Njoo, Unifuate
Oktoba 5–11. “Ameyachukua Masikitiko Yetu, Amejitwika Huzuni Zetu”: Isaya 50–57


Oktoba 5–11 ‘Ameyachukua Masikitiko Yetu, na Amejitwika Huzuni Zetu’: Isaya 50–57,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)

Oktoba 5–11 ‘Ameyachukua Masikitiko Yetu na Amejitwika Huzuni Zetu’” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026

Yesu Kristo akiwa amevaa taji ya miiba

Kukejeliwa kwa Kristo, na Carl Heinrich Bloch

Oktoba 5–11: “Ameyachukua Masikitiko Yetu, Amejitwika Huzuni Zetu”

Isaya 50–57

Katika huduma yake yote, Isaya alizungumza juu ya mkombozi mwenye nguvu. Unabii huu ungekuwa hasa wa thamani sana kwa Waisraeli karne nyingi baadaye wakati wakiwa utumwani Babeli. Mtu ambaye angebomoa kuta za Babeli hakika angekuwa mshindi mwenye nguvu sana. Lakini huyo sio aina ya Masiya ambaye Isaya alimwelezea katika sura ya 52–53: “Alidharauliwa na kukataliwa na watu; mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao. … Tulimdhania kuwa amepigwa, amepigwa na Mungu, na kuteswa” (Isaya 53:3–4).

Kwa kumtuma mkombozi asiyetarajiwa kama huyo, Mungu alitufundisha juu ya ukombozi wa kweli. Ili kutuokoa kutokana na uonevu na mateso, Mungu alimtuma Yule ambaye Yeye mwenyewe alionewa na … kuteswa.” Ambapo wengine walimtarajia simba, Yeye almituma mwana-kondoo (ona Isaya 53:7). Hakika, njia za Mungu sio njia zetu (ona Isaya 55:8–9). Yesu Kristo anatuweka huru sio kwa kufungua gereza tu bali kwa kuchukua nafasi yetu huko. Yeye hutuondolea minyororo yetu ya masikitiko na huzuni kwa kuyabeba Yeye mwenyewe (ona Isaya 53:4–5, 12). Yeye hatuokoi akiwa mbali. Yeye anateseka pamoja nasi, kwa tendo la “fadhili za milele” ambazo “hazitaondolewa kwako” (Isaya 54:8, 10).

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Isaya 50–52

Wakati ujao ni angavu kwa wa watu wa Bwana.

Ingawa Waisraeli walikaa miaka mingi utumwani—na ingawa utumwa huo ulikuwa matokeo ya uchaguzi wao mbaya—Bwana aliwataka wautazamie wakati ujao kwa tumaini. Je, unapata nini katika ujumbe wa Isaya ambacho kinakupa tumaini? Chati kama hii ingeweza kukusaidia kujifunza:

Kile ninachojifunza kuhusu Mungu (ona, kwa mfano, Isaya 50:2, 5–9; 51:3–8, 15–16; 52:3, 9–10)

Jumbe za matumaini (ona, kwa mfano, Isaya 50:9; 51:3–5, 11–12, 22–23; 52:9–10)

Ninachoweza kufanya ili kufanya tumaini kuwa halisi (ona, kwa mfano, Isaya 50:10; 51:1–2, 6–9; 52:1–3, 9–11)

Ona pia Mosia 12:20–24; 15:13–18; 3 Nefi 20:29–46; Mafundisho na Maagano 113:7–10; Russell M. Nelson, “Kumbatia Siku za Usoni kwa Imani,” Liahona, Nov. 2020, 73–76.

Yesu ameubeba msalaba

Kwa Sababu ya Upendo, na Angela Johnson

Wasaidie wanafunzi kuja kwa Yesu Kristo. “Hakuna unachofanya kama mwalimu kitakacho wabariki wanafunzi zaidi kuliko kuwasaidia kumjua Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo na Kuhisi upendo Wao” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi8). Unapojiandaa kufundisha Isaya 50–57 kwa wengine, fikiria jinsi unavyoweza kuwasaidia kuona miunganiko kati ya changamoto za Israeli, unabii wa Isaya wa Kristo, na kupokea msaada wa kiungu kwa mapambano yao wenyewe.

