–16; 15:1–6; 17:1–8, 15–22; Ibrahim 2:6–11
Mungu ananitaka mimi kufanya na kushiika maagano na Yeye.
Kwa nini ni muhimu kwako kujua kuhusu agano ambalo Mungu alifanya na Ibrahimu? Kwa sababu Mungu anataka kufanya agano sawa na hilo na wewe. Yeye aliahidi kwamba agano hili lingeendelea katika uzao wa Ibrahimu, au “watoto,” na kwamba “kadiri wengi watakavyoipokea injili hii watakuwa … wamehesabiwa uzao wako” (ona Ibrahimu 2:10–11). Kwa maneno mengine, agano linaendelea ndani yako—wakati unapobatizwa na kikamilifu zaidi unapofanya maagano hekaluni (ona Wagalatia 3:26–29; Mafundisho na Maagano 132:30–32).
Kwa sababu hiyo, ungeweza kutaka kujifunza Ibrahimu 2:6–11 na kutengeneza orodha ya nini, hasa, Mungu aliwaahidi Ibrahimu na Sara (ona pia Mwanzo 12:1–3; 13:15–16; 15:1–6; 17:1–8, 15–22). Je, ni kwa jinsi gani baraka hizi zinatumika kwako?
Baadhi ya ahadi hizi zina usambamba wa milele. Ni kwa jinsi gani ahadi ni kama nchi ya urithi au uzao mkubwa uliotimizwa milele? (ona Mafundisho na Maagano 131:1–4; 132:20–24, 28–32).
Mbali na kuahidi baraka, Mungu alimwambia Ibrahimu “kuwa baraka” (Mwanzo 12:2;; msisitizo umeongezwa). Unafikiri hiyo ina maana gani? Ni kwa jinsi gani wewe utakuwa baraka? (ona Ibrahimu 2:11).
Kufundisha kuhusu maagano, Mzee Dale G. Renlund alizungumzia kuhusu mkondo wa mawimbi katika Mto Amazon, na Rais Emily Belle Freeman alizungumza kuhusu kutembea kwenye njia ya mawe akiwa na kifundo kilichovunjika (ona “Kupata Nguvu ya Mungu kupitia Maagano,” Liahona, Mei 2023, 35–37; “Kutembea katika Uhusiano wa Agano na Kristo,” Liahona, Nov. 2023, 76–79). Pekua moja au zaidi ya jumbe hizi kwa ajili ya sentensi zinazosaidia kujibu swali “Kwa nini Mungu ananitaka nifanye maagano naye?”
Waalike watu kufundishana. Kama unaifundisha familia yako au darasa la Kanisa kuhusu maagano, fikiria kumpa kila mtu sehemu ya ujumbe wa Mzee Renlund au Rais Freeman kujifunza. Kisha wangeweza kushiriki na wanafamilia wengine au darasa kile walichojifunza. Hii inaruhusu watu kushuhudia na kujifunza kutoka kwa kila mmoja wao, na hiyo inamwalika Roho. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 26.)
Ona pia Mada na Maswali, “Agano la Ibrahimu,” Maktaba ya Injili; “Mawazo ya Kuweka Akilini: Agano,” katika nyenzo hii.
Agano la Ibrahimu, na Dilleen Marsh (utondoti)
Mwanzo 14:18–19; Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 14:25–40
“Melkizedeki alikuwa mtu wa imani.”
Fikiria kuwa ulikuwa ukimtambulisha Melkizedeki kwa mtu ambaye hakumjua. Ungesema nini? Tafuta mawazo katika Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 14:26–27, 33–38 (katika kiambatisho cha Biblia); Alma 13:13–19; Mafundisho na Maagano 107:1–4. Ni sifa zipi kama za Kristo unazozipata katika maelezo haya ya Melkizedeki? Ni kwa jinsi gani kujifunza kwako maisha ya Melkizedeki kunaleta matokeo ya jinsi unavyoutazama Ukuhani wa Melkizedeki?
Mwanzo 14:18–24; Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 14:36–40
Ibrahimu alilipa zaka.
