Njoo, Unifuate
Desemba 21–27. “Ndiye Tuliyemngoja, Naye Atatuokoa”: Krismasi


Desemba 21–27. ‘Ndiye Tuliyemngoja, Naye Atatuokoa’: Krismasi,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)

Desemba 21–27. ‘Ndiye Tuliyemngoja, Naye Atatuokoa’” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026

mtoto Yesu amelala

Kwa Ajili Yetu Mtoto Amezaliwa, na Simon Dewey

Desemba 21–27: “Ndiye Tuliyemngoja, Naye Atatuokoa”

Krismasi

Agano la Kale hubeba roho ya matarajio ya hamu. Kwa njia hiyo, ni kidogo kama msimu wa Krismasi. Kuanzia Adamu na Hawa, mapatiaki wa Agano la Kale, manabii, washairi, na watu walitazamia siku nzuri, zilizojazwa na tumaini la kufanywa upya na ukombozi wa Masiya. Na Waisraeli mara kwa mara walihitaji tumaini hilo—iwe walikuwa utumwani Misri au Babeli au wafungwa kwa dhambi au uasi wao wenyewe. Katika hayo yote, manabii waliwakumbusha kwamba Masiya, Mkombozi, atakuja “kutangaza uhuru kwa wafungwa” (Isaya 61:1).

Tumaini hilo lilianza kutimizwa wakati Yesu Kristo alipozaliwa huko Bethlehemu. Mkombozi mkuu wa Israeli alizaliwa katika zizi na kulazwa katika hori la ng’ombe (ona Luka 2:7). Lakini Yeye hakuwa Mkombozi tu wa Waisraeli wa kale. Yeye alikuja kukukomboa—kuchukua masikitiko yako, kujitwika huzuni zako, kuchubuliwa kwa maovu yako, ili kwamba kwa kupigwa Kwake upate kuponywa (ona Isaya 53:4–5). Hii ndio sababu Krismasi imejaa matarajio ya furaha hata leo. Masiya alikuja zaidi ya miaka 2,000 iliyopita, na Yeye anaendelea kuja maishani mwetu kila tunapomtafuta.

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

ikoni ya seminari
Ninafurahi katika Mkombozi wangu.

Krismasi inajulikana kama majira ya shangwe kwa sababu ya shangwe ambayo Yesu Kristo anaileta ulimwenguni. Karne kabla ya Mwokozi kuzaliwa, manabii wa Agano la Kale pia walihisi furaha walipokuwa wakisema juu ya Masiya anayekuja. Soma baadhi ya vifungu vifuatavyo, na ufikirie kwa nini vingekuwa vya thamani kwa watu ambao walitarajia misheni ya Mwokozi: Zaburi 35:9; Isaya 25:8–9; 44:21–24; 51:11; Sefania 3:14–20; Musa 5:5–11. Kwa nini vifungu hivi ni vya thamani kwako? Ni sababu zipi vifungu hivi vya maandiko vinatoa ili kuwa na shangwe?

Ona pia Dallin H. Oaks, “Good Tidings of Great Joy” (First Presidency Christmas devotional, Dec. 4, 2022), Gospel Library; “JShangwe Kote,” Nyimbo za Dini, no 113.

nyota angavu katika anga la usiku

Ishara zinaweza kunisaidia kumkumbuka Yesu Kristo.

Mila nyingi zinazohusiana na Krismasi zinaweza kuwa na maana ya ishara ambayo inatuelekeza kwa Kristo. Unapojifunza Agano la Kale mwaka huu, unaweza kuwa umeona ishara nyingi za Mwokozi. Chache zimeorodheshwa hapo chini: Fikiria kujifunza hizi na kuandika kile zinachokufundisha kumhusu Yeye.

  • Nyota (Hesabu 24:17; Mathayo 2:2; Ufunuo 22:16).

  • Mchungaji (Zaburi 23; Luka 15:4–7; Yohana 10:11)

  • Mwana kondoo (Mwanzo 22:8; Kutoka 12:5; 1 Petro 1:18–20).

