“Machi 9–15. ‘Bwana Alikuwa pamoja na Yusufu’: Mwanzo 37–41,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)
“Machi 9–15. ‘Bwana Alikuwa pamoja na Yusufu,” Njoo, Unifuate: 2026
Yusufu na Kaka Zake, na Sam Lawlor
Mwanzo 9–15: “Bwana Alikuwa Pamoja na Yusufu”
Mwanzo 37–41
Tunajua kwamba Mungu huwabariki watu wanaomwamini Yeye na kutii amri Zake. Lakini wakati mwingine haionekani hivyo. Wakati mwingine mtu anayemwamini Mungu ananyanyaswa na kutelekezwa na wanafamilia. Wakati mwingine mtu ambaye kwa ujasiri hukataa kuvunja sheria ya usafi wa kimwili hushtakiwa kwa uongo hata hivyo. Wakati mambo kama hayo yanapotokea kwetu, tunaweza kujaribiwa kuwa na hasira dhidi ya Mungu. Tunaweza kujiuliza, “Kuna maana gani ya kujaribu kufanya jambo sahihi kama inaonekana tu kuyafanya maisha kuwa magumu zaidi?”
Yusufu, mwana wa Yakobu, angeweza kujiuliza hivyo. Wakati mwingine, mtu huyu mwaminifu alifanikiwa; wakati mwingine, ilionekana kwamba kadiri alivyokuwa mwaminifu zaidi, ndivyo alivyokumbana na ugumu mwingi. Lakini Joseph kamwe hakumwacha Bwana, na Bwana hakumwacha Yusufu. Hiyo haimaanishi kwamba Bwana alizuia mambo mabaya kutomtokea Yusufu, lakini kupitia hayo yote, “Bwana alikuwa pamoja naye” (Mwanzo 39:3).
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Mwanzo 37:1–28; 39; 41:9–45
Bwana atakuwa nami katika dhiki yangu.
Tena na tena, bahati njema ilionekana kumwacha Yusufu, lakini Bwana kamwe hakumuacha. Unaposoma hadithi ya Yusufu, tafakari maswali kama haya: Je, Yusufu alifanya nini ili kukaa karibu na Bwana? Ni kwa jinsi gani Bwana alikuwa “pamoja naye”? (ona Mwanzo 39; 40:1–19; 41:9–45). Unajifunza nini kutokana na hadithi ya Yusufu ambacho kinaweza kukusaidia kutambua uwepo wa Bwana katika maisha yako?
Ungeweza kujiuliza maswali kama hayo hayo kuhusu maisha yako. Je, ni ushahidi gani umeuona kwamba Bwana hajakuacha katika nyakati za majaribu? Zingatia jinsi unavyoweza kushiriki uzoefu wako na wanafamilia na vizazi vya baadae (ona 1 Nefi 5:14).
Bila shaka, mtakuwa na majaribu mengine katika siku zijazo. Unaweza kufanya nini sasa ili kusaidia kuhakikisha kwamba majaribu hayakuondoi mbali na Bwana? Fikiria kujiandika barua ili kujihimiza wewe binafsi wakati ujao kuwa karibu Naye bila kujali chochote. Unaweza kujumuisha umaizi kutoka kwenye maisha ya Yusufu au kutoka kwenye ujumbe wa Mzee D. Todd Christofferson “Uhusiano Wetu na Mungu” (Liahona, Mei 2022, 78–81).
Ona pia Yohana 14:18; Warumi 8:28; Alma 36:3; Mafundisho na Maagano 121:7–8; “Abide with Me!,” Nyimbo za Dini, na. 166.
Mwanzo 37:5–11; 40; 41:1–38
Kama nitakuwa mwaminifu, Bwana ataniongoza na kunipa mwongozo wa kiungu.
Yusufu alikuwa na karama ya kutambua jumbe kutoka kwa Bwana kupitia ndoto. Je, unaweza kujifunza nini kutoka Mwanzo 37:5–11; 40:5–8; 41:14–25, 37–38 kuhusu kupokea na kuelewa ufunuo kutoka kwa Bwana? Kwa mfano, unaweza kujifunza nini kutokana na mfano wa Yusufu wakati ufunuo unapoonekana mgumu kueleweka? (ona Mwanzo 40:8; 41:16).