Unajifunza nini kuhusu mtazamo wa Ibrahimu juu ya utajiri kutoka Mwanzo 14:18–24 na Joseph Smith Tafsiri, Mwanzo 14:36–40 (katika kiambatisho cha Biblia)? Kwa mfano, kumbuka majibu yake kwa mfalme wa Sodoma katika Mwanzo 14:23. Ni kwa jinsi gani kutii sheria ya zaka kumeathiri mtazamo wako wa pesa?
Mwanzo 16
Mungu ananisikia.
Unaposoma Mwanzo 16, unaweza kufikiria kuhusu wakati ambapo ulihisi ulikuwa unatendewa vibaya, kama Hajiri alivyofanya. Kumbuka kwamba “Ishmaeli” humaanisha “Mungu anasikia.” Ni kwa jinsi gani Mungu amekuonyesha kwamba Yeye amekusikia?
Ona pia “Sala ya Faragha,” Nyimbo za Dini, na. 76.
Kwa ajili ya zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Yesu Kristo anaweza kuniongoza kwa kunishika mkono.
-
Wakati wewe na watoto wako mkisoma Ibrahimu 1:18 na 2:8, mgeweza kuwaalika wasikiliza sehemu ya mwili ambayo inatajwa katika mistari yote miwili. Pengine mngeweza kucheza mchezo ambapo mtoto anafunga macho yake na unamwongoza mtoto mahali fulani kwa mkono. Kisha ungeweza kuzungumza kuhusu jinsi inavyohisi kuwa na Yesu Kristo kutuongoza kwa mkono au kutulinda.
Mwanzo 13:5–12
Ninaweza kuwa mpatanishi.
-
Watoto wako wangeweza kufurahia kuigiza hadithi kutoka Mwanzo 13:5–12, wakijifanya kuwa Ibrahimu, Lutu, na walishaji mifugo. Ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mfano wa Ibrahimu wa kuwa wapatanishi na familia au marafiki zetu? Jaribu kuigiza majibu yao.
Uchaguzi wa Lutu, na William Fredericks © Providence Collection/licensed from goodsalt.com
Mwanzo 13:16; Mwanzo 15:1–6; 17:1–8; Ibrahimu 2:9–11
Mungu ananialika kufanya maagano na Yeye.
-
Fikiria kuwaonyesha watoto wako chombo cha mchanga, nyota katika anga ya usiku, au picha mwishoni mwa muhtasari huu. Hii ingeweza kuwasaidia kuelewa ahadi za Mungu katika Mwanzo 13:16; 15:1–6. Zungumza kuhusu jinsi ulivyojifunza kuamini ahadi za Mungu, hata wakati zilipoonekana haziwezekani.
-
Kuwafundisha watoto wako kuhusu maagano, waombe wakuambie kuhusu wakati walipofanya ahadi au mtu fulani alitoa ahadi kwao. Kama inasaidia, shiriki baadhi ya mifano yako mwenyewe—ikijumuisha maagano uliyofanya na Mungu wakati wa ubatizo au hekaluni. Ni kwa jinsi gani maagano yako yameathiri uhusiano wako na Mungu? Chagua vifungu vichache kutoka Mwanzo 15:1–6; 17:1–8; Ibrahimu 2:9–11 kushiriki baadhi ya baraka ambazo Mungu aliwaahidi.Ibrahimu na Sara.
-
Kuwasaidia watoto wako wajiandae kufanya agano na Mungu wakati wanapobatizwa, ungeweza kutumia baadhi ya mawazo ya shughuli yaliyopendekezwa katika kiambatisho A au kiambatisho B.
Ibrahimu 1:12–17; Mwanzo 16:7–11
Mungu ananisikia.
-
Maisha ya Ibrahimu yalipokuwa hatarini, akamwita Mungu. Wakati Hajiri alipokuwa peke yake nyikani, alijifunza kwamba Mungu alimsikia. Fikiria kushiriki hadithi hizi mbili na watoto wako: “Ibrahimu na Sara” na “Hajiri” katika Hadithi za Agano la Kale, 28–31, 32–33. Tunajifunza nini kuhusu Mungu kutoka kwenye mistari hii? Kisha mngeweza kushiriki na kila mmoja uzoefu wa wakati ulipohisi kwamba Mungu alikusikia. Wimbo kama “A Child’s Prayer” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 12–13) ungeweza kuimarisha kanuni hii.
Abraham and Sarah
Hagar
Kwa ajili ya zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.