“Oktoba 26–November 1. ‘Nitageuza Masikitiko Yao Kuwa Furaha’: Yeremia 31–33; 36–39; Maombolezo 1; 3” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)
“Oktoba 26–Novemba 1. ‘Nitageuza Masikitiko Yao Kuwa Furaha,’” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026
Yeremia Akiomboleza juu ya Maangamizo ya Yerusalemu, na Rembrandt van Rijn
Oktoba 26–Novemba 1: “Nitageuza Masikitiko Yao kuwa Furaha”
Yeremia 31–33; 36–39; Maombolezo 1;3
Wakati Bwana alipomwita Yeremia kwanza kuwa nabii, Alimwambia kwamba kazi yake itakuwa “kung’oa, na kubomoa” (Yeremia 1:10)—na katika Yerusalemu, kulikuwa na uovu mwingi wa kung’oa na kubomoa. Lakini hii ilikuwa ni sehemu tu ya utume wa Yeremia—aliitwa pia “kujenga, na kupanda” (Yeremia 1:10). Ni nini kingeweza kujengwa au kupandwa katika magofu ya ukiwa yaliyoachwa kwa sababu ya uasi wa watu wa agano? Ikiulizwa kwa njia nyingine, wakati dhambi au shida zimeacha maisha yetu kuwa magofu, ni kwa jinsi gani tunaweza kujenga na kupanda tena? Jibu liko katika “Tawi la haki” (Yeremia 33:15), Masiya aliyeahidiwa. Yeye huleta “agano jipya” (Yeremia 31:31)—hilo ambalo linahitaji zaidi ya sura ya nje ya kujitolea. Sheria yake lazima iwe “katika sehemu [zetu] za ndani,” ikiandikwa “mioyoni [mwetu].” Hivyo ndivyo inavyomaanisha kwa Bwana “kuwa Mungu [wetu]” na sisi “kuwa watu [Wake]” (Yeremia 31:33). Ni mchakato wa maisha yote, na bado tutafanya makosa na yanasababisha kuomboleza mara kwa mara. Lakini tunapofanya hivyo, Bwana anaahidi, “Nitageuza masikitiko yao kuwa furaha” (Yeremia 31:13).
Kwa ajili ya muhtasari wa Maombolezo, ona “Maombolezo, Kitabu cha” katika Mwongozo kwenye Maandiko.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Yeremia 31; 33
Bwana atawatoa watu Wake wa agano kutoka utumwani.
Katika Yeremia 31; 33 Bwana alikubali “maombolezo, na kulia kwa uchungu” (Yeremia 31:15) kwamba Waisraeli wangepata uzoefu wakati wanaenda utumwani. Hata hivyo, Naye alitoa maneno ya faraja na tumaini. Yatafute unaposoma sura hizi. Ni ahadi gani unapata ambazo zinatumika kwako?
Yeremia 31:31–34; 32:37–42
“Nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.”
Ingawa Waisraeli walikuwa wamevunja agano lao na Bwana, Yeremia alitabiri kwamba Bwana angeanzisha tena “agano jipya” na “agano la milele” na watu Wake (Yeremia 31:33; 32:40). Agano hilo ni nini? Fikiria kutafuta utambuzi katika Mwongozo wa Maandiko, “Agano Jipya na Lisilo na Mwisho,” Gospel Library.
Unaposoma Yeremia 31:31–34; 32:37–42, tafakari:
-
Inamaanisha nini kwako kuwa sehemu ya watu wa agano wa Mungu.
-
Inamaanisha nini kuwa na sheria Yake imeandikwa katika moyo wako.
-
Bwana anaahidi nini unapofanya maagano na Yeye.
-
Jinsi gani uhusiano wako wa agano na Bwana unavyokubadilisha wewe.
Ni ahadi zipi wewe umezifanya kwa Mungu uliposhiriki katika ibada takatifu? Je, Ni kwa jinsi gani Yeye anatimiza ahadi Zake kwako?
Ona pia David A. Bednar, “Kaa Ndani Yangu, Namii Ndani Yako; Kwa hiyo Tembea Pamoja Nami,” Liahona, Mei 2023, 123–26.
Yeremia 36
Maandiko yana nguvu ya kunigeuza kutoka kwenye uovu.