Tafakari jinsi Bwana anavyofunua mapenzi Yake kwako. Je, wewe unafanya nini ili kuufanyia kazi ufunuo ambao Yeye amekupatia? Je, ni kwa jinsi gani wewe unatafuta mwongozo wa ziada kutoka Kwake?
Joseph Akitafsiri ndoto za Mkuu wa Wanyweshaji na Mkuu wa Waokaji, na François Gérard
Mwanzo 39:1–20
Kwa msaada wa Bwana, ninaweza kukimbia majaribu.
Kama Yusufu angetoa ushauri juu ya jinsi ya kushinda majaribu ya kutenda dhambi ya uasherati, unafikiri angesema nini? Fikiria kuhusu hili unaposoma kuhusu uzoefu wake katika Mwanzo 39. Kwa mfano, fikiria jinsi Yusufu anavyoweza kujibu wasiwasi kama huu:
-
Kama hakuna mtu mwingine anayejua kile ninachofanya, inajalisha nini? (ona mstari wa 8–9).
-
Ninajaribu kupinga, lakini majaribu hayaonekani tu kuacha (ona mstari wa 10).
-
Ninapaswa kufanya nini ninapokuwa katika hali ambapo majaribu yana nguvu sana? (ona mstari wa 12).
Ni kwa jinsi gani ungeelezea kwa nini kutii sheria ya usafi wa kimwili ni muhimu? (ona Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi, 23–28).
Mfano wa Yusufu, bila shaka, unaweza kutumika kwa aina nyingine ya majaribu. Ukiwa na uzoefu wa Yusufu akilini, fikiria kutengeneza mpango kwa ajili ya kukwepa na kupinga vishawishi. Kwa mfano, ungeweza kufikiria juu ya majaribu na kuandika hali ili kuepuka na jinsi utakavyo “kimbia” wakati majaribu yanapoibuka.
|
Majaribu | |
|
Hali za kuepuka: | |
|
Mpango wa kujibu: |
Haya ni baadhi ya maandiko mengine ambayo yanaweza kuarifu mpango wako. Unajifunza nini kutoka kwa kila mmoja kuhusu jinsi Mwokozi anavyoweza kukusaidia kuyashinda majaribu? Mathayo 4:1–11; 1 Wakorintho 10:13; 1 Nefi 15:23–24; 3 Nefii 18:17–18.
Unapotengeneza mpango wako, inaweza pia kusaidia kufikiria kuhusu nyakati zilizopita wakati ambapo kwa mafanikio uliepuka au kupinga majaribu. Ni kwa jinsi gani Mwokozi alikusaidia? (ona 2 Nefi 4:18–33).
Mwanzo 41:15–57
Bwana atanisaidia kujiandaa kwa ajili ya magumu yamkini.
Tafsiri ya Yusufu ya ndoto ya Farao iliongoza kwenye baadhi ya ushauri wa busara na vitendo kwa ajili ya kunusurika na baa la njaa (ona Mwanzo 41:15–57). Fikiria ni jumbe zipi za kiroho Bwana anaweza kuwa nazo kwa ajili yako katika hadithi hili. Je, unahisi anakutaka ujiandae vipi kwa ajili ya shida katika siku zako zijazo?
Ona pia David A. Bednar, “Tutawajaribu,” Liahona, Nov. 2020, 8-11.
Kwa ajili ya zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Mwanzo 37
Naweza kuwa mkarimu kwa familia yangu.
