Vipawa vya Roho Ona pia Karama Baraka maalumu zitolewazo na Bwana kwa watu wenye kustahili kwa manufaa yao wenyewe na kuvitumia kwa ajili ya kuwabariki wengine. Kwa maelezo juu ya vipawa vya Roho, jifunze Mafundisho na Maagano 46:11–33; 1 Wakorintho 12:1–12; Moroni 10:8–18. Takeni kwa dhati karama zilizo bora, 1 Kor. 12:31 (1 Kor. 14:1). Wanefi walipewa vipawa vingi vya Roho, Alma 9:21. Ole wake asemaye Bwana hatendi kazi tena kwa vipawa au kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, 3 Ne. 29:6. Mungu hutoa vipawa kwa walio waaminifu, Morm. 9:7. Vipawa huja kwa Roho wa Kristo, Moro. 10:17. Kuna vipawa vingi na kwa kila mtu kimetolewa vipawa vya Roho, M&M 46:11. Viongozi wa Kanisa wanapewa uwezo wa kupambanua vipawa vya Roho, M&M 46:27. Rais wa Kanisa anavyo vipawa vyote ambavyo Mungu huviweka juu ya kichwa cha kiongozi wa Kanisa, M&M 107:91–92.