Novemba 30–Desemba 6 ‘Yeye Hufurahia Rehema’: Mika; Nahumu; Habakuki; Sefania,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)
Novemba 30–Desemba 6 ‘Yeye Hufurahia Rehema,’” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026
Hapo Mwanzo Kulikuwako Neno, na Eva Timothy
Novemba 30–Desemba 6: “Yeye Hufurahia Rehema”
Mika; Nahumu; Habakuki; Sefania
Kusoma Agano la Kale mara nyingi kunamaanisha kusoma unabii juu ya uharibifu. Bwana kila mara aliwaita manabii ili wawaonye waovu kuhusu hukumu Zake. Huduma za Mika, Nahumu, Habakuki, na Sefania ni mifano mizuri. Kwa maelezo ya kutisha, manabii hawa walitabiri kuanguka kwa miji ambayo, wakati huo, ilionekana kuwa na nguvu na uwezo: Ninawi, Babeli, na Yerusalemu. Lakini hiyo ilikuwa maelfu ya miaka iliyopita. Kwa nini kuna thamani kusoma unabii huu leo?
Ingawa miji hiyo iliyokuwa na kiburi, miji iliyokuwa miovu iliharibiwa, uovu wa kiburi bado unaendelea kuwepo. Tunaweza hata kugundua chembe chembe zake mioyoni mwetu. Manabii wa Agano la Kale wanafunua jinsi tunavyoweza kuachana na maovu haya. Labda hiyo ni sababu moja bado tunasoma maneno yao leo. Hawakuwa tu manabii wa hukumu—walikuwa manabii wa ukombozi. Maelezo ya uharibifu yanapunguzwa makali na mialiko ya kuja kwa Kristo na kupokea msamaha Wake. Kama vile Mika alivyoliweka, Bwana hafurahii katika kutulaani, lakini “Yeye hufurahia katika rehema.” (Mika 7:18). Hii ilikuwa njia ya Bwana zamani, na ni njia yake leo. “Njia zake ni za milele” (Habakuki 3:6).
Kwa mihtasari ya vitabu hivi, ona “Mika,” “Nahumu,” “Habakuki,” na “Sefania” katika Kamusi ya Biblia.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Mika 6:1–8
“Je, Bwana anataka nini kutoka kwako?”
Mika anatualika tufikirie ingekuwaje “kuja mbele za Bwana, na kuinama … mbele za Mungu aliye juu” (Mika 6:6). Je, mstari wa 6–8 inapendekeza nini kwako kuhusu kile ambacho ni muhimu kwa Bwana anapotathmini maisha yako?
Ona pia Dale G.Renlund, “Fanya kwa Haki, Penda Rehema na Tembea kwa Unyenyekevu pamoja na Mungu,” Liahona, Nov. 2020, 109–12.
“Bwana ni mwema, ni ngome siku ya taabu” (Nahumu 1:7).
Nahumu 1
Bwana ni mwenye nguvu na mwenye huruma.
Ujumbe wa Nahumu ulikuwa kutabiri uharibifu wa Ninawi—mji mkuu wa milki yenye jeuri ya Ashuru, ambayo ilitawanya Israeli na kuitesa Yuda. Nahumu alianza kwa kuelezea ghadhabu ya Mungu na nguvu isiyo na kifani, lakini pia alisema juu ya huruma na wema wa Mungu. Tafuta mistari katika sura ya 1 ambayo inakusaidia kuelewa kila moja ya sifa hizi—na sifa zingine za Mungu unazozitambua. Kwa nini unahisi ni muhimu kujua kila mojawapo ya mambo haya kumhusu Bwana?
Habakuki
Ninaweza kuamini mapenzi ya Bwana na wakati Wake.
Hata manabii wakati mwingine wana maswali kuhusu njia za Bwana. Habakuki, ambaye aliishi wakati wa uovu ulioenea katika Yuda, alianza kumbukumbu yake kwa maswali kwa Bwana (ona Habakuki 1:1–4). Ni kwa jinsi gani ungeweza kufanya muhtasari wa maswali ya Habakuki? Je! maswali gani yanayofanana na haya watu wanauliza kuhusu Mungu leo? Je, umewahi kuwa na hisia sawa na hizo? Ungeweza pia kulinganisha maswali yao na mengine katika maandiko, kama yanavyopatikana katika Marko 4:37–38 na Mafundisho na Maagano 121:1–6.
Bwana alijibu maswali ya Habakuki kwa kusema kwamba Yeye angewatuma Wakaldayo (Wababeli) kuiadhibu Yuda (ona Habakuki 1:5–11). Lakini Habakuki bado alikuwa na wasiwasi, kwani ilionekana kuwa sio haki kwa Bwana kusimama karibu “wakati yule mwovu [Babeli] atamla mtu aliye mwenye haki zaidi [Yuda]” (ona mstari wa 12–17). Unapata nini katika Habakuki 2:1–4 ambacho kinakutia msukumo kumwamini Bwana wakati unapokuwa na maswali yasiyo na majibu? ( ona pia Marko 4:39–40; Mafundisho na Maagano 121:7–8; “God Will Lift Us Up” [video], Maktaba ya Injili).
God Will Lift Us Up
Sura ya 3 ni sala ya Habakuki ya sifa na imani. Ni kwa jinsi gani toni ya Habakuki katika sura ya 3 ni tofauti na sura ya 1? Hapa kuna wazo la kukusaidia kutafakari mstari wa 17–19: Tengeneza orodha ya baraka za kimwili na kiroho ambazo Mungu amekupa. Kisha fikiria kwamba umepoteza baraka za kimwili. Hiyo inaweza kukufanya ujisikie vipi kuhusu baraka zingine? Kwa nini ingeweza kuwa vigumu “kufurahia katika Bwana”(mstari wa 18) wakati wa magumu kama yale yaliyoelezwa katika mstari wa 17? Tafakari jinsi unavyoweza kukuza imani kubwa katika Mungu, hata wakati maisha yanaonekana kutokuwa sawa.
Ona pia Gerrit W. Gong, “Vitu VYote kwa Faida Yetu,” Liahona, Mei 2024, 41–44; “Angazia,” Nyimbo za Dini, no. 46; Mada na Maswali, “Kutafuta Majibu kwa Maswali,” Gospel Library.
Kuwa mvumilivu. Wakati mwingine tunataka majibu ya maswali yetu mara moja, lakini umaizi wa kiroho huchukua muda na hauwezi kulazimishwa. Kama Bwana alivyomwambia Habakuki, “ingojee; kwa kuwa haina budi kuja” (Habakuki 2:3).
Sefania
“Mtafuteni Bwana, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia.”
Unaposoma unabii wa Sefania, angalia aina ya mitazamo na tabia ambazo zilipelekea maangamizo—ona hasa Sefania 1:4–6, 12; 2:8, 10, 15; 3:1–4. Kisha tafuta sifa za watu ambao Mungu angewahifadhi—ona Sefania 2:1–3; 3:12–13, 18–19. Je, ni ujumbe gani unahisi Bwana alionao kwako katika mistari hii?
Sefania 3:14–20
Bwana atafurahia pamoja na watu Wake katika Sayuni.
Baada ya kusoma Sefania 3:14–20, ona ni njia ngapi unaweza kukamilisha sentensi hii: “Furahini na ufurahi kwa moyo wote … Kwa nini ni muhimu kwako kujua kuhusu sababu hizi za kufurahia? Ungeweza kulinganisha mstari hii na uzoefu ulioelezewa katika 3 Nefi 17 na utafakari jinsi Yesu Kristo anavyojiikia juu ya watu Wake—ikijumuisha wewe.
Kwa ziada, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Mika 5:2
Yesu Kristo alizaliwa Bethlehemu.
-
Watoto wako wanaweza wasijue kwamba ulikuwa unabii wa Mika ambao uliwasaidia Mamajusi kumpata mtoto Yesu huko Bethlehemu. Ukitumia Mika 5:2 na Mathayo 2:1–6, pengine watoto wako wangeweza kuigiza tena uzoefu wao. Kisha ungeweza kuzungumza kuhusu kwa nini kuzaliwa kwa Yesu kulikuwa muhimu sana kiasi kwamba manabii walijua kuhusu hilo miaka mingi kabla hajazaliwa.
Mtoto Mtakatifu Anazaliwa, na Dana Wood
Nahumu 1:7
“Bwana ni mwema, ni ngome siku ya taabu.”
-
Baada ya kusoma Nahumu 1:7, watoto wako wangeweza kujenga au kuchora “ngome imara” rahisi au ngome (kuna picha moja katika muhtasari huu). Ni zipi baadhi ya sababu za watu kuhitaji ngome? Ni nini kinachofanya siku yetu kuwa “siku ya taabu”? Je, ni kwa jinsi gani Yesu Kristo ni kama ngome kwetu?
Habakuki 2:3
Mungu daima atatimiza ahadi Zake.
-
Ili kutambulisha Habakuki 2:3, wewe na watoto wako mngeweza kuzungumza kuhusu vitu ambavyo ni vizuri lakini tu baada ya kusubiri—kama tunda ambalo linahitaji kuiva au kinyunya kinachohitaji kuokwa. Ni nini kitatokea ikiwa tutajaribu kula tunda au kinyunya kabla havijawa tayari? Kisha ungeweza kuzungumza kuhusu nabii Habakuki, ambaye alitaka kujua ni lini Bwana angesitisha uovu ulimwenguni. Soma jibu la Bwana katika Habakuki 2:3. Ungeweza kuwasaidia watoto wako wafikirie vitu ambavyo Mungu ameahidi. Kwa kila mfano, mngeweza kusema pamoja, ‘Ngoja; Kwani hakika hayo bila shaka yatakuja.
Habakuki 2:14
Ninaweza kuijaza dunia kwa maarifa juu ya Yesu Kristo.
-
Ili kuonyesha Habakuki 2:14, wewe na watoto wako mngeweza kujaza kopo au chombo kingine kwa picha au maneno yanayowakilisha mambo ambayo Yesu alifanya au kufundisha. Ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidia kuujaza ulimwengu na maarifa juu ya Bwana?
-
Ungeweza pia kuwaonyesha watoto wako ramani ya ulimwengu (ona Ramani za Historia ya Kanisa, na.7, “Ramani ya Ulimwengu”). Wasaidie wao wapate mahali ambapo wanaishi na mahali ambapo wamisionari wanaowafahamu wametumikia. Mngeweza kuimba wimbo kuhusu kushiriki injili, kama vile “We’ll Bring the World His Truth” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 172–73). Ni nini tunaweza kuwaambia wengine kuhusu Yesu Kristo?
Sefania 3:14–20
Yesu Kristo anafurahia pamoja na wale wanaomfuata Yeye.
-
Katika Sefania 3:14–20, watoto wako wangeweza kutafuta kitu ambacho kinawafanya watake “kuimba, … furahini na kushangilia kwa moyo wote.” Pengine mngeweza kuimba baadhi ya nyimbo za dini za shangwe au kuimba nyimbo pamoja na kuzungumza kuhusu shangwe mnayoipata katika injili ya Yesu Kristo.
Kwa ziada, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.