Kulingana na Yeremia 36:2–3, kwa nini Bwana alimwamuru Yeremia kuandika unabii wake? Unaposoma Yeremia 36, fikiria jinsi watu wafuatao walivyojisikiai kuhusu unabii huu:
-
Bwana (ona mstari wa 1–3, 27–31)
-
Yeremia (ona mistari 4–7, 32)
-
Baruki (ona mstari wa 4, 8–10, 14–18)
-
Yehudi na Mfalme Yehoyakimu (ona mstari wa 20–26)
-
Elnathani, Delaya, na Gemaria (ona mstari wa 25)
Tafakari jinsi unavyojisikia kuhusu maandiko haya. Ni kwa jinsi gani yamekusaidia kugeuka kutoka kwenye uovu?
Yeremia 37–39
Kuwa imara katika kuwafuata manabii wa Mungu.
Katika Yeremia 37:1–3, 15–21; 38:1–6, 14–28, ni ushahidi gani unaouona kwamba Mfalme Zedekia alimwamini Yeremia kuwa alikuwa nabii wa kweli wa Bwana? Ni ushahidi gani unaouona kwamba Zedekia hakuamini? Je, unajifunza nini kutokana na ulinganisho huu? Unaposoma Yeremia 39, tafakari tofauti ambayo ingeweza kufanyika kama Zedekia na watu wake wangemfuata nabii na kutii amri za Bwana. (Linganisha kile kilichotokea kwa Zedekia na kile kilichotokea kwa familia ya Lehi katika 1 Nefi 1–2.)
Yeremia 38:6–13; 39:15–18
Ninaweza kuwa jasiri katika kusimamia kile kilicho sahihi.
Maafisa wa mfalme walihisi kwamba unabii wa Yeremia ulikuwa unafanya askari wao wasiwe radhi kupigana, hivyo wakamtupa Yeremia katika gereza chafu la chini ya ardhi (ona Yeremia 38:1–4). Katika Yeremia 38:6–13, ni nini kinachokuvutia kuhusu majibu ya Ebedi-meleki Muethiopia? Tazama pia baraka ambazo Bwana alimpa Ebedi-meleki katika Yeremia 39:15–18.
Ni kwa jinsi gani wewe ungeweza kufuata mfano wa Ebedi-meleki?
Kilio cha Yeremia
Maombolezo 1; 3
Bwana anaweza kuniondolea huzuni ninayoipata kwa sababu ya dhambi.
Kitabu cha Maombolezo ni mkusanyiko wa mashairi yaliyoandikwa baada ya kuharibiwa kwa Yerusalemu na hekalu lake. Kwa nini unafikiri ni muhimu zilihifadhiwa? Fikiria ni isitiari gani katika Maombolezo 1 na 3 zinakusaidia wewe kuelewa kuhusu huzuni hiyo kubwa Israeli waliiyosikia. Ni jumbe gani za matumaini katika Kristo ambazo unazipata? (ona hususani Maombolezo 3:20–33; ona pia Mathayo 5:4; Yakobo 4:8–10; Alma 36:17–20).
Rais M. Russell Ballard alitaja baadhi ya hali ambazo zinaweza kusababisha wengine wapoteze matumaini, na akatoa ushauri kuhusu mahali pa kupata matumaini.
“Baadhi yetu tunaweza kuona maisha yetu yamejaa kukata tamaa, masikitiko, na huzuni. Wengi wanahisi kukosa matumaini kukabiliana na vurugu ambayo inaonekana kukithiri ulimwenguni. Wengine wanafadhaika juu ya wanafamilia ambao wamesombwa katika mkondo mkali, uliotanda wa kudhoofika kwa maadili na kushuka kwa viwango vya maadili. … Wengi hata wamejiuzulu wenyewe na kukubali uovu na ukatili wa ulimwengu kama usioweza kurekebishika. Wamekosa matumaini. …
“… Wengine miongoni mwetu yawezekana wamepoteza matumaini yote kwa sababu ya dhambi na uvunjaji wa sheria. Mtu anaweza kuwa amejizamisha kwa kina sana katika njia za ulimwengu kiasi kwamba yeye haoni njia ya kutokea na kupoteza matumaini yote. Maombi yangu kwa wote ambao wametumbukia katika huu mtego wa adui ni kamwe wasikate tamaa! Bila kujali jinsi mambo yanavyokatisha tamaa au jinsi yanavyoelekea kuwa mabaya, tafadhali niamini, unaweza daima kuwa na matumaini. Daima” (“Shangwe ya Tumaini Inatimizwa,” Ensign, Nov. 1992, 31–32).
Ona pia “Come, Ye Disconsolate,” Nyimbo za Dini, na. 115.
Wasaidie wengine wawajibike kwa kujifunza kwao wenyewe. Wakati mwingine inaonekana kama njia rahisi ya kufundisha ni kuwaambia tu wanafunzi kile tunachofikiria kuwa wanapaswa kujua. Hata hivyo, njia rahisi zaidi sio daima ndio njia bora. Mzee David A. Bednar alifundisha: “Kusudio letu halipaswi kuwa ‘Je, niwaambie nini?’ Badala yake, swali la kujiuliza wenyewe ni ‘Ni kipi ninaweza kuwaalika wafanye? Ni maswali gani yenye mwongozo wa kiungu ninayoweza kuuliza ambayo, kama wako tayari kujibu, yataanza kumwalika Roho Mtakatifu katika maisha yao?’” (evening with a General Authority, Feb. 7, 2020, Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25). Kuna njia nyingi za kuwasaidia wanafunzi kuchukua jukumu la kujifunza kwao. Kwa mfano, katika muhtasari huu wanafunzi wanaalikwa kutafuta, kutafakari, kutengeneza orodha, kuangalia picha, kushiriki katika masomo ya vitendo, kuchora, na kushiriki na kutumia kile wanachojifunza.
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Yeremia 31:3
Baba wa Mbinguni na Yesu wananipenda “kwa upendo usio na mwisho.”
-
Unaposoma Yeremia 31:3 pamoja na watoto wako, wangeweza kukusaidia kupata vitu (au picha za vitu) ambavyo vinadumu kwa muda mrefu, kama vile sarafu ya chuma, na baadhi ambavyo havidumu, kama vile kipande cha tunda. Mnaweza kuzungumza kuhusu maana ya “milele” na kushiriki na kila mmoja jinsi mlivyohisi “upendo wa milele” wa Baba wa Mbinguni. Mngeweza pia kuimba wimbo kama “God Is Watching Over All” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 229).
Yeremia 31:31–34; 32:38–41
Mungu atanisaidia niyashike maagano yangu.
-
Watoto wako wangeweza kufurahia kuchora moyo kwenye kipande cha karatasi na kisha kuandika katika moyo vitu wanavyojifunza kutoka Yeremia 31:31–34 kuhusu kufanya maagano na Mungu. Unaweza kutaka kurejelea agano wanalofanya wakati wa ubatizo ( ona Mosia 18:10, 13) na kujadili inamaanisha nini kuwa na ahadi hizi kuandikwa katika mioyo yao.
Yeremia 36:1–4
Maandiko ni neno la Mungu.
-
Ukurasa wa shughuli ya wiki hii ungeweza kuwasaidia watoto wako wajifunze kuhusu Yeremia, Baruki, na mfalme (ona Yeremia 36). Wangeweza pia kufanya vitendo vinavyoendana na maneno katika Yeremia 36:4–10, kama vile kuandika katika kitabu (ona mstari wa 4) na kusoma maandiko kwa watu (ona mistari wa 8, 10).
-
Wewe na watoto wako mngeweza kutazama kitabu cha watoto na nakala ya maandiko na kuzungumza kuhusu jinsi vitabu hivi ni tofauti. Je, ni kitu gani kinafanya maandiko kuwa maalumu? Inaweza kuwa ya kuvutia kushiriki na kila mmoja baadhi ya vifungu vya maandiko ambavyo ni maalumu kwako.
Yeremia 38:6–13
Ninaweza kusimamia kile ninachojua kuwa ni sahihi.
-
Ungeweza kutumia picha mwishoni mwa muhtasari kuwasaidia watoto wako wapate taswira ya hadithi ya Ebedi-meleki katika Yeremia 38:6–13. Pengine ungeweza kuwasaidia watafute mstari ambapo Ebed-meleki alifanya jambo jasiri kumsaidia nabii wa Bwana. Tunaweza kufanya nini kuonyesha kwamba tunajua nabii wetu leo ameitwa na Mungu?
Maombolezo 1:1– 2, 16; 3:22–26
Mwokozi alifanya iwezekane kwangu mimi kusamehewa dhambi zangu.
-
Ili kutambulisha Maombolezo, unaweza kuelezea watoto wako kwamba kwa sababu Waisraeli hawakutubu, Yerusalemu na hekalu viliharibiwa. Mngeweza kushiriki na kila mmoja jinsi ambavyo mngehisi kama mngekuwa mnaishi huko wakati huo (ona Maombolezo 1:1–2, 16). Je, ni kwa jinsi gani ujumbe katika Maombolezo 3:22–26 umekupa wewe matumaini?
-
Mngeweza pia kuambiana kuhusu nyakati ambapo mlisikia huzuni kuhusu uchaguzi mbaya mliofanya. Tunapata nini katika Maombolezo 3:22–26 ambacho kinatusaidia kuelewa msamaha ambao Yesu Kristo anatoa?
Kwa ziada, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.