Maandiko hutumia maneno haya katika njia mbili. Katika maana moja, sisi wote ni watoto halisi wa kiroho wa Baba wa Mbinguni. Katika maana nyingine, wana na mabinti za Mungu ni wale waliozaliwa tena kwa njia ya Upatanisho wa Kristo.
Sisi wazao wa Mungu, Mdo. 17:29 .
Tujitie chini ya Baba wa roho, Ebr. 12:9 .
Watoto waliozaliwa tena kupitia Upatanisho
Kadiri wengi walivyompokea aliwapa uwezo wa kuwa wana wa Mungu, Yn. 1:12 (Rum. 8:14 ; 3 Ne. 9:17 ; M&M 11:30 ).
Sasa tu wana wa Mungu, 1 Yoh. 3:1–2 .
Mtaitwa watoto wa Kristo, wana na mabinti zake, Mos. 5:7 .
Watu wote ni lazima wazaliwe tena, ili kuwa wana na mabinti zake, Mos. 27:25 .
Watakuwa wana wangu na mabinti zangu, Eth. 3:14 .
Wewe hakika utafanyika mtoto wa Kristo, Moro. 7:19 .
Wale wote wenye kuipokea injili yangu ni wana na mabinti, M&M 25:1 .
Wao ni miungu, hata wana wa Mungu, M&M 76:58 .
Hivyo wote wapate kufanyika wana wangu, Musa 6:68 .
Wengi wameamini na wamekuwa wana wa Mungu, Musa 7:1 .