“Septemba 28–Octoba 4. ‘Watulizeni Mioyo, Watu Wangu’: Isaya 40–49,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)
“Septemba 28–Octoba 4. ‘Watulizeni Mioyo, Watu Wangu,’” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026
Kumponya Mtu Asiyeona, na Carl Heinrich Bloch, katika Makumbusho ya Frederiksborg ya Historia ya Kitaifa
Septemba 28–Oktoba 4: “Watulizeni Mioyo, Watu Wangu”
Isaya 40–49
“Watulizeni Mioyo” ni maneno ya kwanza ya Isaya sura ya 40. Inaashiria mwanzo wa sauti tofauti, mkazo tofauti katika ujumbe wa nabii. Maandishi ya awali ya Isaya yalionya Israeli na Yuda kuhusu maangamizo na utumwa ambavyo vingekuja kwa sababu ya dhambi zao. Lakini unabii huu wa baadaye ulikusudiwa kuwafariji Wayahudi zaidi ya miaka 150 katika siku zijazo—baada ya Yerusalemu na hekalu kuharibiwa na watu kuchukuliwa mateka na Babeli. Unabii huu hata hivyo, unafika hata mbali zaidi katika siku za usoni kuliko kwa Waisraeli walioshindwa, waliovunjika moyo. Unazungumza nasi, ambao wakati mwingine pia huhisi kushindwa, kuvunjika moyo, na hata kupotea.
Ujumbe wa Isaya kwao na kwetu ni rahisi: “Msiogope” (Isaya 43:1). Vyote havijapotea. Bwana hajakusahau, na Yeye ana nguvu juu ya hali ambazo zinaonekana kuwa nje ya udhibiti wako. Je, Bwana, ambaye “aliziumba mbingu” (Isaya 42:5), si mwenye nguvu zaidi kuliko Babeli, kuliko dhambi, kuliko chochote kinachokushikilia wewe utumwani? “Unirudie,” Yeye anasihi, “maana nimekukomboa.” (Isaya 44:22). Anaweza kuponya, kurejesha, kutia nguvu, kusamehe, na kufariji—chochote kinachohitajika kwako, kwa upande wako, ili kukombolewa.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Isaya 40–49
Yesu Kristo anaweza kunifariji na kunipa tumaini.
Wakati Waisraeli walipokuwa mateka katika Babeli, wengi wangeweza kujiuliza kama milele walikuwa wamepoteza nafasi yao kama watu wateule wa Mungu, watu wa agano. Unaposoma Isaya 40–49, tafuta vifungu ambavyo vingeweza kutoa faraja na tumaini. Kwa kila kifungu unachopata, tafakari na uandike kile Bwana anaweza kuwa anasema kwako katika mistari hii. Hapa kuna mistari michache ambayo unaweza kuanza nayo.
-
40:11, 29–31:
-
41:10–13, 17–18:
-
42:6–7:
-
43:1–7, 25:
-
44:1–4, 21–24:
-
46:3–4:
-
49:7–16:
Unahisi Bwana anakutaka wewe ujue nini kuhusu Yeye?
Unaweza kuona wimbo “Msingi Imara” (Wimbo, na. 85) unachukua maneno ya Isaya katika Isaya 41:10; 43:2–5; 46:4. Fikiria kuimba au kusikiliza wimbo huu, ukitafuta ulinganifu kati ya mashairi na mistari hii kutoka isaya. Ni kwa jinsi gani Bwana ametimiza ahadi katika msitari hii katika maisha yako?
Ona pia Patrick Kearon, “Amefufuka na Uponyaji katika Mbawa Zake: Tunaweza Kuwa Zaidi ya Washindi,” Liahona, Mei 2022, 37.
Tumia maandiko ya ziada. Wakati mwingine tunaweza kuelewa Agano la Kale vyema zaidi kama tutaongeza kujifunza kwetu kwa mistari kutoka Kitabu cha Mormoni. Kwa mfano, manabii wa Kitabu cha Mormoni Nefi na Yakobo walipata maandishi ya Isaya kwenye mabamba ya shaba (ona 1 Nefi 19:22–23), na walitumia unabii huu kufundisha kuhusu Mwokozi. Kujifunza jinsi Nefi na Yakobo walivyofananisha Isaya 48–49 kwa watu wao, ona 1 Nefi 22. Hiyo inaweza kukusaidia kufananisha sura hizi na maisha yako mwenyewe.
Kwa kumtii Bwana, tunaweza kuwa na “amani … kama mto” (Isaya 48:18).
Isaya 40–49
“Wewe ni mtumishi wangu;”
Kote katika Isaya 40–49 Bwana anazungumza juu ya “mtumishi” Wake na “mashahidi” Wake. Maneno haya yanaweza kumrejelea Yesu Kristo (ona Isaya 42:1–7), kwa nyumba ya Israeli (ona Isaya 45:4), na kwa Mfalme Koreshi, ambaye aliruhusu Wayahudi kurudi Yerusalemu na kujenga upya hekalu (ona Isaya 44:26–28; 45:1–4). Unaweza pia kufikiria jinsi vifungu hivi vinatumika kwako kama mtumishi na shahidi wa Bwana. Kwa mfano, tafakari maswali kama haya:
Isaya 40:1–3, 9–11; 43:1–12. Ni namna gani wewe umekuwa shahidi wa Yesu Kristo? Ni “habari njema” zipi ambazo unaweza kushiriki kama shahidi Wake? Unaweza kufikiria kwamba umeitwa kwenye kizimba cha ushahidi kusimama katika kesi mahakamani. Katika mashtaka haya, Yesu Kristo anashitakiwa kwa kudai kama ilivyoandikwa katika Isaya 43:11. Ni ushuhuda gani unaweza kutoa kuunga mkono madai ya Yesu? Ni ushahidi gani kutoka katika maisha yako ungewasilisha?
Isaya 41:8–13; 42:6; 44:21. Je! Bwana amekuita ufanye nini? Fikiria miito rasmi ya Kanisa pamoja na majukumu mengine ya agano ya kumtumikia. Ni kwa jinsi gani Yeye “amekuumba” au kukuandaa wewe kuwa mtumishi Wake? Ni kwa jinsi gani Yeye anakusaidia unapotumikia?
Isaya 49:1–9. Ni jumbe ganii unazipata katika mistari hii ambazo zinaweza kusaidia wakati juhudi zako na huduma zinaonekana kuwa “si kitu, na ni bure”? (mstari wa 4).
Isaya 40:3–8, 15–23; 42:15–16; 47:7–11
Nguvu za Mungu ni kubwa kuliko nguvu za ulimwengu.
Isaya aliwakumbusha watu wake mara kwa mara juu ya nguvu isiyo na kifani ya Mungu, hata ikilinganishwa na nguvu dhalimu ya kidunia iliyowazunguka. Tafuta ujumbe huu unaposoma Isaya 40:3–8, 15–23; 42:15–16; na 47:7–11 (kumbuka kwamba sura ya 47 imeelekezwa kwa mtekaji nyara wa Israeli, Babeli). Je, vifungu hivi vinakufundisha nini kuhusu mambo ya kilimwengu? Vinakufundisha nini kuhusu Mungu? Tafakari kwa nini ujumbe huu unaweza kuwa muhimu kwa watu Wayahudi walioko utumwani. Kwa nini ni wa thamani kwako?
Isaya 48–10; 49:13–16
Bwana anaweza kunitakasa kupitia mateso yangu.
Unaposoma Isaya 48:10, tafakari “tanuru la mateso.” Ni kwa jinsi gani Bwana “anakutakasa” wewe? Ni kwa jinsi gani Isaya 49:13–16 hutusaidia wewe wakati unapoteseka?
Ona pia “The Refiner’s Fire” (video), Gospel Library.
The Refiner's Fire
Kwa ziada, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Isaya 40:3–5
Ninaweza kusaidia kuandaa “njia ya Bwana.”
-
Fikiria baadhi ya njia za kuelezea kile inachoweza kumaanisha “kuiandaa … njia ya Bwana,” kama ilivyoelezewa katika Isaya 40:3–5. Kwa mfano, wewe na watoto wako mngeweza kunyoosha kitu ambacho kimevunjika, kusafisha sakafu iliyojaa, au kutengeneza njia iliyo wazi kwenye ardhi ya miamba. Pia ungeweza kuonyesha picha za Yohana Mbatizaji na Joseph Smith (ona Kitabu cha Sanaa cha Injili, na. 35,87). Je, waliandaaje njia kwa ajili ya ujio wa Bwana? (ona Luka 3:2–18; Mafundisho na Maagano 135:3). Ni kwa jinsi gani sisi tunaweza kusaidia? Hii inaweza kuwa fursa ya kuzungumza kuhusu jinsi wenye Ukuhani wa Haruni wanavyosaidia kuandaa njia ya Bwana (ona Mafundisho na Maagano 84:26–28).
Isaya 43:10
Ninaweza kuwa shahidi wa Bwana.
-
Baada ya kusoma Isaya 43:10 pamoja, mnaweza kuzungumza kuhusu kile inachomaanisha kuwa shahidi. Shiriki na kila mmoja mambo uliyopitia ambayo unaweza kuwa “shahidi” wa—kwa mfano, chakula ulichoonja, sehemu uliyotembelea, au mtu unayemjua. Je, ina maana gani kuwa shahidi wa Bwana? Tunaweza kuwaambia nini watu wengine kumhusu Yeye?
Isaya 44:3-4; 45:8
Bwana “atanimwagia” baraka Zake.
-
Baada ya kusoma mistari hii, watoto wako wanaweza kumwagilia mmea wanapozungumza juu ya baraka ambazo Bwana amemwaga juu yao. Ni nini kinachotokea kwa mmea wakati unamwagiliwa maji? Ni kwa jinsi gani baraka za Bwana zimetusaidia kukua?
“Haki yetu [inaweza kuwa] kama mawimbi ya bahari” (Isaya 48:18).
Isaya 48:17–18
Kutii amri za Mungu kunaleta amani.
-
Picha au video za mito na mawimbi ya bahari zingeweza kuwasaidia watoto wako wapate taswira ya Isaya 48:18 (kama vile picha katika muhtasari huu). Watoto wako wangeweza kufurahia kusogeza mikono yao na mikono kama mto na mawimbi ya bahari. Amani inawezaje kuwa kama mto vipi? Je, wema unawezaje kuwa kama mawimbi? Zungumza kuhusu jinsi kutii amri za Mungu kulivyokusaidia kuhisi amani kama mto au imara kama mawimbi.
-
Imbeni pamoja wimbo kuhusu amri, kama vile “Keep the Commandments” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146–47). Wimbo huu unafundisha nini kuhusu kwa nini tunapaswa kutii amri za Mungu?
Isaya 49:14–16
Bwana kamwe hatanisahau mimi.
-
Isaya 49:14–16 inaweza kuwa faraja kubwa kwa watoto wako kwa miaka ijayo. Unaposoma mstari wa 14, ungeweza kuzungumza kuhusu nini kinaweza kuwafanya watu wahisi kusahaulika au kutelekezwa. Je, tunajuaje kuwa Bwana hajatusahau?
-
Ili kutambulisha mstari wa 15–16, ungeweza kuwauliza watoto wako kuhusu mtu ambaye kamwe hawatamsahau, kama mwanafamilia au rafiki. Kulingana na Isaya 49:15–16, kwa nini Bwana kamwe hatatusahau sisi? Kisha mngeweza kushiriki hisia zenu kuhusu Yesu Kristo.
Kwa ziada, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .