Njoo, Unifuate
Oktoba 19–25. “Kabla Sijakuumba katika Tumbo Nalikujua”: Yeremia 1–3; 7; 16–18; 20


“Oktoba 19–25. ‘Kabla Sijakuumba katika Tumbo Nalikujua’: Yeremia 1–3; 7; 16–18; 20,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)

“Oktoba 19–25. ‘Kabla Sijakuumba katika Tumbo Nalikujua’” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026

Yeremia akimtazama mtu mwingine

Yeremia, na Walter Rane

Oktoba 19–25: “Kabla Sijakuumba katika Tumbo Nalikujua”

Yeremia 1–3; 7; 16–1820

Mwanzoni, Yeremia hakufikiria iwapo angekuwa nabii mzuri. “Tazama, siwezi kusema,” alipinga (Yeremia 1:6). Lakini Bwana alimhakikishia, “Nimetia maneno yangu kinywani mwako” (mstari wa 9), Yeremia alihisi kuwa yeye ni “mtoto” asiye na uzoefu (mstari wa 6), lakini Bwana alielezea kwamba alikuwa amejiandaa zaidi kuliko alivyofikiria—alikuwa ametawazwa kwa wito huu hata kabla ya kuzaliwa (ona mstari wa 5). Hivyo Yeremia akaweka kando woga wake na akakubali wito. Aliwaonya wafalme na makuhani wa Yerusalemu kwamba utakatifu wao wa kujifanya hautawaokoa. “Mtoto” ambaye alidhani kuwa hawezi kusema alikuja kuhisi neno la Mungu “moyoni [mwake] kama moto uwakao” na hakuweza kunyamaza (Yeremia 20:9).

Hadithi ya Yeremia ni hadithi yako pia. Mungu alikujua wewe, pia, kabla ya kuzaliwa na kukuandaa kwa ajili ya misheni yako katika maisha. Miongoni mwa mambo mengine, misheni hiyo ni pamoja na jambo ambalo Yeremia aliliona mapema: kukusanya watu wa Mungu, mmoja mmoja, “kuwaleta Sayuni” (Yeremia 3:14). Na hata kama hatujui nini cha kufanya au kusema, hatupaswi “kuogopa … , kwa kuwa mimi ni pamoja nawe, asema Bwana” (Yeremia 1:8, 19).

Kwa ajili ya muhtasari wa kitabu cha Yeremia, ona “Yeremia” katika Kamusi ya Biblia.

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Yeremia 1:4–19; 7:1–7; 20:8–9

Manabii huitwa kunena neno la Mungu.

Fikiria unazungumza na rafiki ambaye hajawahi kusikia juu ya manabii, na unaamua kuelezea dhana kwa kutumia wito wa Yeremia kuwa nabii katika Yeremia 1:4–19. Unapata nini katika mistari hii ambacho kinafundisha kitu fulani kuhusu manabii wa Mungu? Ungeweza pia kuangalia katika Yeremia 7:1–7; 20:8–9 na wimbo wa dini kama “Sauti ya Nabii” (Nyimbo za Dini, na. 13).

Unaweza pia kutaka kumfundisha rafiki yako kuhusu nabii aliye hai wa leo. Je, kuna chochote katika mistari hii ambacho kingeweza kusaidia? Manabii katika siku yetu “wanang’oa” au “wanabomoa” nini? Ni nini “wanajenga” na “kupanda”? (Yeremia 1:10). Ni kwa jinsi gani umekuja kujua kwamba nabii wetu aliye hai ameitwa na Mungu?

Ona pia Makala ya Imani 1:6, 9; “Why Do We Have Prophets?” (video), ChurchofJesusChrist.org.

1:37

Why Do We Have Prophets?

Yeremia 1:5

ikoni ya seminari
Mungu alinijua kabla sijazaliwa.

Yeremia alijifunza nini kuhusu yeye mwenyewe katika Yeremia 1:5? Kama nabii mpya aliyeitwa, kwa nini habari hiyo ingekuwa muhimu kwake kujua?

Mengi ya kile Yeremia alijifunza kuhusu yeye mwenyewe katika Yeremia 1:5 pia ni kweli juu yako. Mungu pia alikujua kabla hujazaliwa na kukuandaa kwa majukumu mahususi. Ili kujifunza zaidi kuhusu maisha yako kabla ya kuzaliwa, soma Alma 13:1–4; Mafundisho na Maagano 138:53–56; na Ibrahimu 3:22–23. Ungeweza kutengeneza orodha ya kweli unazogundua. Kwa nini habari hizi ni muhimu kwako kujua?

