“Septemba 21–27. ‘Kazi ya Ajabu na Muujiza’: Isaya 13–14; 22; 24–30; 35,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)
“Septemba 21–27. ‘Kazi ya Ajabu na Muujiza ,’” Njoo, Unifuate: 2026
Kijisitu Kitakatifu, na Brent Borup
Septemba 21–27: “Kazi ya Ajabu na Muujiza”
Isaya 13–14; 22; 24–30; 35
Jambo moja ambalo Bwana huwaomba manabii kufanya ni kuonya juu ya matokeo ya dhambi. Kwa manabii wa Agano la Kale, hii mara nyingi ilimaanisha kuwaambia watawala wa falme zenye nguvu kwamba walihitaji kutubu. Ilikuwa ni kazi ya hatari, lakini Isaya hakuwa na woga, na maonyo yake kwa falme za siku zake—zikiwemo Israeli, Yuda, na mataifa jirani—yalikuwa ya ujasiri (ona Isaya 12–23).
Hata hivyo, Isaya pia alikuwa na ujumbe wa matumaini. Ijapokuwa uharibifu uliotabiriwa mwishowe ulikuja juu ya falme hizi, Isaya aliona nafasi ya urejesho na kufanywa upya. Bwana angewaalika watu Wake warudi Kwake. Angefanya “mchanga ung’aao … utakuwa ziwa la maji, na nchi yenye kiu itakuwa chemchemi za maji” (Isaya 35:7). Angefanya “kazi ya ajabu na mwujiza” (Isaya 29:14), kurejesha kwa Israeli baraka ambazo Yeye aliwaahidi. Si Isaya wala mtu yeyote aliye hai kwa wakati huo aliishi kuona kazi hii ya ajabu. Lakini sisi tunaiona leo. Ukweli ni kwamba, sisi ni sehemu yake.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Isaya 13:1–11, 19–22; 14:1–20
Kiburi na mambo ya kiulimwengu vitashindwa.
Katika siku za Isaya, Babeli ilikuwa ufalme wenye nguvu wenye mtawala aliye na nguvu. Sasa Babeli ni historia ya kale. Kwa nini ujumbe wa Isaya kwa Babeli, katika Isaya 13–14, ni muhimu kwetu leo? Kwa sababu Babeli inaashiria kiburi, uchoyo, na dhambi, mambo ambayo bado yanatuzingira leo. Fikiria kuhusu ishara hii unaposoma Isaya 13:1–11, 19–22; 14:1–20. Ungeweza pia kufikiria maswali kama haya:
-
Je, ni kufanana gani unakokuona kati ya kiburi cha mfalme wa Babeli na kiburi cha Shetani? (ona Isaya 14:4–20; Musa 4:1–4). Ni maonyo gani unayapata kwa ajili yako mwenyewe katika mistari hii?
-
Je! Mwokozi hutoaje “raha baada ya huzuni yako, na baada ya taabu yako”? (Isaya 14:3).
“Yeye ataimeza mauti katika ushindi” (Isaya 25:8).
Isaya 22:22–23; 24:21–23; 25:6–8; 26:19; 28:16
Yesu Kristo ndiye Masiya mwahidiwa.
Mafundisho ya Isaya mara nyingi yanarejea huduma ya Mwokozi, pamoja na dhabihu Yake ya upatanisho, Ufufuo, na Ujio wa Pili. Ni mambo gani ya huduma Yake yanayokuja akilini unaposoma mistari ifuatayo: Isaya 22:22–23; 24:21–23; 25;6–8; 26:19; 28:16? Je, ni vifungu gani vingine ambavyo vinakukumbusha juu ya Mwokozi?
Wape wanafunzi fursa za kutoa ushuhuda juu ya Yesu Kristo. “Kuwa mwalimu wa injili ya Yesu Kristo inamaanisha kuwasaidia wengine kuelewa na kuyategemea mafundisho Yake, nguvu ya kukomboa, na upendo mkamilifu” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi;8). Njia moja rahisi ya kufanya hivyo kila wakati unapofundisha ni kuuliza swali kama “Ulipata nini katika maandiko wiki hii ambacho kilikufundisha kitu fulani kuhusu Mwokozi?” Kisha waruhusu wanafunzi washiriki uzoefu wao na kuimarisha imani ya kila mmoja wao.
Isaya 24:1–12; 28:1–8; 29:7–13; 30:8–14
Kugeukia mbali na Mungu huleta hatari ya kiroho.
Kwa rehema Zake, Bwana alimtuma Isaya kuwaonya watu wa agano kwamba walikuwa wanapotoka kutoka Kwake. Ona kama unaweza kupata ishara za onyo la kiroho la hili katika Isaya 24:5; 29:13; 30:8–12. Kwa nini mitazamo na vitendo hivi ni hatari kiroho?
Ili kuonya kuhusu matokeo ya kugeuka kutoka kwa Bwana, Isaya alitumia baadhi ya milinganisho ya kukumbukwa. Unapojifunza, jiulize jinsi kugeuka kutoka kwa Bwana kunavyokuwa:
-
Dunia yenye huzuni, iliyo tupu (Isaya 24:1–12).
-
Kileo (Isaiah 28:7–8).
-
Njaa na kiu (Isaya 29:7–10).
-
Ukuta au chombo kilichovunjika (Isaya 30:13–14).
Kwa nini ni muhimu kwako kuwa karibu na Bwana?
Isaya 29; 30:18–26; 35
Bwana anaweza kurejesha kile kilichopotea au kuvunjika.
