Mwana wa Zakaria na Elizabethi katika Agano Jipya. Yohana alitumwa kuwaandaa watu kwa kumpokea Masiya (Yn. 1:19–27 ). Alishikilia funguo za Ukuhani wa Haruni na alimbatiza Yesu Kristo.
Aliwekwa gerezani na akakatwa kichwa, Mt. 14:3–12 (Mk. 6:17–29 ).
Gabrieli alitangaza kuzaliwa na huduma ya Yohana kwa Zakaria, Lk. 1:5–25 .
Yesu alifundisha kuwa Yohana Mbatizaji alikuwa nabii mkuu, Lk. 7:24–28 .
Alimtambua Yesu kama ni Mwana wa Mungu, Yn. 1:29–34 .
Wanafunzi wa Yohana wakaja kuwa wanafunzi wa Yesu, Yn. 1:25–29, 35–42 (Mdo. 1:21–22 ).
Hakufanya muujiza, Yn. 10:41 .
Kama mtu mfufuka, alitumwa kuwatawaza Joseph Smith na Oliver Cowdery katika Ukuhani wa Haruni, M&M 13 (M&M 27:7–8 ; JS—H 1:68–72 ).
Alitawazwa na malaika wakati alipokuwa na umri wa siku nane, M&M 84:28 .