“Februari 9–15. ‘Nuhu Akapata Neema Machoni pa Bwana’: Mwanzo 6–11; Musa 8,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)
“Februari 9–15. ‘Nuhu Akapata Neema Machoni pa Bwana’,” Njoo, Unifuate: 2026
Yehova Anatimiza Ahadi, na Sam Lawlor
Februari 9–15: “Nuhu Akapata Neema Machoni pa Bwana”
Mwanzo 6–11; Musa 8
Kuishi katika siku za mwisho, tuna sababu maalum ya kuwa makini na hadithi ya Gharika. Wakati Yesu alipofundisha jinsi tunavyopaswa kutazamia kwa ajili ya Ujio Wake wa Pili, Yeye alisema, “Kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo pia kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Mtu” (Joseph Smith—Mathayo 1:41). Kwa nyongeza, maneno ambavyo yanaelezea siku ya Nuhu, kama “imeharibika” na “imejaa dhuluma,” yanaweza tu kuwa yanaelezea wakati wetu (Mwanzo 6:12–13; Musa 8:28). Hadithi ya Mnara wa Babeli pia yaonekana kutumika kwa siku yetu, na maelezo yake ya kiburi yakifuatiwa na mkanganyiko na kisha mgawanyiko.
Simulizi hizi za kale ni za thamani si tu kwa sababu zinatuonyesha sisi kwamba uovu unajirudia wenyewe katika historia yote. Muhimu zaidi, zinatufundisha sisi kitu cha kufanya kuhusu hilo. Nuhu “akapata neema machoni pa Bwana” (Musa 8:27) Na familia za Yaredi na kaka yake walimgeukia Bwana na walilindwa kutoka mkanganyiko na mgawanyiko uliokuwa katika Babeli (ona Etheri 1:33–43). Kama tunashangaa juu ya jinsi ya kujiweka wenyewe na familia zetu salama wakati wa uharibifu na ghasia, hadithi hizi katika milango hii zinayo mengi ya kutufundisha.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Mwanzo 6; Musa 8
Kuna usalama wa kiroho katika kumfuata nabii wa Bwana.
Je, unaona chochote katika maelezo ya siku ya Nuhu ambacho kinaonekana sawa na hali katika siku yetu? Hasa, angalia katika Musa 8:15–24, 28. Ni dhima gani unaona zikirudiwa?
Mfanano mmoja muhimu utakaouona ni kwamba Mungu alimwita Nuhu kuwa nabii, na amemwita nabii leo pia. Fikiria kutengeneza orodha ya kweli unazojifunza kuhusu manabii kutoka Musa 8:13–30. Ni kwa jinsi gani nabii wetu aliye hai ni kama Nuhu? Bila shaka, nabii wa Bwana leo hatoi onyo la Gharika au kutualika sisi kusaidia kujenga safina. Lakini anatuonya sisi kuhusu nini? Na anatualika tufanye nini? Ili kusaidia kujibu maswali haya, ungeweza kurejea sura kutoka Teachings of Presidents of the Church katika Maktaba ya Injili, hasa sehemu ya “Mialiko na Baraka Zilizoahidiwa”. Pengine ungeweza kuchagua onyo moja na mwaliko mmoja ambao unaonekana muhimu hasa kwako.
Mzee Allen D. Haynie alifundisha, “Baba mkamilifu na mwenye upendo aliye Mbinguni amechagua mpangilio wa kufunua ukweli kwa watoto Wake kupitia nabii” (“Nabii Aliye Hai kwa ajili ya Siku za Mwisho,” Liahona, Mei 2023, 25). Fikiria kujifunza ujumbe wa Mzee Haynie, ukitafuta sababu za kuwa na nabii ni ishara ya upendo wa Baba wa Mbinguni. Ni kwa jinsi gani kumfuata nabii wa Bwana kumekusaidia kujisikia salama kuishi katika siku za mwisho?
Ona pia Mada na Maswali, “Manabii,” Maktaba ya Injili; “Why Do We Have Prophets?” (video), Maktaba ya Injili.
Why Do We Have Prophets?
Mwanzo 6:5–13
Gharika ilikuwa kitendo cha rehema ya Mungu.
Baadhi ya Watu wanastaajabu kuhusu haki ya Mungu katika kutuma gharika “kumwangamiza mwanadamu” (Mwanzo 6:7). Mzee Neal A. Maxwell ilieleza kwamba wakati wa Gharika Kuu, “uharibifu ulikuwa umefikia kiwango cha kuharibu haki ya kujiamulia kwamba roho hazikuweza, katika haki, kuletwa hapa” (We Will Prove Them Herewith [1982], 58). Unaweza pia kufikiria jinsi Gharika ilivyokuwa tendo la rehema. Unapata nini katika Mwanzo 6:5–13 ambacho kinaonyesha huruma nyororo na upendo wa Bwana kwa watu?
Mwanzo 9:8–17
Ishara au alama zinanisaidia kukumbuka maagano yetu na Bwana.
Kulingana na Mwanzo 9:8–17, je, upinde wa mvua unaweza kuleta nini katika mawazo yako? Je, Tafsiri ya Joseph Smith ya, Mwanzo 9:21–25 (katika kiambatisho cha Biblia) inaongeza nini katika uelewa wako? Unaweza pia kufikiria kutengeneza orodha ya vitu vingine (kama ishara, vitu, au kitu kingine chochote) ambacho Mungu amekupa ili kukukumbusha juu ya maagano yako. Je, vitu hivi vinakufundisha nini? Ni kwa jinsi gani vinakusaidia kukumbuka?
Ona pia Gerrit W. Gong, “Daima Mkumbuke Yeye,” Liahona, Mei 2016, 108–11; “Reverently and Meekly Now,” Nyimbo za Kanisa, na. 185.
Mnara wa Babeli, na David Green
Mwanzo 11:1–9
Kumfuata Yesu Kristo ndiyo njia pekee kwenda kwa Baba wa Mbinguni.
Hadithi ya watu wa Babeli kujenga mnara yanatoa utofauti wa kuvutia kwenye hadithi ya Henoko na watu wake kujenga Sayuni, ambayo mlijifunza wiki iliyopita. Makundi yote mawili ya watu yalikuwa yakijaribu kufika mbinguni lakini katika njia tofauti. Je, ni kwa jinsi gani watu wa Sayuni waliipata mbinguni? (ona Musa 7:18–19, 53, 62–63, 69). Unajifunza nini kutoka Mwanzo 11:1–9 na Helamani 6:26–28 kuhusu watu wa Babeli? Hii inatufundisha nini kuhusu juhudi zetu wenyewe za kurudi kwenye uwepo wa Mungu? Mungu ametoa nini ili kutusaidia sisi “kufika mbinguni” Mwanzo 11:4; ona pia Yohana 3:16).
Jifunze kwa bidii. Kujifunza kunaweza kuhusisha zaidi kuliko kusoma tu au kusikiliza. Kwa mfano, unapojifunza kuhusu Mnara wa Babeli, wewe na familia yako au darasa lako mnaweza kuandika, kwenye vipande vya karatasi, vitu ambavyo vinatuondoa kutoka kwa Mungu. Kisha, kwenye vipande vingine vya karatasi, ungeweza kuandika vitu ambavyo vinatuleta karibu zaidi na Mungu. Panga kundi la kwanza la karatasi kwenye umbo la mnara na kundi la pili katika umbo la hekalu.
Kwa ajili ya zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Mwanzo 6:14–22; 7–8; Musa 8:16–24
Kumfuata nabii wa Bwana kutanibariki mimi na familia yangu.
-
Watoto wengi wanapenda hadithi ya Nuhu na safina. Fikiria kuwapa watoto wako fursa za kushiriki kuhusu kile wanachokijua kuhusu hiyo. Ili kuwasaidia, ungeweza kutumia picha katika muhtasari huu, “Nuhu na Familia Yake” katika Hadithi za Agano la Kale (22–25), na mstari wa tatu wa “Follow the Prophet” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 110–11). Wasaidie watoto wako kuigiza sehemu za hadithi—kwa mfano, kwa kujifanya kutumia zana kujenga safina au kutembea kama wanyama wanaoingia ndani ya safina.
-
Mnapozungumza kuhusu Nuhu pamoja, wasaidie watoto wako waone jinsi tulivyobarikiwa kuwa na nabii wa Mungu leo. Wasaidie watoto wako kupekua Musa 8:16–24 ili kutafuta vitu ambavyo Nuhu alifundisha ambavyo manabii wa Bwana bado wanafundisha leo. Je, ni kwa jinsi gani tunabarikiwa tunapotii mafundisho haya?
Mwanzo 9:15–16
Mungu atatimiza ahadi Zake kwangu.
-
Watoto wako pengine wangefurahia kuchora au kupaka rangi upinde wa mvua wakati ukizungumza kuhusu kile ambacho upinde huu unakiwakilisha (ona Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 9:21–25 [katika kiambatisho cha Biblia]). Mungu alitaka Nuhu na familia yake wafikirie nini wakati wo wote wanapoona upinde wa mvua?
-
Ungeweza pia kuwaonyeshe watoto wako kitu fulani ulichonacho ambacho kinakukumbusha jambo muhimu katika maisha yako, kama vile pete ya harusi, picha, au jarida. Acha watoto wako washiriki mifano yao wenyewe. Hii ingeweza kuongoza kwenye majadiliano kuhusu vitu ambavyo vinatusaidia kukumbuka maagano yetu, kama vile sakramenti, ambayo inatusaidia kukumbuka agano letu la ubatizo la kumfuata Yesu Kristo (ona Mafundisho na Maagano 20:75–79).
Mungu aliiambia familia ya Nuhu kwamba upinde wa mvua ungekuwa “ishara ya agano ninalofanya kati yangu mimi na ninyi” (Mwanzo 9:12).
Mwanzo 11:1–9
Kumfuata Yesu Kristo ndiyo njia pekee ya kwenda mbinguni.
-
Inaweza kuwa ya kufurahisha kujenga mnara kutokana na matofali au vitu vingine pamoja na watoto wako. Unapofanya hivyo, elezea kwamba watu wa Babeli walidhani wangeweza kufika mbinguni kwa kujenga mnara mrefu. Kisha ungeweza kutazama pamoja picha ya Mwokozi na kuwauliza watoto wako jinsi Yeye anavyotusaidia kufika mbinguni. Kisha mngeweza kuzungumza kuhusu mambo mnayoweza kufanya ili kumfuata Mwokozi.
-
Kwa kuongezea kwenye kusoma hadithi ya mnara wa Babeli katika Mwanzo 11:1–9, wewe na watoto wako mngeweza kusoma Helamani 6:28. Kulingana na mstari huu, kwa nini watu wa Babeli walijenga mnara? Kwa nini kujenga mnara huu ilikuwa njia isiyo sahihi ya kufika mbinguni? Kisha ungeweza kupekua 2 Nefi 31:20–21 na Helamani 3:28 kutafuta njia sahihi ya kufika mbinguni. Je, ni ushauri gani ungeweza kutoa kwa watu wa Babeli?
Kwa ajili ya zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.