-
Kusoma kuhusu hisia ngumu katika familia ya Yusufu kunaweza kuchochea mjadala kuhusu jinsi tunavyopaswa kuwatendea wanafamilia. Ili kusimulia hadithi ya Yusufu na kaka zake kutoka Mwanzo 37, ungeweza kutumia picha katika muhtasari huu au katika “Ndoto za Yusufu zenye Mwongozo wa Kiungu” (katika Hadithi za Agano la Kale, 47–51). Waruhusu watoto washiriki utondoti wanaoujua kuhusu hadithi hii. Unaweza kuwaomba watoto wako wafikirie kuwa walikuwa katika familia ya Yusufu. Wangesema nini au kufanya nini ili kuwa wapatanishi katika familia hiyo? Kwa mfano, inamaanisha nini “kuzungumza kwa amani” katika familia yetu? (mstari wa 4). Ni kwa jinsi gani Yesu Kristo ni mpatanishi katika familia ya Mungu?
2:17Joseph’s Inspired Dreams
Mwanzo 37:18–28; 39:20–23; 41:38
Mungu anaweza kunisaidia wakati mambo mabaya yanapotokea.
-
Wakati watoto wako wanapokabiliana na nyakati ngumu, wanahitaji kujua kwamba Bwana atakuwa pamoja nao, kama alivyokuwa pamoja na Yusufu. Pengine ungeweza kuwasaidia watoto wako watengeneze orodha ya vitu vigumu ambavyo vilimtokea Yusufu (ona Mwanzo 37:23–28; 39:20; au “Ndoto za Yusufu zenye Mwongozo wa Kiungu” na “Yusufu huko Misri,” katika Hadithi za Agano la Kale, 47–51, 52–56). Baada ya kila ugumu wanaopata, waalike watoto wako warudie, “Bwana alikuwa pamoja na Yusufu” (Mwanzo 39:2).
2:17Joseph’s Inspired Dreams
2:50Joseph in Egypt
-
Pengine watoto wako wangeweza kupekua Mwanzo 39:1–3, 20–23 kwa kila mfano wa kirai “Bwana alikuwa pamoja na Yusufu” na virai sawa na hivyo. Waache washiriki kile wanachofikiri kiraii hiki kinamaanisha. Ni kwa jinsi gani tunajua kwamba Bwana yu pamoja nasi? Elezeaneni kuhusu jinsi mlivyohisi Mungu alikuwa nanyie wakati wa changamoto.
Yusufu wa Misri Gerezani, na Jeff Ward (maelezo)
Mwanzo 39:7–12
Kwa msaada wa Bwana, ninaweza kukimbia majaribu.
-
Hapa kuna somo la vitendo ambalo linaweza kuwasaidia watoto wako wafuate mfano wa Yusufu wa kukimbia kutoka kwa mke wa Potifa: Tumia sumaku mbili kumwakilisha Yesu Kristo na Shetani. Tumia kifaa kidogo cha chuma, kama vile kibana karatasi, ili kutuwakilisha sisi. Kisha waache watoto wako waone jinsi ushawishi wa sumaku kwenye kifaa cha chuma una nguvu zaidi wakati wanaposogeza kitu karibu nacho. Ni kwa jinsi gani uzoefu wa Yusufu katika Mwanzo 39:7–12 unaelezea ukweli huu? Tunaweza kufanya nini ili kuondokana na dhambi na kuwa karibu zaidi na Yesu? Video “Temptation Fades as We Seek Christ in Every Thought” (Gospel Library) na wimbo kama “I Need Thee Every Hour” (Nyimbo za Dini, na. 98) zinaweza kusaidia katika mjadala huu.
2:58Temptation Fades as We Seek Christ in Every Thought
Tumia muziki. Nyimbo za dini na nyimbo takatifu nyinginezo zinaweza kuwasaidia watoto kuhisi upendo wa Mungu, kumhisi Roho, na kujifunza kweli za injili. Melodi, uzani, na mashairi rahisi vinaweza kuwasaidia watoto kukumbuka kweli za injili kwa miaka mingi ijayo. Unapoimba na watoto wako, wasaidie kugundua na kuelewa kanuni zilizofundishwa katika wimno huu” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 32).
-
Wasaidie watoto wako wafikirie juu ya majaribu wanayoweza kukabiliana nayo. Waache waigize jinsi ambavyo wangeweza “kukimbia” kutoka kwenye majaribu haya.
Kwa ajili ya zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .