“Desemba 14–20. ‘Nimewapenda Ninyi, Asema Bwana’: Malaki,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)
“Desemba 14–20. ‘Nimewapenda Ninyi, Asema Bwana,’” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026
Desemba 14– 20: “Nimewapenda Ninyi, Asema Bwana”
Malaki
“Nimewapenda ninyi,” Bwana aliwaambia watu Wake kupitia nabii Malaki. Lakini Waisraeli, ambao walikuwa wameteseka kwa vizazi vingi vya mateso na utumwa, walimuuliza, “Umetupenda kwa njia gani?” (Malaki 1:2). Baada ya yote Israeli iliyopitia, huenda wakajiuliza ikiwa historia ya Israeli ya kale kweli ni hadithi ya upendo wa Mungu kwa watu Wake wa agano. Kwa njia fulani, ni rahisi kuiona kama hadithi ya udhaifu na uasi wa binadamu. Walakini kupitia yote hayo, Mungu hakuacha kamwe kuwafikia kwa upendo. Wakati wana wa Yakobo walipomtendea vibaya ndugu yao Yusufu, Bwana bado aliandaa njia ya kuwaokoa na baa la njaa (ona Mwanzo 45:4–6). Wakati Israeli walipolalamika jangwani, Yeye aliwalisha mana (ona Kutoka 16:1–4). Hata Israeli walipogeukia miungu wengine, na kutawanywa, Mungu aliwaahidi kwamba ikiwa watatubu, atawakusanya na kuwakomboa “kwa rehema nyingi” (ona Isaya 54:7). Kwa kweli, Agano la Kale ni hadithi ya subira ya Mungu, upendo wa kudumu. Na hadithi hii inaendelea leo. Yesu Kristo, “Jua la Haki,” kama Malaki alivyomwita, amekuja “na uponyaji katika mabawa yake” (Malaki 4:2). Yeye ndiye ushahidi mkuu wa upendo wa Mungu kwa Israeli ya kale na kwa ajili yetu sote.
Kwa habari zaidi kuhusu kitabu cha Malaki, (ona “Malaki” katika Kamusi ya Biblia.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Malaki 1–4.
“Nirudieni nami nitawarudia.”
Katika siku za Malaki, Waisraeli walikuwa tayari wamejenga upya hekalu huko Yerusalemu, lakini kama watu bado walihitaji kujenga tena uhusiano wao na Bwana. Unapojifunza Malaki, tafuta maswali ambayo Bwana aliwauliza Waisraeli au ambayo walimwuliza Yeye. Fikiria kujiuliza maswali kama hayo (mifano kadhaa imependekezwa hapa chini) kukusaidia kutathmini uhusiano wako na Bwana na kusogea karibu na Yeye.
-
Je, ni kwa jinsi gani nimeusikia upendo wa Bwana kwa ajili yangu? (ona Malaki 1:2).
-
Je! Matoleo yangu kwa Bwana ni kweli yanamheshimu Yeye? (ona Malaki 1:6–11).
-
Ni kwa njia gani ninahitaji “kurudi” kwa Bwana? (ona Malaki 3:7).
-
Je! mimi ninamwibia Mungu kwa njia yo yote ile? (ona Malaki 3:8–11).
-
Je! Mtazamo wangu wakati wa shida unadhihirisha hisia zangu kwa Bwana? (ona Malaki 3:13–15; ona pia 2:17).
Malaki 1:6–14.
Bwana anataka “dhabihu iliyo safi.”
Unaposoma kuhusu matoleo yaliyoelezewa katika Malaki 1, unagundua nini kuhusu dhabihu ambazo makuhani walikuwa wanatoa? Je! Dhabihu hizi zinapendekeza nini juu ya hisia za makuhani kwa Bwana? (ona Malaki 1:13). Fikiria kutengeneza orodha ya matoleo, au dhabihu, ambayo unafanya kwa Bwana. Kwa kila kitu kilicho kwenye orodha, wanaweza kujadili ni kitu gani ambacho kinaweza kuifanya matoleo kuwa “najisi” au matoleo kuwa “safi” (Malaki 1:7).
Malaki 3:8–12.
Bwana hufungua madirisha ya mbinguni ninapoonyesha imani yangu kwa kulipa zaka.
Fikiria una rafiki ambaye amegundua kwamba unalipa zaka. “Kwa nini unafanya hivyo?” rafiki yako anauliza. Fikiria kuhusu hili unaposoma Malaki 3:8–12. Je, unapata nini ambacho kingeweza kusaidia kujibu swali la rafiki yako? Ni kipi kingine ungetaka rafiki yako aelewe kuhusu zaka? Kwa msaada zaidi, ungeweza kutafuta ujumbe wa Mzee Neil L. Andersen “Zaka: Kufungua mAdirisha ya Mbinguni” (Liahona, Nov. 2023, 32–35), ukitafuta majibu ya maswali kama haya:
-
Je, ni kwa nini Bwana anataka sisi tuilipe zaka?
-
Nini kinaweza kumzuia mtu kulipa zaka, na ni kwa jinsi gani tunaweza kushinda vikwazo hivyo?
-
Ni kwa jinsi gani kulipa zaka kunaimarisha imani yetu kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?
Ungeweza pia kushiriki na rafiki yako jinsi Bwana alivyokubariki wakati unapolipa zaka. Unaweza kupata mawazo katika sehemu yenye kichwa cha habari “Somo Namba 1—Baraka Muhimu lakini Zenye Ugumu” katika ujumbe wa Mzee David A. Bednar “Madirisha ya Mbinguni” (Liahona, Nov. 2013, 17–18). Tunakuwa watu wa namna gani kwa kulipa zaka?