Isaya 53

ikoni ya seminari
Yesu Kristo alijichukulia juu Yake dhambi zangu na huzuni zangu.

Ni sura chache katika maandiko zinaelezea ujumbe wa ukombozi wa Yesu Kristo kwa uzuri zaidi kuliko Isaya 53. Fikiria shughuli kama hizi ili kuelewa vyema na kutumia mafundisho haya yenye nguvu:

  • Tafakari au jadili jinsi hadithi na sinema mara nyingi huonyesha mashujaa wanaowaokoa watu. Tofautisha ufafanuzi huo na maelezo ya Mwokozi katika Isaya 53.

  • Baada ya kusoma kila mstari, pumzika ili kutafakari Mwokozi aliteseka nini—“huzuni,” “masikitiko,” na “makosa” Yeye aliyoyabeba—kwa ajili ya watu wote na hasa kwa ajili yako. Unaweza kubadlisha maneno kama “sisi” na “yetu” na “mimi” na “yangu” unaposoma. Je! ni hisia au mawazo gani mistari hii inakutia moyo?

  • Fikiria kutazama video “My Kingdom Is Not of This World” (Gospel Library), na tafakari jinsi unabii katika Isaya 53 ulivyotimia. Ni baadhi ya huzuni na masikitiko gani ambayo Mwokozi aliyabeba kwa ajili yetu?

    5:25

    My Kingdom Is Not of This World

  • Tafuta picha za matukio yanayohusiana na Upatanisho wa Yesu Kristo (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 56–60). Kisha ungeweza kutafuta virai katika Isaya 53 ambavyo vinaelezea matukio katika picha hizo. Je, mafundisho haya yanatupatia msukumo kufanya nini?

Ona pia “Tazama Mkombozi Afa,” Nyimbo za Dini, na. 104

Isaya 54; 57:15–19

Yesu Kristo ananitaka nirudi Kwake.

Sisi sote tuna nyakati ambapo tunahisi tuko mbali na Bwana kwa sababu ya dhambi zetu au madhaifu yetu. Baadhi hata wamekata tamaa kwamba Yeye hatawasamehe kamwe. Isaya 54 na57 ni sura nzuri za kusoma kwa uhakikisho na kutiwa moyo nyakati kama hizo. Hasa katika Isaya 54:4–10; 57:15–19, ni maneno gani yanakufundisha jinsi Mwokozi anavyohisi kukuhusu wewe? Kuna tofauti gani katika maisha yako kujua vitu hivi vinavyomhusu Yeye?

Rais Dieter F. Uchtdorf alifundisha:

“Bila kujali ni kiasi gani maisha yetu yanaweza kuonekana kuharibika. Bila kujali dhambi zetu ni nyekundu kiasi gani, uchungu mkubwa kiasi gani, wapweke kiasi gani, tumetelekezwa, au kuvunjika kwa mioyo yetu kunavyoweza kuwa. Hata wale wasio na matumaini, wanaoishi katika kukata tamaa, ambao wameusaliti uaminifu, wametelekeza uadilifu wao, au kugeukia mbali na Mungu wanaweza kujengwa upya. …

“Habari ya furaha ya injili ni hii: kwa sababu ya mpango wa furaha wa milele uliotolewa na Baba yetu wa Mbinguni mwenye upendo na kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, hatuwezi tu kukombolewa kutoka kwenye hali yetu ya anguko na kurejeshwa kwenye usafi, bali tunaweza pia kuvuka mawazo ya maisha ya kidunia na kuwa warithi wa uzima wa milele na washiriki wa utukufu usioelezeka wa Mungu” (“Atakubeba Mabegani Mwake na Kukupeleka Nyumbani,” Liahona, Mei 2016, 102).

Ona pia Patrick Kearon, “Kusudi la Mungu Ni Kukuleta Nyumbani,” Liahona, Mei 2024, 87–89.

Isaya 55–56

Bwana anawaalika wote “lishikeni agano langu.”

Kwa vizazi vingi, Israeli ilitambuliwa kama watu wa Mungu wa agano. Walakini, mpango wa Mungu umejumuisha zaidi ya taifa moja tu, kwani “kila aonaye kiu” amealikwa “njoni … majini” (Isaya 55:1). Weka hiliakilini unaposoma Isaya 55 na 56, na tafakari inamaanisha nini kuwa watu wa Mungu. Je! ni ujumbe gani wa Mungu kwa wale ambao wanahisi “wametengwa kabisa” kutoka Kwake? (Isaya 56:3). Fikiria kuwekea alama mistari inayoelezea mitazamo na matendo ya wale ambao “wanashikilia agano langu” (ona Isaya 56:4–7).

Kwa ziada, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .

ikoni ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Isaya 51–52

Bwana ananialika mimi “kujivika nguvu [yangu].”

  • Inaweza kuwa ya kufurahisha kwa watoto wako kugundua virai kama “amka,” “simama,” na “jivike nguvu zako” katika Isaya 51:9, 17; 52:1–2, 9 na kisha waigize virai hivyo. Baada ya kufanya hivyo, unaweza kuzungumza kuhusu kile inachomaanisha kuamka, kusimama, na kuvaa nguvu kiroho. Bwana anatuomba tufanye nini katika mistari hii?

  • Waalike watoto wasome Isaya 51:1, 4 na kubainisha nani Bwana anazungumza naye na nini Yeye anawataka wao wafanye. Je, nini maana ya “kumsikiliza” Bwana? Je, tunawezaje kumwonesha Bwana kwamba “tunamsikiliza” Yeye?

Isaya 53:3–9

Yesu Kristo alijichukulia juu Yake dhambi zangu na huzuni zangu.

  • Wewe na watoto wako mngeweza kuangalia picha kadhaa zinazoonyesha mateso na kifo cha Yesu Kristo (ona, kwa mfano, Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 56, 5758). Kisha mngeweza kusoma pamoja Isaya 53:3–6, 9 na mtafute maneno ambayo yanaelezea nini kinatokea katika picha hizo. Wasaidie watoto wako waelewe kwamba Isaya alishiriki kweli hizi mamia ya miaka kabla ya mambo kutokea. Kwa nini ingekuwa muhimu watu kujua mambo haya miaka mingi kabla? (ona Alma 39:15–19).

  • Baada ya kusoma kutoka Isaya 53:4, “Ameyachukua masikitiko yetu, na amejitwika huzuni zetu,” watoto wako wangeweza kujaribu kuinua kitu kizito (au kujifanya kukiinua). Eleza kwamba “masikitiko” na “huzuni” (au kukosa furaha) vinaweza kuonekana kuwa ni vizito na vigumu kubeba. Kwa nini Yeye aliteseka “masikitiko,” “huzuni,” na “maovu” au “dhambi”? (Ona pia Alma 7:11–12).

Yesu Kristo pamoja na watoto

Isaya 55:6

Ninaweza kumtafuta Bwana na kumlingana Yeye.

  • Ili kuwafundisha watoto wako kuhusu Isaya 55:6, ungeweza kuficha picha ya Yesu mahali fulani chumbani. Ungeweza kuwaalika watoto wako watafute picha na kutaja njia moja wanayoweza “kumtafuta … Bwana wakati anapoweza kupatikana.” Wimbo kama “Seek the Lord Early” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 108) ungeweza kuwapa baadhi ya mawazo. Kisha ungeweza kumruhusu mmoja wa watoto kuficha picha na kurudia shughuli hiyo.

Isaya 55:8–9

Njia za Bwana zi juu sana kuliko njia zangu.

  • Baada ya kusoma Isaya 55:9, inaweza kuwa burudani watoto wako kusimama kwenye kiti na kuzungumza kuhusu jinsi mambo yanavyoonekana tofauti unapokuwa “juu zaidi.” Au wangeweza kuchora picha ya kile Isaya 55:9 inamaanisha kwao. Ungeweza kujadili baadhi ya njia za Bwana ambazo ziko juu sana kuliko zetu. Kwa mfano, ni ipi njia Yake ya kuwatendea wenye dhambi? (ona Marko 2:15–17). Je, ni ipi njia Yake ya kuwaongoza wengine? (ona Mathayo 20:25–28). Waambie watoto jinsi ulivyojifunza kutumainia njia za juu na mawazo ya juu ya Bwana.

Kwa ziada, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.

picha ya Yesu

Nuru Yake, na Michael Malm

Ukurasa wa shughuli ya Watoto: ninaweza kumtafuta Bwana na kuliita jina Lake.