Ili kujifunza kuhusu jinsi kweli hizi zilivyogusa maisha ya Mzee Ahmad S. Corbitt, jifunze ujumbe wake “Unaweza Kukusanya Israeli!” (Liahona, Mei 2021, 63–63). Ni kwa jinsi gani kujua kuhusu maisha ya awali kunaleta matokeo ya jinsi tunavyoishi maisha ya duniani?

Hiki ndicho Rais Russell M. Nelson alichosema kuhusu maisha yako kabla ya kuja duniani:

“Baba yako wa Mbinguni amekujua wewe kwa muda mrefu sana. Wewe, kama mwana au binti Yake, ulichaguliwa na Yeye kuja duniani katika wakati mahususi, kuwa kiongozi katika kazi Yake kuu duniani. Wewe ulichaguliwa sio kwa ajili ya sifa zako za kimwili bali kwa sifa zako za kiroho kama vile ushupavu, ujasiri, uaminifu wa moyo, kiu ya ukweli, njaa ya hekima, na shauku ya kuwahudumia wengine.

“Ulikuza baadhi ya sifa hizi kabla ya kuzaliwa. Zingine unaweza kuzikuza hapa duniani kwa mwendelezo unapoendelea kuzitafuta” (“Maamuzi kwa Ajili ya Milele,” Liahona, Nov. 2013, 107).

Fikiria juu ya baadhi ya hali ambazo unaweza kukumbana nazo ambapo itakuwa muhimu kukumbuka kweli hizi kuhusu maisha yako kabla ya kuja duniani. Unaweza kufanya nini ili kujikumbusha juu ya kweli hizi?

Ona pia Russell M. Nelson, “Maamuzi ya Milele,” Liahona, Nov. 2013, 106–9; Mada na Maswali, “Kutawazwa,” “Kabla Ya Kuja Duniani,” Maktaba ya Injili.

kushoto, mtu amesimama katika tangi kubwa tupu; kulia, maporomoko ya maji

Katika Yeremia 2:13, Bwana alilinganisha hali ya kiroho ya watu na “matanki yaliyopasuka” na kujifananisha Yeye Mwenyewe na “chemchemi ya maji ya uzima.”

Yeremia 2; 7

“Wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima.”

Katika eneo kame ambalo Waisraeli waliishi, watu walihifadhi maji yenye thamani katika mabwawa ya chini ya ardhi yaliyoitwa matangi. Unafikiria “matangi yaliyopasuka” yaliyotajwa katika Yeremia 2:13 yanaweza kumaanisha nini? Kwa nini kupokea maji kutoka kwenye chemichemi itakuwa bora kuliko kutegemea matangi? Inamaanisha nini kuacha “chemchemi ya maji yaliyo hai”? Unaposoma Yeremia 2 na 7, gunda jinsi gani watu hawa walikuwa wakimwacha Bwana aliye maji ya uzima (ona, kwa mfano, Yeremia 2:26–28; 7:2–11). Kwa nini “maji ya uzima” ni ishara nzuri ya kile ambacho Mwokozi hutupatia? Fikiria kuhusu jinsi wewe unavyopokea maji ya uzima.

Yeremia 7 imeelekezwa kwa watu waliokuwa wakiingia “nyumba ya Bwana … kumwabudu Bwana,” lakini matendo yao hayakufanana na ibada zao za nje (ona mstari wa 2–11). Ni jumbe gani unahisi Bwana anaweza kuwa nazo kwa ajili yako katika mstari wa 21–23?

Tumia masomo ya vitendo. Manabii wa Bwana mara nyingi hulinganisha kweli za kiroho na vitu tunavyovijua. Fikiria kufanya vivyo hivyo unapojifunza na kufundisha injili. Kwa mfano, kupata taswira Yeremia 2:13, unaweza kuweka maji katika chombo kilicho na ufa au chombo kilichopasuka au kunywa kutoka kwenye chemichemi ya maji ya kunywa. Ni kwa jinsi gani Yesu ni kama “chemichemi ya maji ya uzima”? (Yeremia 2:13). Je, ni kwa jinsi gani tunakunywa kutoka Kwake maji ya uzima?

Yeremia 3:14–18; 16:14–21

Bwana atawakusanya watu Wake.

Katika Yeremia 16:14–15, Yeremia alilinganisha kukusanyika kwa Israeli katika siku za mwisho na Kutoka kwa Israeli kutoka Misri. Kwa maoni yako, kwa nini kukusanyika kungekuwa muhimu zaidi kwa watu wa Mungu kuliko Kutoka?