Je, umewahi kupoteza kitu ambacho ulifikiri kamwe hungekipata tena? Au labda kitu kilivunjika, na una wasiwasi kwamba hakiwezi kufanyiwa ukarabati. Tunapogeukia mbali na Bwana, Shetani anataka tufikirie kwamba kamwe hatuwezi kurudi au kuponywa. Walakini, Isaya alielezea mambo mazuri ambayo Bwana atayafanya kutusaidia kurudia Kwake. Unajifunza nini kutoka katika Isaya 29:13–24; 30:18–26;35 kumhusu Bwana, upendo Wake, na nguvu Zake? Pengine ungeweza kupata kirai katika vifungu hivi ambacho kinakupa tumaini wakati unapohitaji uponyaji. Ungeweza pia kuangalia katika ujumbe wa Dada Amy A. Wright “Kristo Anaponya Kile Kilichovunjika” (Liahona, Mei 2022, 81–84).
Njia moja Bwana anadhihirisha nguvu Zake na rehema Zake ni kupitia Urejesho wa injili Yake. Isaya 29 ina vifungu kadhaa ambavyo vina kwenda sambamba na matukio ya Urejesho huo. Kwa mfano:
-
Linganisha Isaya 29:11–12 na 2 Nefi 27:6–26 na Joseph Smith—Historia 1:63–65.
-
Linganisha Isaya 29:13–14 na Mafundisho na Maagano 4 na Joseph Smith—Historia 1:17–19.
-
Linganisha Isaya 29:18–24 na ukurasa wa Jina wa Kitabu cha Mormoni.
Kwa maoni yako, kwa nini “ni ya ajabu” na “mwujiza” (Isaya 29:14) maneno mazuri ya kumwelezea Bwana kurejesha injili Yake? Ni kwa jinsi gani unaweza kusaidia kutimiza unabii kuhusu Urejesho? Kwa ajili ya mawazo, angalia katika ujumbe wa Mzee Gerrit W. Gong “Mataifa Yote, Kabila, na Lugha” (Liahona, Nov. 2020, 38–41).
Ona pia “Urejesho wa Utimilifu wa Injili ya Yesu Kristo: Tangazo kwa Ulimwengu la Maadhimisho ya Miaka Mia Mbili,” Maktaba ya Injili; “Asubuhi Kunakucha,” Nyimbo za Dini, na 1.
Kwa ziada, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Isaya 14:3; 25:8–9; 28:16
Yesu Kristo anaweza kuniokoa kutokana na dhambi na kifo.
-
Ni kwa jinsi gani utawasaidia watoto wako wamwone Mwokozi katika maandiko ya Isaya? Unaweza kuwasaidia watafute virai ambavyo vinawakumbusha juu Yake katika Isaya 14:3; 25:8; au 28:16. Wangeweza pia kuoanisha mistari hii kutoka kwa Isaya na mistari mingine ambayo inafundisha kuhusu Mwokozi, kama vile Mathayo 11:28–30; 1 Wakorintho 15:53–57; Helamani 5:12. Je, ni mambo gani makuu Bwana amefanya kwa ajili yetu?
-
Baada ya kusoma Isaya 25:8–9 pamoja, mngeweza kuangalia picha za Mwokozi akiwa Gethsemane, msalabani, na baada ya Ufufuko Wake. Acha watoto wako wazungumze kuhusu kile kinachotendeka katika picha na kwa nini wanampenda Yesu na “kufurahia wokovu wake” (mstari wa 9).
-
Unaweza kuchagua kuwaambia watoto wako kuhusu huzuni uliyohisi wakati mtu unayempenda alipofariki. Shuhudia juu ya faraja unayopokea kwa sababu ya Yesu Kristo. Pengine watoto wako wangeweza kuchora uso unaolia na kisha kufuta machozi mnaposoma Isaya 25:8 pamoja.
Mapenzi Yako Yatimizwe, na Ken Spencer
Isaya 25:4–6
Yesu ananipa “kimbilio kwenye dhoruba.”
-
Je, wewe na watoto wako mmewahi kupata baraka ya makazi salama wakati wa dhoruba au kivuli siku ya majira ya joto? Au umewahi kufurahia chakula kizuri ulipokuwa na njaa? Zungumza kuhusu uzoefu huu unaposoma Isaya 25:4–6. Ni kwa jinsi gani Yesu ni kama vitu hivi?
Isaya 29:11–18, 24
Urejesho wa injili ni “kazi ya ajabu.”
-
Wewe na watoto wako mnaposoma Isaya 29:14, shiriki nao maneno mengine ambayo yana maana sawa na “ajabu” na “mwujiza.” Waache wakusaidie kutafuta vitu au picha ambazo zinawakilisha baadhi ya kazi za ajabu za Bwana wakati wa siku za mwisho. Hizi zinaweza kujumuisha nakala ya Kitabu cha Mormoni, picha ya hekalu, au picha ya Ono la Kwanza (kuna moja mwanzoni mwa muhtasari huu). Kisha watoto wako wangechagua kitu kimoja na kushiriki kwa nini ni cha ajabu kwao.
-
Wimbo kuhusu Urejesho wa injili ungeweza kwenda vizuri pamoja na Isaya 29, kama vile “On a Golden Springtime” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 88). Na pengine uzoefu binafsi ungeweza kuwasaidia watoto kuelewa urejesho humaanisha nini. Kwa mfano, wewe na watoto wako mngeweza kuzungumza kuhusu kitu fulani ambacho ulikipoteza na jinsi ulivyokipata. Wasaidie watoto wako walinganishe hili na Urejesho wa injili. Kulingana na Isaya 29:13–15, kwa nini tunahitaji Urejesho? Ni kazi gani za ajabu Bwana anafanya ili kurejesha injili Yake? (ona ukurasa wa shughuli ya wiki hii).
Kwa ziada, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.