Njoo, Unifuate
Novemba 23–29. “Mtafuteni Bwana, nanyi Mtaishi”: Amosi; Obadia; Yona


“Novemba 23–29. ‘Mtafuteni Bwana, Nanyi Mtaishi,’Amosi; Obadia; Yona,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale,” 2026 (2026)

“Novemba 23–29. ‘Mtafuteni Bwana, Nanyi Mtaishi,’” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026

Yona alitupwa ufukweni mwa bahari

Yona kwenye Ufuko wa Ninawi, na Daniel Lewis

Novemba 23–29:“Mtafuteni Bwana, Nanyi Mtaishi”

Amosi; Obadia; Yona

Yona alikuwa kwenye merikebu iliyokuwa ikielekea Tarshishi. Hakuna chochote kibaya kwa kusafiri kwenda Tarshishi, isipokuwa kwamba ni mbali sana na Ninawi, ambapo Yona alipaswa kwenda kutoa ujumbe wa Mungu. Wakati merikebu ilipokabiliwa na dhoruba kubwa, Yona alijua ni kwa sababu ya kutotii kwake. Kwa msisitizo wa Yona, mabaharia wenzake walimtupa ndani ya kina cha bahari ili kuzuia dhoruba. Ilionekana kama mwisho wa Yona na huduma yake. Lakini Bwana hakuwa amekata tamaa na Yona—kama vile hakuwa amewaacha watu wa Ninawi, na nyumba ya Israeli au yeyote kati yetu.

Hivyo anaendelea kuwatuma manabii—kama Yona, Amosi, Obadia na manabii wetu leo—pamoja na ujumbe kwamba tukitubu, hatutatupiliwa mbali milele. Kati ya “siri”zote Mungu anazofunua (ona Amosi 3:7), hii ni miongoni mwa zile zenye thamani kubwa: kwamba kwa sababu ya Yesu Kristo, hakuna kuchelewa katika kubadilika. Bado anataka kutusaidia kuishi kulingana na maagano tuliyofanya Naye, na Yeye yuko tayari kutupatia nafasi nyingine.

Kwa muhtasari wa vitabu hivi, ona “Amosi,” “Obadia,” na “Yona” katika Kamusi ya Biblia.

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Amosi 3:1–8; 7:10–15

ikoni ya seminari
Bwana hufunua ukweli kupitia kwa manabii Wake.

Katika Amosi 3:3–6, nabii Amosi aliwasilisha mifano ya hitimisho tunaloweza kupata kutoka kwa ishara tunazosikia au kuona: wakati simba anaunguruma, lazima atakuwa imekamata mawindo; kama ndege amekamatwa katika mtego, lazima palikuwa na chambo huko. Katika mstari wa 7–8, Amosi alitumia mantiki hii kwa manabii. Ni hitimisho gani tunaweza kupata wakati nabii anapotoa unabii? Unajifunza nini zaidi kuhusu manabii kutoka kwa Amosi 7:10–15?

Bwana amefunua nini kwako kupitia manabii Wake?

Mzee Ulisses Soares alisema kwamba “kuwa na manabii ni ishara ya upendo wa Mungu” (“Manabii Wanazungumza kwa Uwezo wa Roho Mtakatifu,” Liahona, Mei 2018, 99). Fikiria jinsi ambavyo ungekamilisha sentensi hii: “Ninajua Mungu ananipenda, kwa sababu Yeye anawatuma manabii ambao …” Haya ni baadhi ya maandiko ambayo yanaweza kusaidia: Kumbukumbu la Torati 18:18; Ezekieli 3:16–17; Waefeso 4:11–14; 1 Nefi 22:2; Mafundisho na Maagano 21:4–6; 84:36–38; 107:91–92.

Ungesema nini kwa mtu ambaye anahisi manabii hawahitajiki leo?

Ona pia Mada na Maswali, “Manabii,” Maktaba ya Injili.

Amosi 4–5

“Mtafuteni Bwana, Nanyi Mtaishi.”

Kulingana na Amosi 4:6–13, ni nini Bwana alitarajia kitatokea baada ya Waisraeli kupata majaribu? (ona pia Helamani 12:3). Wakati jaribu lako linaweza kuwa halijatumwa na Mungu, tafakari jinsi linavyoweza kukupa fursa za kumtafuta Yeye.