Unafikiri kirai “sitakufungua madirisha ya mbinguni” (mstari wa10) kinaweza kumaanisha nini? Pengine ungeweza kutazama nje ya dirisha na kufikiria kuhusu madhumuni ya madirisha. Kwa nini “madirisha ya mbinguni” ni njia nzuri ya kuelezea jinsi Bwana anavyotubariki tunapolipa zaka?
Ono ndani ya Hekalu la Kirtland, na Gary Smith
Malaki 4:5–6.
“Nitawapelekea Eliya nabii.”
Wakati Moroni aliponukuu Malaki 4:5–6 kwa Joseph Smith, alifanya hivyo “kwa tofauti kidogo na jinsi inavyosomwa” katika Biblia (ona Joseph Smith—Historia 1:36). Tofauti ya Moroni inaongeza nini kwa uelewa wako juu ya unabii huu? Hasa, tafakari maswali kama haya:
-
Hawa akina baba ni nani? (ona Kumbukumbu la Torati 29:13). Ni ahadi gani zimetolewa kwao? (ona Ibrahimu 2:9–11). Ni kwa jinsi gani unasaidia kutimiza ahadi hizi?
-
Ni uzoefu upi umekusaidia ugeuze moyo wako uwaelekee mababu zako? Kwa nini hilo ni muhimu sana kwenye mpango wa Mungu?
Ili kujifunza zaidi kuhusu ujio wa Eliya na jinsi unabii huu unavyotimizwa leo, ona Mafundisho na Maagano 110:13–16 na D. Todd Christofferson, “Nguvu ya Kuunganisha” (Liahona, Nov. 2023, 19–22). Kwa nini una shukrani kwamba Eliya amekuja?
Ona pia Gerrit W. Gong, “Kila Mmoja Wetu Ana Hadithi,” Liahona, Mei 2022, 43–46; “Turn Your Hearts,” Nyimbo za Dini, na. 291; “The Sealing Power” (video), ChurchofJesusChrist.org.
The Sealing Power
Kwa ziada, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Malaki 1:2
Bwana ananipenda mimi.
-
Ni kwa jinsi gani wewe na watoto wako mngejibu swali linalopatikana katika Malaki 1:2—”[Bwana] Umetupendaje? Shirikianeni sababu zingine mnazojua kuwa Yeye anawapenda. Pengine watoto wako wangeweza kuchora picha ambazo zinawakumbusha juu ya upendo Wake.
Wahusishe watoto katika mijadala ya injili. Kama unafundisha watoto wadogo, unaweza kuhitaji kufikiria njia za ubunifu ili kuwahusisha katika mijadala ya injili. Kwa mfano, watoto wako wangeweza kupitisha mpira kuzunguka; wanaposhikilia mpira, wangeweza kushiriki sababu moja wanajua Yesu anawapenda wao.
Malaki 3:8–12.
Bwana atanibariki ninapolipa zaka.
-
Ni kwa jinsi gani utawasaidia watoto wako wajifunze kuhusu zaka? Ungeweza kuwaomba kuhesabu vitu vidogo 10, kama vile sarafu kwenye ukurasa wa shughuli ya wiki hii. Kisha wangeweza kutenganisha mojawapo ya vitu kutoka kwa vingine—hivi ndivyo tunavyompa Bwana kama zaka. Kulingana na Malaki 3:8–12, kwa nini Bwana anatutaka sisi tulipe zaka? (ona pia “Malaki Nabii” katika Hadithi za Agano la Kale, 171–72; “First Things First!” [video], Maktaba ya Injili).
0:58Malachi the Prophet
1:18First Things First!
-
Mnaposoma Malaki 3:10 pamoja, ungeweza kuwaalika watoto wako wasimame karibu na dirisha wakati unaposoma kirai “madirisha ya mbinguni.” Au unaweza kumimina maji katika kikombe mpaka kifurike ili kuelezea kirai “hakutakuwa na nafasi ya kutosha ya kuzipokea.” Waambie watoto kuhusu baraka ambazo Mungu amekupatia unapolipa zaka. Watoto wako wangeweza kuchora picha zinazowakilisha baraka hizi na kuzitundika au karibu na dirisha nyumbani mwako.
Malaki 4:5–6
Eliya alikuja kugeuza mioyo yetu kuwaelekea familia zetu.
-
Katika Malaki 4:5–6, watoto wako wangeweza kutafuta majibu ya maswali yafuatayo kuhusu unabii wa Malaki: Ni nani Bwana aliahidi kumtuma? Ni lini Yeye alisema mtu huyu angekuja? Ni nini Bwana alisema mtu huyu angefanya? Kwa nini mtu huyu angehitajika kuja? Ni wapi unabii huu ulitimizwa? (ona Mafundisho na Maagano 110:13–16).
-
Ili kugundua jinsi ahadi katika Malaki 4:5 ilivyotimizwa, unaweza pia kurejelea “Joseph na Oliver Wanapokea Funguo za Ukuhani” katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 26–30. Wimbo kama “The Hearts of the Children” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 92) unaweza kuwasaidia watoto wako wajifunze kwa nini ilikuwa muhimu sana kwamba Eliya alikuja. Mngeweza pia kutembelea FamilySearch.org/discovery, aplikesheni ya Mti wa FamilySearch, au kijitabu cha Familia Yangu kwa ajili ya shughuli ambayo inaweza kuwasaidia watoto wako kugeuza mioyo yenu kwa wahenga wenu.
Kwa ziada, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .