Liahona Katika Kitabu cha Mormoni, ni mpira wa shaba nyeupe wenye mishale miwili yenye kuonyesha mwelekeo—kama vile dira—na pia maelekezo ya kiroho kwa Lehi na wafuasi wake wakati walipokuwa waaminifu. Bwana aliwapa Liahona na kutoa maelekezo kupitia hiyo. Lehi aliona mpira wa shaba nyeupe wenye mishale miwili iliyoonyesha njia ambayo Lehi na familia yake walipaswa kwenda, 1 Ne. 16:10. Mpira ulifanya kazi kulingana na imani na bidii, 1 Ne. 16:28–29 (Alma 37:40). Benjamini alimpa Mosia mpira, Mos. 1:16. Mpira au mwelekezi kiliitwa Liahona, Alma 37:38. Liahona ilifananishwa na neno la Kristo, Alma 37:43–45. Mashahidi Watatu wa Kitabu cha Mormoni watamwona mwelekezi aliyepewa Lehi, M&M 17:1.