Njoo, Unifuate
Machi 2–8. “Acha Mungu Ashinde”: Mwanzo 24–33


“Machi 2–8. ‘Acha Mungu Ashinde’,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)

“Machi 2–8. ‘Acha Mungu Ashinde’,” Njoo, Unifuate: 2026

Esau anauza haki yake ya kuzaliwa kwa Yakobo kwa bakuli la ndengu

Esau Anauza Haki Yake ya Kuzaliwa, na Glen S. Hopkinson (maelezo)

Machi 2–8: “Acha Mungu Ashinde”

Mwanzo 24-33

Ni kwa jinsi gani unajipatia kwa ajili yako mwenyewe baraka kutoka kwa Mungu? Unaweza kusema kwamba tukio la Yakobo, mjukuu wa Ibrahimu na Sara, ni hadithi ya mtu aliyejifunza jibu kwa swali hilo. Katika utamaduni ambapo mwana mzaliwa wa kwanza alipokea baraka ya mzaliwa wa kwanza, Yakobo alizaliwa wa pili, akishikilia kisigino cha kaka yake pacha, Esau. Jina “Yakobo” linamaanisha “twa mahali pa”—mtu anayechukua nafasi ya mtu mwingine. Yakobo aliishi kwa jina hilo kwa kujaribu, zaidi ya mara moja, kumbadili mahali pa Esau kama mrithi wa baraka ya haki ya mzaliwa wa kwanza kwa sababu Esau hakustahili (ona Mwanzo 25:30–34; 26:34–35; 27:36). Matokeo yalikuwa ya kutofautiana katika familia, na Yakobo alilazimika kukimbia kwa ajili ya uhai wake kwenda nyikani.

Miaka kadhaa baadaye, Mungu alimwamuru Yakobo kurudi nyumbani. Njiani, Yakobo, kwa unyenyekevu, tena alitafuta baraka kutoka kwa Mungu. Maandiko yanaelezea wakati huu kama “mweleka” wa Yakobo, na alitamka kwamba hangekata tamaa “sikuachi usiponibariki ” (Mwanzo 32:26). Kisha likaja somo—na baraka. Mungu alibadilisha jina la Yakobo kuwa Israeli—ikimaanisha, miongoni mwa mambo mengine, “acha Mungu ashinde.” Israeli alijifunza kwamba ili kupokea baraka za Mungu zenye thamani kubwa, baraka Zake za agano, siyo lazima kubadili mahali pa mtu mwingine. Baraka zake hazinunuliwi au kutwaliwa au kushinda. Yeye anawapatia kwa uhuru wote wanaoishi kulingana na jina la Israeli—ambao huacha Mungu ashinde katika maisha yao.

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Mwanzo 24

Ndoa ya Agano ni muhimu kwa mpango wa milele wa Mungu.

Unaposoma Mwanzo 24, jiulize kwa nini Ibrahimu alifikiria ndoa ya mwanawe Isaka kuwa muhimu sana. Kwa nini ndoa ni muhimu kwa Mungu?

Ni sifa zipi unazipata kwa Rebeka ambazo zingechangia katika ndoa na familia imara? (ona hasa mstari wa 15–28, 57–61).

Ona pia Mada na Maswali, “Ndoa,” Maktaba ya Injili.

Mwanzo 25:29–34

Ninaweza kutathamini vitu vya milele badala ya vitu vya kidunia.

Katika utamaduni wa Isaka na Rebeka, mwana mkubwa alipokea haki ya mzaliwa wa kwanza, ambayo ilimaanisha urithi mkubwa zaidi, pamoja na majukumu makubwa ya kuitunza familia. Unaposoma Mwanzo 25:29–34, tafakari kwa nini Esau alikuwa yuko tayari kutoa haki yake ya kuzaliwa kwa kubadilishana na mlo. Ni masomo gani unayoyapata kwa ajili yako mwenyewe katika hadithi hii? Inaweza kusaidia kutengeneza orodha mbili: (1) baraka za milele Mungu anazotaka kukupa wewe na (2) mambo ya kidunia ambayo yanaweza kukuvuruga kimawazo. Kisha ungeweza kusoma kifungu, kubadilisha “haki ya kuzaliwa” na kitu fulani kutoka orodha ya kwanza na “mlo”na kitu fulani kutoka orodha ya pili. Ni kwa jinsi gani utafokasi kwa Mwokozi na baraka za milele za injili Yake?

Ona pia Mathayo 6:19–33; M. Russell Ballard, “Kumbuka Kilicho Muhimu Zaidi,” Liahona, Mei 2023, 105–7.

Yakobo huko Betheli

Yakobo huko Betheli, na James Smetham

Mwanzo 28

ikoni ya seminari
Maagano ya nyumba ya Bwana huleta nguvu za Mungu katika maisha yangu.

Akiwa amelala kwenye mto wa mawe, Yakobo alikuwa na ndoto ya kubadili maisha. Ilikuwa ni kama uzoefu mtakatifu kwamba Yakobo aliita mahali pale Betheli, au “nyumba ya Mungu,” akitamka, “Kweli Bwana yupo mahali hapa” (Mwanzo 28:16).

Unaposoma Mwanzo 28, unaweza kujiuliza ni kitu gani kilifanya uzoefu huu kuwa mtakatifu sana kwa Yakobo. Alikuwa anapitia nini wakati huo? Ni kwa jinsi gani Yakobo alikuwa akihisi? Ungeweza pia kutafuta maneno na virai katika mstari wa 10–22 ambayo vinakukumbusha juu ya nyumba ya Bwana. Ni misukumo ipi unayoipokea kuhusu Mungu, nyumba Yake, na maagano Yake?

Mwishoni mwa muhtasari huu kuna mchoro unaoonyesha ndoto ya Yakobo; unaweza kuirejelea unaposoma. Kama ungetengeneza picha yako mwenyewe ya kisanii ya ndoto yake, ungefanya nini? Ni kweli zipi kutoka kwenye hadithi hii ambazo ungejaribu kuelezea?

Wimbo “Nearer, My God, to Thee” (Nyimbo za Dini, na.100) kulingana na uzoefu wa Yakobo. Ni uhusiano gani unaouona kati ya wimbo huu na Mwanzo 28:10–22? Ni kwa jinsi gani hekalu linakusaidia kuhisi uko karibu zaidi na Mungu? Fikiria kutafuta majibu ya swali hili katika ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Hekalu na Msingi Wako wa Kiroho” (Liahona, Nov. 2021, 93–96). Unaweza pia kutaka kurejelea maagano na baraka za nyumba ya Bwana katika Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 27.2 (Maktaba ya Injili). Ni kwa jinsi gani kuweka maagano haya kunaleta nguvu za Mungu ndani ya maisha yako?

Kuwa mbunifu. Kuna njia nyingi za kujifunza kutoka kwenye maandiko mbali na kuyasoma tu. Baadhi ya watu wanaona kwamba wanaelewa maandiko vyema zaidi kama watachora picha za matukio. Wengine hupata umaizi wa kiroho katika muziki mtakatifu unaohusiana na maandiko. Usijiwekee mipaka kwenye njia moja ya kujifunza; kuwa tayari kujaribu mbinu tofauti tofauti.

Mwanzo 29:31–35; 30:1–24

Bwana ananikumbuka katika majaribu yangu.

Unaposoma Mwanzo 29:31–35 na 30:1–24, tafuta maneno na yayoelezea rehema za Mungu kwa Raheli na Lea. Tafakari jinsi Bwana “alivyoangalia juu ya mateso [yako]” na “akakukumbuka” (Mwanzo 29:32; 30:22).

Mwanzo 32–33

Mwokozi anaweza kuiponya familia yangu.

Yakobo aliporudi Kanaani, alikuwa “anaogopa sana na kufadhaika sana” kuhusu jinsi ambavyo Esau angempokea (Mwanzo 32:7). Unaposoma Mwanzo 32–33, tafakari uhusiano wa familia yako mwenyewe—pengine hususani mmoja ambao unahitaji uponyaji. Pengine hadithi hii inaweza kukuvutia kumfikia mtu fulani? Maswali kama haya yangeweza kuongoza usomaji wako:

  • Je, ni kwa jinsi gani Yakobo alijiandaa kukutana na Esau?

  • Je ni kitu gani kinajitokeza kwako wewe kuhusu maombi ya Yakobo yanayopatikana katika Mwanzo 32:9–12?

  • Je, unajifunza nini kuhusu msamaha kutokana na mfano wa Esau?

  • Je, ni kwa jinsi gani Mwokozi anaweza kutusaidia kuponya uhusiano wa kifamilia?

Kwa ajili ya zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .

ikoni ya 01 ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Mwanzo 24:10–21

Naweza Kuwa mkarimu kwa wengine.

  • Ili kuangazia mfano mzuri wa ukarimu wa Rebeka, ungeweza kuwaonesha watoto wako picha iliyopo hapo chini au ukurasa wa shughuli ya wiki hii unapofanya muhtasari wa hadithi katika Mwanzo 24:10–21. Watoto wako wangeweza kufurahia kuigiza hadithi hii. Hii ingeweza kuongoza kwenye mazungumzo kuhusu matendo ya ukarimu ambayo wewe na watoto wako mmeyaona.

  • Fikiria kuimba wimbo kuhusu ukarimu pamoja, kama vile “Kindness Begins with Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 145). Watoto wako wangeweza kusikiliza kwa ajili ya neno “fadhila” (au neno linalofanana) na wasimame wanapolisikia. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa wakarimu kama Rebeka ?

mchoro wa Rebeka

Mashujaa wa Agano la Kale, na Dilleen Marsh (utondoti)

Mwanzo 25:21–34

Mambo ya milele ni muhimu zaidi kuliko mambo ya kiliulimwengu.

  • Fikiria kutumia “Yakoba na Esau” (katika Hadithi za Agano la Kale, 38–41) ili kuwasaidia watoto wako waelewe hadithi katika Mwanzo 25:21–34. Pengine watoto wako wangeweza kufikiria kwamba Esau aliomba ushauri wao kuhusu kama anapaswa kuuza haki yake ya kuzaliwa wa kwanza kwa ajili ya bakuli ya ndengu. Wao wangesema kwake?

    2:5

    Jacob and Esau

  • Ni mambo gani yaliyo muhimu milele kwako na kwa watoto wako? Pengine watoto wako wangeweza kutafuta picha au vitu ambavyo vinawakilisha vitu hivi. Ni kwa jinsi gani tunaweza kumwonyesha Bwana kwamba vitu hivi ni muhimu kwetu?

Mwanzo 28:10–22

Maagano yananisaidia kurudi kwa Baba wa Mbinguni.

  • Mnaposoma Mwanzo 28:10–22 pamoja, mnaweza kutumia ngazi inayohamishika au ngazi za ndani ya jengo (au picha kama ile iliyo mwisho wa muhtasari huu) ili kuzungumza kuhusu jinsi maagano yetu ni kama ngazi. Pengine watoto wako wangeweza kujifanya wanapanda ngazi na kwa kila hatua, zungumza kuhusu nyakati tulipoahidi kumtii Mungu kama vile tunapobatizwa, tunapopokea sakramenti au kwenda hekaluni. Je, ni kwa jinsi gani maagano yetu yanatuleta karibu zaidi na Mungu?

Mwanzo 32:6–11; 33:1–4

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanaweza kunisaidia mimi niipende familia yangu.

  • Ili kutambulisha mistari hii, unaweza kueleza kwamba baada ya miaka mingi ya hisia ngumu, Yakobo alikuwa anaenda kukutana na Esau tena. Someni pamoja Mwanzo 32:6–11. Je, Yakobo alihisi vipi? Alifanya ili kupata msaada? Someni pamoja Mwanzo 33:1–4 ili kugundua jinsi Bwana alivyojibu sala ya Yakobo. Kama Yakobo na Esau wangeweza kuongea na sisi leo, je, wangeweza kusema nini kwetu ili kutusaidia sisi wakati kunapokuwa na ugomvi katika familia zetu?

Kwa ajili ya zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .

Yakobo akiota ndoto ya ngazi na malaika wakishuka kutoka mbinguni

Ndoto ya Yakobo, na J. Ken Spencer

ukurasa wa shughuli wa Msingi: Ninaweza kuwa mkarimu kwa wengine