Unaposoma Amosi 5:4, 14–15, tafakari jinsi Bwana amekuwa mwenye hisani kwako. Ni kwa jinsi gani kumtafuta Yeye kumekuletea uhai?

Amosi 8:11–12

Neno la Bwana linaweza kukidhi njaa na kiu ya kiroho.

Unaposoma Amosi 8:11–12, fikiria ni kwa nini njaa ni mfananisho mzuri wa kuishi bila neno la Mungu (ona pia Yohana 6:26–35; 2 Nefi 9:50–51; 32:3; Enoshi 1:4–8). Ni kwa jinsi gani unajua unapokuwa na njaa ya kiroho?

Mistari hii ingeweza pia kutumika katika Ukengeufu Mkuu (ona Mada na Maswali, “Ukengeufu,” Gospel Library). Ni kwa jinsi gani “njaa” hiyo ya kiroho imewaathiri watoto wa Mungu? Ni kwa jinsi gani Urejesho unakidhi njaa kiroho?

Ona pia “The Great Apostasy” (video), Maktaba ya Injili.

16:36

The Great Apostasy

Obadia 1:21.

Ni nani “waokozi … juu ya mlima Sayuni”?

Akirejelea Obadia 1:21, Rais Gordon B. Hinckley alieleza kwamba tunakuwa waokozi kwenye Mlima Sayuni wakati tunapopokea ibada kwa ajili ya wafu hekaluni (ona “Maneno ya Kufunga,” Liahona, Nov. 2004, 105). Ni kwa jinsi gani kufanya kazi hiyo kunafanana—hata kwa njia ndogo tu—na kile Mwokozi alichofanya kwa ajili yetu? Ni kwa jinsi gani kufanya kazi hii kumekusaidia kuhisi uko karibu zaidi na Mwokozi?

Ona pia “Mahekalu Matakatifu juu ya Mlima Sayuni,” Nyimbo za Kanisa, na. 289.

kundi la vijana nje ya hekalu

Yona 1–4

Bwana ni mwenye rehema kwa wote wanaomgeukia Yeye.

Ninawi ilikuwa adui wa Israeli iliyojulikana kwa vurugu na ukatili. Kwa Yona, ilionekana kutokuwa na uhakika kwamba walikuwa tayari kutubu. Ingeweza kusaidia kulinganisha mtazamo wa Yona (ona Yona 1; 3–4) na hisia za Alma na wana wa Mosia (ona Mosia 28:1–5; Alma 17:23–25). Je, unajifunza nini kutoka kwa Yona 3 ambacho kinakuhimiza kushiriki injili hata na watu ambao hawaonekani kuwa tayari kubadilika?

Unaposoma Yona, tafuta mifano ya rehema ya Bwana. Kwa nini unahisi Yona “hakupendezwa” na “kukasirika sana” (Yona 4:1) wakati Bwana alipowahurumia watu wa Ninawi? Je, unahisi Bwana alikuwa anajaribu kumfundisha nini yeye katika sura ya 4? Tafakari jinsi ulivyoona rehema Yake maishani mwako. Unajifunza nini kutoka kwa Yona ambacho kinaweza kukusaidia kuwa mwenye rehema zaidi?

ikoni ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Kwa sababu Jumapili hii ni Jumapili ya tano ya mwezi, walimu wa Watoto wanahimizwa kutumia shughuli za kujifunza katika “Kiambatisho B: Kuwaandaa Watoto kwa Ajili ya Maisha Yote kwenye Njia ya Mungu ya Agano.”

Amosi 3:7

Manabii ni wajumbe wa Yesu Kristo.

  • Ili kuwasaidia watoto wako waelewe Amosi 3:7, ungeweza kunong’ona ujumbe rahisi kwa mmoja wao na uwaombe kushiriki ujumbe pamoja na watoto wengine. Ni kwa jinsi gani mjumbe katika shughuli hii ni kama nabii? Kwa nini Bwana anatupatia sisi manabii?

  • Ili kujifunza zaidi kuhusu manabii hufanya nini, wewe na watoto wako mngeweza kurejelea jumbe za hivi karibuni kutoka kwa Rais wa Sasa wa Kanisa. Mngeweza pia kuimba wimbo kuhusu manabii, kama vile “Follow the Prophet” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 110–11). Shiriki na kila mmoja kwa nini unachagua kumfuata nabii wa Mungu.

Wasaidie watoto kukariri maandiko. Mzee Richard G. Scott alishiriki: “Kukariri andiko ni kuanzisha urafiki mpya. Ni kama kugundua mtu mpya ambaye anaweza kusaidia wakati wa shida, kutoa mwongozo wa kiungu na faraja, na kuwa chanzo cha motisha ya mabadiliko yanayohitajika” (“The Power of Scripture,” Ensign, Nov. 2011, 6). Ili kuwasaidia watoto wako kukariri yote au sehemu ya Amosi 3:7, ungeweza kuiandika na kuirudia pamoja. Kisha ungeweza kufuta au kufunika maneno machache kwa wakati mmoja mpaka watoto wako waweze kurudia mstari mzima kutoka kwenye kumbukumbu.

Amosi 8:11–12

Urejesho wa Injili ulimaliza baa la njaa ya ukengeufu.

  • Waalike watoto wako wajifanye kuwa na njaa unaposoma Amosi 8:11–12. Je, unajisikiaje tunapokuwa na njaa ya neno la Mungu? Pengine watoto wako wangeweza kujifanya wanakula wakati mnaposhiriki mmoja na mwingine baadhi ya maandiko mliyoyapenda.

  • Ungeweza kutumia Mwongozo kwenye Maandiko, “Ukengeufu” (Gospel Library), au “Baada ya Agano Jipya” (katika Hadithi za Agano Jipya, 167–70) ili kuwasaidia watoto wako waelewe “baa la njaa” ambalo lilikuja kutokana na Ukengeufu Mkuu na jinsi lilivyomalizika kwa Urejesho. Shirikianeni sababu za wewe kuwa na shukrani kwamba Bwana alirejesha injili Yake katika siku zetu.

    2:52

    After the New Testament

Yona 1–3

Bwana atanisaidia kumtii Yeye, hata wakati ni vigumu.

  • Ili kuwasaidia watoto wako kujifunza hadithi ya Yona, ungeweza kurejea “Yona Nabii” katika Hadithi za Agano la Kale; ona pia ukurasa wa shughuli ya wiki hii). Kisha ungeweza kuuliza:

    • Ni nini kilitokea wakati ambapo Yona hakumtii Bwana? (ona Yona 1:4–17).

    • Yona alifanya nini ili kutubu? (ona Yona 1:10–12; 2:1–4, 9; 3:1–4).

    • Nini kilitokea wakati Yona alipotii? (ona Yona 3:35).

    2:30

    Jonah the Prophet

  • Watoto wako wangeweza kufurahia kusimulia tena hadithi ya Yona au kuiigiza. Shirikianeni baadhi ya uzoefu wakati Bwana alpotaka ufanye kitu ambacho kilikuwa kigumu kwako. Ni kwa jinsi gani Yeye alikusaidia kumtii Yeye?

Yona 1–4

Bwana ni mwenye rehema kwa wote wanaomgeukia Yeye.

  • Pengine watoto wako wangeweza kujifanya wanamhoji Yona kuhusu uzoefu wake. Ni maswali gani wangemwuliza? Wahimize wao kuuliza maswali ili kujua kitu ambacho Yona alijifunza kuhusu Bwana. Yona angeweza kusema nini, kwa mfano, kuhusu rehema ya Bwana? (ona, kwa mfano, Yona 2:7–10; 3:10; 4:2).

Yesu akimfikia mtu aliyeshushwa chini kupitia kwenye paa la nyumba

Kristo na Mtu mwenye Kupooza, na J. Kirk Richards

  • Wasaidie watoto wako wafikirie mifano wakati Mwokozi alipoonesha rehema kwa wengine, kama vile Marko 2:3–12; Luka 23:33–34; na Yohana 8:1–11. Wewe na watoto wako mngeweza kutafuta picha za mifano hii. Je! Ni fursa gani tunazo za kuwa na rehema kwa wengine?

Kwa ziada, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .

Yona akiwa ametupwa baharini kutoka kwenye merikebu, ambapo kivuli cha samaki mkubwa hakionekani kabisa

Yona na Nyangumi, na Kevin Carden

Ukurasa wa shughuli ya Watoto: Bwana atanisaidia kumtii Yeye, hata kama ni vigumu