  • Maji (Kutoka 17:1–6; Yeremia 2:13; Ezekieli 47:1–12; Yohana 4:7–14).

  • Mwamba (1 Samweli 2:2; 2 Samweli 22:2–3; Zaburi 118:22–23; Isaya 28:16; Waefeso 2:20).

  • Tawi (Isaya 11:1–2; Yeremia 23:5; 33:15).

  • Nuru (Zaburi 27:1; Isaya 9:2; 60:19; Mika 7:8; Yohana 8:12).

Je, ni ishara gani zingine, vifungu, na maelezo umeyapata katika maandiko ambayo yanayoshuhudia juu ya Yesu Kristo?

Ona pia 2 Nefi 11:4; Mosia 3:14–15; Musa 6:63; “Aina au Ishara za Kristo” na “Yesu Kristo,” kote katika Mwongozo wa Maandiko (Maktaba ya Injili).

“Jina Lake litaitwa Ajabu.”

Yesu Kristo anatajwa kwa majina na vyeo vingi tofauti. Tafuta vyeo katika mstari ifuatayo: Zaburi 23:1; 83:18; Isaya 7:14; 9:6; 12:2; 63:16; Amosi 4:13; Zekaria 14:16; Musa 7:53. Je, ni vyeo gani vingine unavyoweza kuvifikiria? Ungeweza kufurahia kuorodhesha vyeo vya Yesu Kristo ambavyo umevipata katika nyimbo za Krismasi. Je, kila jina linashawishi vipi katika njia unayofikiria kumhusuYake?

Fikiria kuchagua jina au jukumu la Mwokozi ambalo litakusaidia kumkumbuka Yeye mwaka ujao.

Ona pia Quentin L. Cook, “Amani Binafsi katika Nyakati zenye Changamoto,” Liahona, Nov. 2021, 89–92; “Malaika Waimba,” Nyimbo za Dini, no. 120.

Kwa ziada, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana..

ikoni ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Agano la Kale hunifundisha kuhusu Yesu.

  • Wewe na watoto wako mnaweza kuwa na baadhi ya mapambo ya Krismasi unayoweza kutumia kuanza mazungumzo kuhusu Yesu Kristo. Pengine ungeweza kuzungumza kuhusu jinsi nyota ya Krismasi, taa, au zawadi inavyotukumbusha juu ya Mwokozi. Kisha ungeweza kutafuta moja au zaidi ya maandiko yafuatayo kwa ajili ya kitu ambacho kinaweza kuashiria Yesu Kristo: Mwanzo 22:8; Hesabu 24:17; Zaburi 23:1; 27:1. Pengine watoto wako wangeweza kunyanyua juu picha au mapambo ambayo yanaendana na kila mstari wanapoisoma. Ni jinsi gani Yesu ni kama mwana kondoo, maji, mwamba, mchungaji au nuru? Fikiria kuimba wimbo wa Krismasi pamoja, kama vile “Stars Were Gleaming” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 37).

  • Watoto wako wangeweza pia kutazama picha mwishoni mwa muhtasari huu unapowasomea Isaya 9:6. Waombe watoto wako wamwonyeshe mtoto Yesu wakati wanaposikia kirai “mtoto amezaliwa.” Shiriki ushuhuda wako kwamba manabii katika Agano la Kale walijua kwamba Yesu angezaliwa.

  • Unapojiandaa kusoma maisha ya Yesu Kristo katika Agano Jipya mwaka ujao, fikiria kupitia pamoja na watoto wako yale waliyojifunza kumhusu Yeye mwaka huu katika Agano la Kale. Unaweza kukagua muhtasari wa nyenzo hii na maelezo yoyote ya kibinafsi ya kukusaidia kukumbuka kile ulichojifunza. Watoto wadogo wanaweza kufaidika kwa kutazama Hadithi za Agano la Kale au picha katika Njoo, Unifuate. Je! Ni unabii gani au hadithi gani zimejitokeza bayana? Je, tumejifunza nini kuhusu Mwokozi?

