“Agosti 10–16. ‘Bado Nitamtumainia Yeye’: Ayubu 1–3; 12–14; 19; 21–24; 38–40; 42,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Agano la Kale 2026 (2026)
“Agosti 10–16. ‘Bado Nitamtumainia Yeye,’” Njoo, Unifuate: Agano la Kale 2026
Hukumu za Ayubu, na Joseph Brickey
Agosti 10–16: “Bado Nitamtumainia Yeye”
Ayubu 1–3; 12–14; 19; 21–24; 38–40; 42
Ni kawaida kujiuliza kwa nini mambo mabaya hutokea kwa watu wazuri—au kwa maana hiyo, kwa nini mambo mazuri hutokea kwa watu wabaya. Kwa nini Mungu, ambaye ni mwenye haki, anaruhusu hayo. Kitabu cha Ayubu kinachunguza maswali kama haya. Ayubu alikuwa mmoja wa watu wema ambao mambo mengi mabaya yalitokea. Kwa sababu ya majaribu ya Ayubu, marafiki zake walijiuliza kama yeye kweli alikuwa mtu mzuri baada ya yote hayo. Ayubu alithibitisha uadilifu wake mwenyewe na kujiuliza ikiwa kweli Mungu alikuwa mwenye haki kwa wote. Lakini licha ya mateso yake na kujiuliza, Ayubu alidumisha uadilifu wake na imani katika Yesu Kristo. Katika kitabu cha Ayubu, imani inapimwa na kujaribiwa lakini haiachwi kabisa. Hii haimaanishi maswali yote yanajibiwa. Lakini kitabu cha Ayubu kinafundisha kwamba mpaka yatakapojibiwa, maswali yanaweza kuishi pamoja na imani. Na bila kujali nini kinatokea wakati huu, tunaweza kusema juu ya Bwana wetu, “Bado nitamtumainia yeye” (Ayubu 13:15).
Kwa ajili ya muhtasari wa kitabu cha Ayubu, ona “Ayubu” katika Mwongozo wa Maandiko (Maktaba ya Injili).
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Ayubu 1–3; 12–13
Tunaweza kumtumainiai Mungu katika hali zote.
Sura za ufunguzi za Ayubu zinasisitiza, katika njia ya kishairi, jukumu la Shetani kama adui au mshitaki wetu; hawaelezei mwingiliano halisi kati ya Mungu na Shetani. Unaposoma kile Shetani alichosema kuhusu Ayubu (ona Ayubu 1:9–11; 2:4–5), ungeweza kujiuliza, “Kwa nini ninabaki mwaminifu kwa Mungu?” Kwa nini ingekuwa hatari kumtii Bwana kwa sababu tu alizopendekeza Shetani?
Ni nini kinachokuvutia kuhusu majibu ya Ayubu kwa majaribu yake? (ona Ayubu 1:20–22; 2:9–10).
Marafiki wa Ayubu walipendekeza kwamba Mungu alikuwa akimwadhibu (ona Ayubu 4–5; 8; 11). Ni matatizo gani unayoyaona kwa wazo hili? Soma jibu la Ayubu katika sura ya 12–13. Ayubu alijua nini kuhusu Mungu ambacho kilimwezesha kuendelea kutumaini? Unafahamu nini kuhusu Mungu ambacho hukusaidia kukabiliana na changamoto?
Ayubu 19
Yesu Kristo ni Mkombozi wangu.
Wakati mwingine tunajifunza kweli muhimu zaidi wakati wa nyakati zetu ngumu sana. Tafakari majaribu Ayubu aliyoyaelezea katika Ayubu 19:1–22 na kweli alizozitangaza katika mstari wa 23–27. Unajuaje kuwa Mkombozi wako yu hai? Je! Maarifa haya yanaleta tofauti gani katika maisha yako?