Ni nini Yeremia 3:14–18; 16:14–21 inapendekeza kuhusu jinsi mkusanyiko unavyotokea?

Katika ujumbe wake “Tumaini la Israeli,” Rais Russell M. Nelson, kama Yeremia, alifundisha kwamba kukusanyika kwa Israeli “ni jambo muhimu sana linalofanyika duniani leo” (ibada ya vijana ulimwenguni kote, Juni 3, 2018, Gospel Library). Soma au sikiliza ujumbe wake, na uone kama unaweza kugundua (a) jinsi Rais Nelson anavyofafanua mkusanyiko wa Israeli, (b) jinsi anavyoelezea umuhimu wake, na (c) jinsi unavyoweza kuwa sehemu ya kukusanyika huku.

Kwa ziada, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana..

ikoni ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Yeremia 1:5

Baba wa Mbinguni alinijua kabla sijazaliwa.

  • Ili kutambulisha ukweli muhimu uliofundishwa katika Yeremia 1:5, ungeweza kuwaonesha watoto wako picha ya mtoto mchanga (au, kama inawezekana, mngeweza kutazama picha za watoto wako walipokuwa watoto). Waulize watoto wako kama wanajua mahali walipoishi kabla ya kuzaliwa. Mngeweza pia kuimba pamoja wimbo ambao unafundisha kuhusu maisha kabla ya kuja duniani, kama vile “I Lived in Heaven” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 4).

  • Kama watoto wako wangependa kujifunza zaidi, ungeweza kuwasaidia kutafuta “Maisha Kabla ya Kuja Duniani” katika Mwongozo wa Maandiko. Wangeweza kutafuta majibu ya “nani,” “lini,” na “nini” maswali kuhusu maisha kabla ya kuja duniani.

msichana amembeba mtoto mchanga

Yeremia 1:4–19

Manabii wameitwa kunena maneno ya Bwana.

  • Fikiria kuonyesha picha za nabii au manabii walio hai kutoka kwenye maandiko (unaweza kupata baadhi katika majarida ya Kanisa, Kitabu cha Sanaa ya Injili, na Njoo, Unifuate). Waulize watoto wako ni nini wanachojua kuhusu manabii hawa.

  • Ili kufundisha kuhusu manabii wanafanya nini, ungeweza kuchagua baadhi ya mistari yenye msaada kutoka katika Yeremia 1, kama vile msatari wa 5, 7, 10, na 19. Watoto wako wangeweza kila mmoja kuchagua moja ya mistari, kuisoma, na kushiriki jambo wanalojifunza kuhusu manabii.

Yeremia 16:14–16

Ninaweza kuwasaidia watoto wa Baba wa Mbinguni kurudi Kwake.

  • Unaposoma Yeremia 16:16, watoto wako wangeweza kujifanya “kuvua samaki” au “kuwinda” vitu chumbani. Rais Russell M. Nelson amelinganisha wavuvi na wawindaji katika mstari huu na wamisionari (ona “Kukusanyika kwa Israeli Iliyotawanyika,” Liahona, Nov. 2006, 81). Wamisionari wanafanya kazi gani? Ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidia “kuvua samaki” na “kuwinda” Israeli iliyotawanyika? (ona “A Message for Children from President Russell M. Nelson” [video], ChurchofJesusChrist.org).

    3:30

    Video: A Message for Children from President Russell M. Nelson

Yeremia 18:1–6

Ninaweza kumruhusu Bwana aongoze maisha yangu, kama vile mfinyanzi anavyoumba udongo.

  • Ili kuchunguza mistari hii, unaweza kujadili au kuonyesha jinsi ufinyazi unavyoumbwa (ona picha mwishoni mwa muhtasari huu). Je, ni ujumbe gani Bwana anao kwa ajili ya Israeli katika Yeremia 18:1–6? Je, inamaanisha nini kuwa udongo mikononi mwa Bwana? (ona pia Isaya 64:8). Kwa hadithi nyingine ambayo inatulinganisha sisi na udongo wa mfinyanzi, ona ujumbe wa Mzee Richard J. Maynes “Shangwe ya Kuishi Maisha yanayolenga kwa Kristo” (Liahona, Nov. 2015, 27–30).

Kwa ziada, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .

mikono ikiunda umbo la ufinyazi kwenye gurudumu

“Angalieni, kama udongo ulivyo katika mkono wa mfinyanzi, ndivyo mlivyo ninyi katika mkono wangu, Ee nyumba ya Israeli” (Yeremia 18:6).

Ukurasa wa shughuli ya Watoto: Ninaweza kuwasaidia watoto wa Baba wa Mbinguni kurudi Kwake.