Mila ya Krismasi inaweza kumwonyesha Yesu Kristo.

  • Familia za Waisraeli zilikuwa na mila, kama Pasaka na karamu zingine, ambazo zilikusudiwa kuelekeza mioyo na akili zao kwa Bwana (ona Kutoka 12). Je! ni mila gani wewe na watoto wako mlizonazo wakati wa Krismasi ambazo zinawasaidia kufokasi kwa Yesu Kristo? Je, ni mila gani unazoijua kutoka katika historia ya familia yako? Unaweza kufikiria kujadili na watoto wako baadhi ya mila unazotaka kuanza. Baadhi ya mawazo yanangeweza kujumuisha kumtumikia mtu aliye na uhitaji, kuchagua kitu fulani ninyi mnaweza kutoka kama “zawadi” kwa Mwokozi, kumwaalika rafiki kutazama ibada ya Krismasi ya Urais wa Kwanza pamoja na wewe (broadcast.ChurchofJesusChrist.org), kuandika wimbo wako mwenyewe wa Krismasi, au kutafuta njia ya ubunifu ya kushiriki ujumbe wa kuzaliwa kwa Kristo.

Nyumbani, kujifunza na kuishi haviwezi kutenganishwa. “Injili inachukua uhusiano wa haraka nyumbani. Hapo watu ambao unajifunza injili pamoja nao ni watu utakaoishi nao injili hiyo—kila siku. Ukweli, muda mwingi, kuishi injili ni jinsi gani sisi tunajifunza injili. Kwa hivyo unapojifunza na kufundisha injili nyumbani, angalia njia unazoweza kuunganisha kile unachojifunza na kile unachofanya. Nyumbani mwako, acha injili iwe kitu unachojitahidi kukiishi, siyo tu kitu unachokizungumzia” (Kufundisha Katika Njia ya Mwokozi31).

mandhari ya kuzaliwa kwa Yesu

Kielelezo cha Kuzaliwa kwa Yesu, na Ethan Brown

Baba wa Mbinguni alinipa zawadi ya Mwanawe ya kuwa Mwokozi wangu.

  • Ni kwa jinsi gani ninaweza kuwasaidia watoto wangu kuhisi staha na shangwe ya kuzaliwa kwa Kristo? Mngeweza kutazama video ya “The Christ Child: A Nativity Story” (Maktaba ya Injili) au kusoma pamoja Mathayo 1:18–25; 2:1–12; Luka 1:26–38; 2:1–20. Kila mtoto anaweza kuchagua mtu kutoka kwenye video au maandiko na kushiriki jinsi mtu huyo alivyohisi kuhusu Mwokozi. Kisha mngeweza kushiriki hisia zenu wenyewe kumhusu Yeye.

    17:57

    The Christ Child

  • Pengine wewe na watoto wako mngeweza kuzungumza kuhusu zawadi ambazo umetoa au kupokea kwa miaka mingi ambazo zimeleta shangwe. Kisha mngeweza kusoma Isaya 25:9 pamoja na kuzungumza kuhusu kwa nini mnafurahia kwamba Baba wa Mbinguni alimtuma Mwokozi. Ili kuwasaidia watoto wako waelewe vyema zaidi jukumu la Yesu Kristo kama Mwokozi wetu, waalike wasome Isaya 25:8–9; 53:3–5; na Hosea 13:14. Je, maandiko haya yanatufundisha nini kuhusu jinsi Bwana anavyotuokoa?

  • Mngeweza pia kuimba wimbo wa Krismasi pamoja, kama vile “Away in a Manger” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 42–43) or “Mji Mwema, Bethlehemu” (Nyimbo za Dini, no. 119). Wasaidie watoto wako watafute virai katika wimbo ambavyo vinawasaidia kujua kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanawapenda.

Kwa ziada, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.

mandhari ya kuzaliwa kwa Yesu

Kuzaliwa kwa Yesu, na N. C. Wyeth

Ukurasa wa shughuli ya Watoto: Agano la Kale linanifundisha kuhusu Yesu