Fikiria kuimba au kusikiliza wimbo kuhusu Yesu Kristo, kama vile “Najua Kristo Yu Hai” (Nyimbo za Dini, na.68). Ni maneno gani kutoka kwenye wimbo huu yanaelezea hisia zako kumhusu Yeye?
Ona pia Mafundisho na Maagano 121:1–12;122.
Ayubu 21–24
“Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.”
Katika Ayubu 21–24, utasoma mjadala kati ya Ayubu na rafiki zake. Katika kiini cha mjadala huu lilikuwa swali watu wengi wameuliza: Kwa nini watu wenye haki wakati mwingine wanateseka?
Ingawa hatuna majibu yote, katika injili ya urejesho ya Yesu Kristo, tuna baadhi ya kweli ambazo zinaweza kutusaidia kuleta maana ya dhiki na mateso. Hapa chini ni maandiko ya siku za mwisho ambayo yana baadhi ya kweli hizi. Maandiko haya yanatufundisha nini kuhusu Baba wa Mbingu na mpango Wake?
Ungeweza pia kusoma mafundisho ya Rais Spencer W. Kimball kuhusu dhiki katika “Janga au Hatima?” (Teachings of Presidents of the Church: Spencer W. Kimball [2011]), 11–21).
Kulingana na kile ulichojifunza, unawezaje kujibu swali kama “Kwa nini Mungu huruhusu watu wenye haki kuteseka?”
Utulivu na Nyota, na Yongsung Kim. Picha kwa hisani ya havenlight.com
Ayubu 38–40; 42
Mtazamo wa Mungu ni mkubwa kuliko wangu.
Akikanganywa na shutuma za rafiki zake (ona Ayubu 16:1–5; 19:1–3), Ayubu alimwuliza Mungu mara kwa mara kwa nini alipaswa kuteseka sana (ona Ayubu 19:6–7; 23:1–9; 31). Bwana hakutoa sababu ya wazi katika kitabu cha Ayubu. Lakini Yeye alifundisha ujumbe muhimu katika sura ya 38–40. Ni kwa jinsi gani ungeweza kufanyia muhtasari ujumbe huo? Kwa mfano, unajifunza nini kutokana na maswali ya Bwana katika Ayubu 38:1–7, 18–24?
Utagundua kwamba Bwana alizungumza na Ayubu kuhusu baadhi ya viumbe Vyake na matendo mengine makuu (ona Ayubu 38–39). Unaweza kutazama baadhi ya viumbe hivyo (au picha zake). Ni kwa jinsi gani vitu hivi vinakusaidia kufikiria tofauti kuhusu Mungu? kuhusu majaribu yako? Ni kwa jinsi gani vilibadilisha mtazamo wa Ayubu? (ona Ayubu 42:1–6; ona pia Musa 1:8–10).
Hapa kuna jumbe mbili za mkutano mkuu ambazo zinaweza kusaidia kubadili mtazamo wetu: Tamara W. Runia, “Kuona Familia ya Mungu kupitia Lenzi ya Ujumuishi” (Liahona, Nov. 2023, 62–69); Russell M. Nelson, “Fikiria Selestia!” Liahona, Nov. 2023, 117–20). Katika ujumbe wo wote, tafuta kitu ambacho utataka kukumbuka wakati ujao majaribu yako yanapoonekana kukuzidia. Ni kwa jinsi gani utajikumbusha juu ya kile ulichojifunza?
Kuwa mbunifu. Kujifunza hakupaswi tu kujumuisha kusoma, kufikiri, na kuzungumza. Wakati mwingine kujifunza kwa kukumbukwa huja kwa njia za kimwili za kushiriki kikamilifu. Kwa mfano, unaposoma kuhusu jinsi Bwana alivyobadilisha mtazamo wa Ayubu katika Ayubu 38–40, ungeweza kutembea na kuangalia baadhi ya viumbe vya Bwana, vikubwa na vidogo. Au ungeweza kuangalia kitu kutoka mitazamo tofauti—kutoka juu, chini, karibu, mbali sana, na kadhalika.
Kwa zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Ayubu 1–2; 12; 19
Imani katika Yesu Kristo itanisaidia katika nyakati ngumu.
-
Wahimize watoto wako wakuambie kile wanachojua kuhusu kuzaliwa Ayubu. Kama wanahitaji msaada, ungeweza kuwaelekeza kwenye Ayubu 1:1, 13–22; 2:7–10 au “Ayubu” (katika Hadithi za Agano la Kale, 145–47). Je, ni jinsi gani Ayubu alijibu changamoto? (ona Ayubu 1:21; 2:10).
1:55Job
-
Ayubu alikuwa mwaminifu katika changamoto zake kwa sababu ya kile alichojua kuhusu Bwana. Pengine wewe na watoto wako mngeweza kutazama picha za Yesu Kristo mkijumuika na wengine (kama zile zilizopo hapa chini au picha katika Kitabu cha Sanaa ya Injili). Zungumza kuhusu kile unachojua kuhusu Yeye na vile Yeye alivyo. Hapa kuna baadhi ya mistari inayoonyesha kile Ayubu alichojua kuhusu Bwana: Ayubu 12:10, 13, 16; 19:25–27. Kwa nini ni muhimu kujua kuhusu vitu hivi kumhusu Yeye?
Aliwaponya Wote, na Michael Malm
Ayubu 14:14
Kwa sababu ya Yesu Kristo, mimi nitaishi tena baada ya kufa.
-
Ayubu aliuliza swali muhimu katika Ayubu 14:14. Pengine wewe na watoto wako mngeweza kufanya zamu kushiriki jinsi utakavyomjibu Ayubu. Ungeweza kutafuta mawazo katika Alma 11:42–44, katika video “In a Coming Day” (Gospel Library), au katika wimbo kuhusu Ufufuo, kama vile “Did Jesus Really Live Again?” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 64).
#BECAUSEofHIM: An Easter Message of Hope and Triumph
Ayubu 16:1–5; 22:5–11
Marafiki wema huinuana na kutiana moyo wao kwa wao.
-
Wakati Ayubu alikuwa na huzuni, marafiki zake walisema kwamba Mungu alikuwa anamhadhibu kwa sababu alikuwa ametenda dhambi (ona Ayubu 22:5). Kama tungekuwa marafiki wa Ayubu, ni kwa jinsi gani tungejaribu kumsaidia? Ni kwa jinsi gani maneno yetu yanawasaidia wengine wanapokuwa na huzuni? (ona Ayubu 16:5). Fikiria kuonyesha picha moja au zaidi katika muhtasari huu unapojadili maswali haya.
-
Fikiria kuwaomba watoto wako waorodheshe baadhi ya sifa za rafiki mwema na wamtaje rafiki mwenye sifa hizi. Kisha ungeweza kutazama picha ya Yesu Kristo. Ni kwa njia gani Yesu ni rafiki mwema wa kila mmoja wetu? Unaweza kufikiria juu ya mtu ambaye anapitia wakati mgumu. Panga jinsi utakavyokuwa rafiki kama Kristo kwao.
Ayubu 19:23–27
Yesu Kristo ni Mkombozi wangu.
-
Baada ya kusoma Ayubu 19:23–27, wewe na watoto wako mngeweza kuzungumza kuhusu jinsi mnavyojua kwamba Mkombozi wetu yu hai. Mngeweza kufanya kazi kwa pamoja kuweka ushuhuda wenu (au michoro wa Mwokozi) katika kitabu, kama vile shajara ya familia (ona mstari wa 23).
-
Mngeweza pia kuimba wimbo ambao unamshuhudia Mwokozi, kama vile “I Know That My Redeemer Lives” (Nyimbo za Dini, na.136). Shiriki virai kutoka kwenye wimbo ambavyo vinaimarisha imani yako Kwake. Kwa nini ni muhimu kujua kwamba Yesu Kristo yu hai?
Kwa ziada, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .