Njoo, Unifuate
Mawazo ya Kuweka Akilini: Agano


“Mawazo ya Kuweka Akilini: Agano,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya na Nyumbani na Kanisani Agano la Kale 2026 (2026)

“Agano,” Njoo, Unifuate: 2026

ikoni ya mawazo

Mawazo ya Kuweka Akilini

Agano

Kote katika Agano la Kale, mara kwa mara utasoma neno agano. Leo kwa kawaida tunafikiria juu ya agano kama ahadi takatifu na Mungu, lakini katika ulimwengu wa kale, maagano yalikuwa pia ni sehemu muhimu ya maingiliano katika mtu mmoja na mwingine. Kwa ajili ya usalama na kupona kwao, watu walihitaji kuweza kuaminiana, na maagano yalikuwa ndiyo njia ya kupata kuaminiana huko.

Hivyo wakati Mungu aliponena na Henoko, Nuhu, Musa, na wengine kuhusu maagano, Yeye alikuwa akiwaalika wao kuingia katika uhusiano wa kuaminiana na Yeye. Tunaita agano hili agano jipya na lisilo na mwisho au agano la Ibrahimu—rejeleo la agano ambalo Mungu alifanya na Ibrahimu na Sara na kisha kufanywa upya na wazao wao Isaka na Yakobo (pia anaeitwa Israeli). Katika Agano la Kale, ilijulikana tu kama “agano.” Utaona kwamba Agano la Kale kimsingi ni hadithi za watu ambao walijiona wenyewe kama warithi wa agano hili—watu wa agano.

Agano la Ibrahimu linaendelea kuwa muhimu leo, hususani kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho. Kwa nini? Kwa sababu sisi pia ni watu wa agano, iwe au tusiwe wazawa halisi wa moja kwa moja wa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo. Kwa sababu hii, ni muhimu kuelewa agano la Ibrahimu ni nini na linatumikaje kwetu sisi leo.

Agano la Ibrahimu ni nini?

Ibrahimu alitaka “kuwa mfuasi mkubwa wa haki” (Ibrahimu1:2), hivyo Mungu alimwalika katika uhusiano wa agano. Ibrahimu hakuwa wa kwanza kuwa na tamaa hii, na hakuwa wa kwanza kupokea agano. Ilikuwa, hata hivyo, agano lisilo na mwisho. Ibrahimu alitafuta “baraka za mababu” (Ibrahimu 1:2)—baraka ambazo zilitolewa kwa agano kwa Adamu na Hawa na baada ya hapo kwa wale waliozitafuta baraka hizo kwa bidii.

Agano la Mungu na Ibrahimu aliahidi baraka za kupendeza: urithi wa nchi, uzao mkubwa, kupatikana kwa ibada za ukuhani, na jina ambalo litaheshimiwa na vizazi vingi vijavyo. Lakini mtazamo wa agano hili haukuwa tu juu ya baraka ambazo Ibrahimu na familia yake wangepokea bali pia juu ya baraka ambayo wao wangekuwa kwa watoto wote wa Mungu. “Nawe utakuwa baraka,” Mungu alitangaza, “na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa” (Mwanzo 12:2–3).

Je, agano hili lilimpa Ibrahimu , Sara, na wazao wao hadhi ya upendeleo miongoni mwa watoto wa Mungu? Kwa pekee katika mtazamo tu kwamba ni heshima ya kuwabariki wengine. Familia ya Ibrahimu ilikuwa “ibebe huduma hii na Ukuhani kwa mataifa yote,” kushiriki “baraka za Injili, ambazo ni baraka za wokovu, hata za uzima wa milele” (Ibrahimu 2:9, 11). Kuwa watu wa agano wa Mungu haikumaanisha walikuwa bora kuliko wengine; ilimaanisha walikuwa na wajibu wa kuwasaidia wengine kuwa bora.

Agano hili lilikuwa baraka Ibrahimu alikuwa akiitamani. Baada ya kupokea, Ibrahimu alijisemea moyoni mwake, “Mtumishi wako amekutafuta kwa dhati; sasa nimekupata” (Ibrahimu 2:12).

Hiyo ilikuwa maelfu ya miaka iliyopita, lakini agano hili limerejeshwa katika siku yetu.. Na kwa sasa inatimizwa katika maisha ya watu wa Mungu. Utimilifu wa agano unajenga kasi katika hizi siku za mwisho kadiri kazi ya Mungu inavyoendelea, ikibariki familia ulimwenguni kote. Na yoyote ambaye, kama Ibrahimu, anataka kuwa mfuasi mkubwa wa haki— yeyote anayemtafuta Bwana kwa dhati—anaweza kuwa sehemu yake.

familia mbele ya hekalu

Je, Agano la Ibrahimu lina maana gani kwangu mimi?

Wewe ni mtoto wa ahadi. Unafanya agano na Mungu wakati unapobatizwa na unapopokea sakramenti. Na unapokea utimilifu wa agano pamoja na ibada takatifu za hekaluni.

Kupitia maagano haya na ibada hizi, tunakuwa watu wa Mungu. Tumeunganishwa Kwake “kwa uhusiano usio na mwisho.” “Mara tunapofanya agano na Mungu,” Rais Russell M. Nelson amefundisha, “tunaondoka milele kwenye uwanda usio na upande wo wote milele. Mungu hatatupilia mbali uhusiano Wake na wale ambao wameunda mfungamano kama huo na Yeye. Hakika, wale wote ambao wamefanya agano na Mungu wana njia ya kupata aina maalumu ya upendo na rehema. … Kwa sababu ya agano letu na Mungu, Yeye kamwe hatachoka katika juhudi Zake za kutusaidia sisi, na kamwe sisi hatuwezi kumaliza subira Yake ya rehema kwetu.” Utaona hili katika historia ya watu wa Mungu wa agano katika Agano la Kale, na utaliona katika maisha yako mwenyewe kama mmoja wa watoto Wake wa agano.

Yesu amesimama juu ya maji na mikono akiwa amenyoosha

Usiogope, na Dan Wilson

Huu ndio uelewa wa thamani uliotolewa kwetu kwa sababu ya urejesho wa agano la Ibrahimu kupitia Nabii Joseph Smith. Hivyo basi unaposoma kuhusu maagano katika Agano la Kale, usifikiri tu kuhusu uhusiano baina ya Mungu na Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Fikiria pia kuhusu uhusiano Wake na wewe. Wakati unaposoma kuhusu ahadi ya uzao usio na idadi, usifikiri tu kuhusu mamilioni ambao leo wanamwita Ibrahimu baba yao. Fikiria pia kuhusu ahadi ya Mungu kwako ya familia za milele na ongezeko la milele. Wakati unaposoma kuhusu ahadi ya nchi ya urithi, usifikirie tu kuhusu nchi ya ahadi kwa Ibrahimu. Fikiria pia kuhusu hatima ya kiselestia ya dunia yenyewe—urithi ulioahidiwa kwa “wapole” ambao “wanamngojea Bwana” (Mathayo 5:5; Zaburi 37:9, 11). Na unaposoma kuhusu ahadi kwamba watu wa Mungu wa agano watabariki “familia zote za dunia” (Ibrahimu 2:11), usifikiri tu kuhusu huduma ya Ibrahimu au manabii wa uzao wake. Fikiria pia kuhusu wewe unaweza kufanya nini—kama mfuasi wa agano wa Yesu Kristo—kuwa baraka kwa familia zinazokuzunguka.